Pongezi kwenu Single Mothers
Ni kweli mkuu. Ila sina wasi wasi nae kabisa, anajitambua sana. Huwa ananambia wanaume wengi wanatuogopa kwa sababu wanahisi tutawacheat na ma x wetu jambo ambalo linategemea na akili na utashi wa mtu.
Unakosea kusema anajitambua sana. Kukaa nae wiki hakutoshi kusema anajitambua sana. Jiulize huyo mzazi mwenzake amekaa nae muda gani vipi hajaliona hilo. Anawezaje kumuacha mwanamke aliyeweza kuingia leba kwa ajili yake ili apanue ukoo wake kama kweli ni.mtu anayejitambua n kueleweka sana. Mkuu weka akiba ya maneno.
N pia mjini njaa kali mzee baba mtu akijichangnya kutaka kukulipia pango chakula matibabu n dharura zingine kwanini utajirahisishe tu. Mjini akili humu
 
Uzi wako malengo yake nayafahamu.Nakushauri tu uache kuleta siasa za Alinacha
 
Mtazamo!
Jamii za kiafrika, zina mitazamo hasi kuhusu Single mother........
 
kelele zote hizi kumbe hata ndoa bado. Oa kwanza ndio uje kutoa somo kidogo unaweza kueleweka.
 
Write your reply...we jamaa ni fala Sana embu jaribu kutuskiliza sisi wanaume wenzako tunajua tuliyokutana nao tunajua uchungu wako usipotusikiliza sisi utamsikiliza Nani?
angalia kwa akili ya kawaida wengi wanakwambiaje? na siku zote wengi wape hao wanaume wanakushauri usitusikilize hawataki kuumia peke yao wengi wameumizwa wengi hawakutakii mema na wengi wanao kusapoti ni wanawake hii Mada inamuhusu mwenzao unataka wafanyaje?
mkuu lisemwalo lipo Kama halipo lajaa we hivi vitu hujawahi kuvishuhudia in real life ila sisi tumewahi hivi inamaana unataka uniambie pia ujawahi kuona hata nyuzi za mrejesho kuhusu hili swala?
we unadhani wazazi wako watajiskiaje sema tu ukwel wanaskia mwanao kaoa mwanamke mwenye mtoto unadhani watajiskiaje? kweli umeshindwa utafute binti kigori uanze nae familia unaenda oa demu alienda mzalisha mwenzako yaani mke wa mwanaume mwenzio?
embu jifikirie Mara mbilimbili akili yako haiko sawa au amekuroga nini
Kupenda ndugu yangu, nampenda sana hapo sijui nifanyeje.
 
Daniel Adrian,
Wewe endelea na maisha yako na mtarajiwa wako, usikatishwe tamaa na ushauri hasi unaotolewa humu jf.
Maisha ya ndoa kitu cha kwanza unamtanguliza YESU KRISTO, pili maisha ya ndoa ni nyinyi kuwa na lugha moja na kupatana katika kila jambo . Kuaminiana na uwazi hapo mtafanikiwa sana kwenye maisha yenu.
Nikwambie jambo mkuu, ndoa ni "paradiso hakika" , mkiweza kuwa na mawasiliano mazuri na ya karibu yenye uwazi.
Kuwa na mtoto wala hakuna tatizo , wewe mpende tena toka moyoni mwako mkubali kuwa ni mwanao, haijalishi baba yake yupo hai au amefariki.
Na mtoto anapokosea wewe ongea na vizuri tu kama baba yake na kumweleza kipi kizuri na kipi kibaya muda ule ule anapokuwa amekosea , kupiga kuchapa siyo siyo dawa ya kumrekebisha mtoto.
Penda kuwa na muda mwingi na familia na siyo marafiki.
Familia ndiyo kila kitu.
Angalizo: ndoa nyingi zinaharibika mmoja wapo anapoanza kuchepuka. Ambako kuna sababishwa na kununiana, kutokuwa na mawasiliano mazuri toka asubuhi mpaka jioni, kutokuheshimiana, mazoea ndiyo hasa yanaharibu sana ndoa.
Jitahidi kumfanya mkeo mpya kila siku.
Hata kama hamjui mapenzi muwe wazi mfundishane. Msioneane aibu.
Mzee wa Msoga alisema akili za kuambiwa changanya na zako mambo yanaenda.
Asante sana ndugu.
 
Unakosea kusema anajitambua sana. Kukaa nae wiki hakutoshi kusema anajitambua sana. Jiulize huyo mzazi mwenzake amekaa nae muda gani vipi hajaliona hilo. Anawezaje kumuacha mwanamke aliyeweza kuingia leba kwa ajili yake ili apanue ukoo wake kama kweli ni.mtu anayejitambua n kueleweka sana. Mkuu weka akiba ya maneno.
N pia mjini njaa kali mzee baba mtu akijichangnya kutaka kukulipia pango chakula matibabu n dharura zingine kwanini utajirahisishe tu. Mjini akili humu
Anasema waliachana kwa sababu X wake alitaka watoe mimba.
 
Acha pombe kijana. Hayo yote ya kuona shape km wema inawezekana ni pombe tu.
 
