Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unakutuna na mitihani.Anaanza kuzungumza Mkamba huku akitikisa kichwa.
"Kaka huyu dada nilimkuta ana mtoto wa miaka 5. Mtoto alikuwa na afya imechoka sana. Sababu yule mama aliniambia mengi kuhusiana na baba wa mtoto. Kuwa hamjali, hakuwa akiwapenda. Mlevi na malaya. Nami nliamua kumpenda huyu dada nikamuuliza hadhani kama watarudiana na mzazi mwenzie?
Alijibu "over my dead body" basi mi nikaanza mpenda na kumhudumia mtoto.nili mtreat kama mtoto wangu na shule nikaanza mlipia ada.kakaanza kusoma. Kakawa kanakula vizuri kakapendeza.
Shida ikawa mama wa mtoto kulea hajui.mtoto anasekezwa sana ...utasikia Twalib hivi Twalib vile. Mtoto analilia chochote anataka apewe. Ukisema sina pesa mama ananuna na anaanza onesha kama vile ananyanyaswa.
Unamsikia anamwambia mtoto 'nisamehe tu mwanangu baba yako ndo angekuwa na uchungu nawe...tuombe tu Mungu" anajikunyata. Yaani hapo naonekana simpendi na simjali mtoto. Ila anakula,anavaa,anaenda shule,ana baiskel nmemnunulia na toys kibao tu. Akikosa kitu kimoja tu hayo mengine yanasahaulika.
Baadaye mama akaanza nikisema sina pesa aliyotaka ananiambia. Jumamosi asubuhi ngoja nikaonane na baba Twalib anipatie pesa flani ili usipate mzigo kumlea huyu mtoto. Mara nyingi namwambia kwa nini usivumilie siku mbili tatu ntakupa.
Basi hapo anasema haya. Anachangamka. Baadaye ikawa ndo mchezo. Nikamruhusu nenda. Akaenda akarudi saa 10 mchana.nikamuuliza ulikuwa wapi muda wote huo toka saa 3 na ulisema unaenda chukua tu pesa.
Anajibu... "Yaani utaenda tu kuchukua pesa na kuondoka?kwani pale bank? Lazima mkae muongee kidogo na kumpa feedback ya mwanaye" akawa anajifanya kama amechoka sana ili niwe na wivu au niumie roho. Usiku tumelala nikamgusa tu wakati nageuka. Akaniambia "sweet leo niache tu nimechoka na safari ya huko nlikoenda" nikamwambia tu "usijali nlikuwa nageuka tu" sikutiana naye tena.
Mara ya pili, mara ya tatu aliomba nimpatie tsh 350,000 ya sherehe ya birthday.nikamwambia nitampa tsh 150,000 tu. Akaniambia. "Sasa 150,000 nayo kweli ni pesa?hivi angekuwa mwanao kabisa ungemfanyia hivi?unamtesa huyu mtoto unadhani hivi atakupenda kweli?" Alinikwaza sana.
Nikamwambia "mimi natimiza tu wajibu wangu kwa mtoto.suala la kunipenda au kutonipenda namwachia yeye"
Akawa ana dial number akaanza kuongea na kutoka nje. Baadaye anarudi ananiambia "baba yake kaniambia weekend atakuwepo niende nikachukue pesa" nikamwambia sawa.
Ijumaa nikamwambia mpeleke na mtoto angalau amsalimie baba yake. Akasema " sawa tena itakuwa vizuri aanze fahamiana naye vizuri zaidi"
Akaondoka. Nikachukua nguo zake na za mtoto wake. Nikakusanya kila kitu chake. Na baiskeli pia. Nikafunga nikaweka kwa jirani. Maana tupo kwenye apartments. Nikawaambia mama T atakuja vichukua vitu akirudi.
Nikafunga milango yote. Pale ni kwangu alikuja alinikuta.yeye alikuja na nguo zake tu