Kwahiyo ndugu unahisi nimepotea. Nikuulize swali: Ushawahi kupenda achana na kutamani kutokana na sifa za nje kupenda ishawahi kukutokea ?
Hicho ulichoandika sio mapenzi ya kweli, ni tamaa ndio inakusumbua.
 
Nadhani mtoa mada anahitaji kutofautisha upendo na tamaa za mwili. Hizi ni sexual excitement tu. Si dhani kama ndani ya muda mfupi namna hii unaweza ukawa umemfaham MTU vya kutosha na kuamua kufanya maamuzi makubwa namna hii. Isitoshe hawa viumbe hasa wanapohitaji kuolewa huwa wanauwezo mkubwa sana wa kuigiza (pretend). Nakushauri utumie muda zaidi kumchunguza, umfaham vizuri!
 
Gawa kadi za michango sasa kiongozi ili hili swala liwe faster
 
Week moja mmeshaanza mipango ya ndoa mkuu

Ila asante kwa kutusifia [emoji847] na wahenga walisema usitukane mamba kabla haujavuka mto ndio kilichokukuta
 
Daniel Adrian,
Wewe endelea na maisha yako na mtarajiwa wako, usikatishwe tamaa na ushauri hasi unaotolewa humu jf.

Maisha ya ndoa kitu cha kwanza unamtanguliza YESU KRISTO, pili maisha ya ndoa ni nyinyi kuwa na lugha moja na kupatana katika kila jambo . Kuaminiana na uwazi hapo mtafanikiwa sana kwenye maisha yenu.
Nikwambie jambo mkuu, ndoa ni "paradiso hakika" , mkiweza kuwa na mawasiliano mazuri na ya karibu yenye uwazi.
Kuwa na mtoto wala hakuna tatizo , wewe mpende tena toka moyoni mwako mkubali kuwa ni mwanao, haijalishi baba yake yupo hai au amefariki.
Na mtoto anapokosea wewe ongea na vizuri tu kama baba yake na kumweleza kipi kizuri na kipi kibaya muda ule ule anapokuwa amekosea , kupiga kuchapa siyo siyo dawa ya kumrekebisha mtoto.
Penda kuwa na muda mwingi na familia na siyo marafiki.
Familia ndiyo kila kitu.

Angalizo: ndoa nyingi zinaharibika mmoja wapo anapoanza kuchepuka. Ambako kuna sababishwa na kununiana, kutokuwa na mawasiliano mazuri toka asubuhi mpaka jioni, kutokuheshimiana, mazoea ndiyo hasa yanaharibu sana ndoa.
Jitahidi kumfanya mkeo mpya kila siku.
Hata kama hamjui mapenzi muwe wazi mfundishane. Msioneane aibu.
Mzee wa Msoga alisema akili za kuambiwa changanya na zako mambo yanaenda.
Mkuu ina maana hujawahi kuona au kusikia ndoa za walokole zimevunjika tena wengine ni wahubiri wakubwa tu? Ndoa ni hatua muhimu sana kwenye maisha ya mtu sio jambo la kufanya majaribio haswa kwenye scenario kama hii ambayo kuna vulnerable and innocent kid atakuwa involved kwenye complex affair , maandiko yanasema AONYWAYE MARA NYINGI NA KUSHUPAZA SHINGO. ...........
 
Habari za saa hizi Wanajamvi.

Leo kuna jambo fulani nataka kushare nanyi, jambo ambalo huenda mnalifahamu au hamlifahamu lakini kwa vyovyote najua kwa mjadala huu mtafahamu zaidi.

Tunatofautiana mitazamo. Kuna mitazamo tofauti tofauti kuelekea swala la kuoa Singo maza (naomba nitohoe najua inapaswa kuwa 'Single mother' ila sipendi kuchanganya lugha).

Kuna watu tumejizatiti hatutaoa singo maza ila hii kitu ni rahisi zaidi kuzungumza kuliko kuweka katika matendo. Kwanini ?

Mara nyingi kumpenda mtu hutokea bila hiari. Bila kuamua na kupatanisha maamuzi yako na mtazamo wako hiyo ndiyo sababu baadhi yetu tumejikuta tukienda kinyume na mitazamo yetu linapokuja swala la kuoa singo maza.

Acha nieleze jinsi nilivyozama kwa Singo Maza na kujikuta napuuza mtazamo wangu.

Mwishoni mwa mwezi wa tisa nilipewa mwaliko wa kuhudhuria sherehe za harusi fulani ya swahiba wangu sana.
Ilikuwa siku ya Jumamos usiku wa hiyo sherehe, wakati sherehe inaendelea na sisi (mimi na kampani fulani ya rafiki yetu) tumekaa kwenye meza ile kwenye meza jirani palikuwa na msichana fulani. Mweupee, mzuri kweli kweli, shape kama la Wema Sepetu. Nilipomuona nikamstua nikampa hi kisha nikakausha maana niliamini sio hadhi yangu ile . Najijua life langu 'dongotee' kula kwa kuunga unga na mishe ziende vizuri ndo nivae. Watoto wazuri kama wale wanataka matunzo.

Basi nikiwa naendelea kushusha bia, nikapaliwa. Bia ikanimwagikia kwenye shati. Shati likachafuka, miongoni mwa watu waliniona hili likitokea ni yule mrembo, rafiki zangu walipoona hili walinicheka sana ila yule mrembo (acha nimwite Asha) aliinuka alipokuwa na kunifata akanipa pole akatoa kitambaa chake akanipa nijifute. Nikakataa akanibembeleza nikaona sooo nikachukua ila sikujifutia chake niliinuka nikaenda msalani. Ila mpaka hapo akawa amenigusa kwa kiasi fulani nikaanza kumuona wife material.

Niliporudi nikamuomba namba akanipa. Niliporudi home nilimpigia simu aiseee! tulizungumza mpaka asubuhi, akanambia anaomba alale nikamuacha ila nikamuomba tukutane siku hiyo hiyo (jumapili) akasema sawa tutakutana jioni. Kweli jioni hiyo tukaweza kukutana maeneo fulani hivi ya ubungo tukaenda Bar fulani hivi. Kwanza kujiamini kuliniisha maana toto zuri vile linakubali appointment na mie tena sehemu km ile ila nikajikaza mpaka nikafanikiwa kumtongoza.

Hakukataa wala hakunambia chochote ila akasema ntakujibu siku nyingine. Nikaona 'Sawa.' mazungumzo yakaendelea ila sasa katika mazungumzo yake alikuwa mwepesi sana kusema maneno fulani yakuonesha kuwa yeye ni mtu wa dini. Lakini pia alikuwa mwenye ushauri chanya sana na kuonesha uzoefu mkubwa wa maisha jambo ambalo lilinifanya nione huyu ni 'wife material.' Istoshe hakuaguza pombe wala soda ila maji tu na akanambia atalipia yeye, nikasema mke si ndo huyu sasa.
Baada ya kama wiki moja hivi toka tuanze kuwasiliana mahusiano yakawa yameanza rasmi na kwakuwa nilishazama na KUDATA kwake sana nikaona sasa ni wasaa rasmi wa kupanga maswala ya harusi maana ni wife material haswa: hana lawama, hana mizinga, ata ukimwambia njoo saa nane usiku anaweza akaja, mshauri mzuri na mzoefu sana wa maisha istoshe ni MZURI MNO wa muonekano mpaka shape yaani kama ya wema.

Waswahili wanasema usione vyaelea vimeundwa, tukiwa katika mazungumzo akanambia kuna kitu nataka nikwambie, nikamwambia niambie, basi nilijua anaomba hela(maana hivyo ndivyo nnavowajua wanawake kwa uzoefu wangu) kumbe na tofauti kabisa na hilo. "Mimi nna mtoto," unasemaje ? niliuliza "Nna mtoto ana miaka mitatu, Nimeona bora nikwambie mapema kabla hatujaingia kwenye ndoa".

Sasa ndo tunarudi kwenye mada hii, unaweza kuwa na mtazamo fulani kuhusu wanawake wenye watoto, kwamba labda hutooa mwanamke mwenye mtoto katika maisha yako lakini mi nakwambia mwanaume mwenzangu unasema hivyo kwa sababu hujawai PENDA mwanamke mwenye mtoto.
Mimi nilikuwa na mtazamo huo huo lakini mpaka kufikia hatua hii ambayo nimependa kiasi hiki, mtazamo wangu nauona wa Kipumbavu sana, najiuliza kwanini nilikuwa naona si vizuri kuoa mwanamke mwenye mtoto ? Hapa saa hizi nawaza namna maisha yatakavyokuwa nitakapokuwa na familia yangu mpya na mtoto wa nyongeza, nna mtazamo mzuri sana kuelekea singo maza wangu na nataka nimpende mwanae kama mwanangu wa kumzaa kwa sababu sasa nimebaini nguvu ya upendo.

Kama hupendi kuoa singo maza sawa huo ni mtazamo wako, ila Mtazamo wako waweza badilika siku moja ukikutana na mwanamke utakaempenda kweli kweli kama mimi ilivonitokea kwahiyo nikushauri usiseme wala kukashifu watu waliooa masingo maza kama hujui nguvu ya upendo, huenda nawe ukajikuta katika njia hii hii.

Singo maza wote jamani nyie watu mna mbinu sana maana leo nimejikuta nakana nilichokishikilia kwa mda mrefu.

Mnisamehe wote niliowakwaza kwa kushea swala hili lililonikuta kwa kweli acha tu nikiri kuwa nimedata, na nimebadili mtazamo wangu.

Ila ushauri kwa wanaume wenzangu, usikashifu wala usiweke itikadi ya SITAOA singo maza, maana utajikuta unakana mtazamo wa kukolea kwa singo maza fulani, hii imenitokea kama mipango itakwenda vizuri basi tutaalikana kwenye harusi.

Mnisamehe kwa kuandika maneno meengi. Karibuni kwa mchango wenu.
Shauri yako. Mwanakulitaka mwanakulipata. Na utapolipata usije kulialia hapa, pambana na hali yako.
 
Back
Top Bottom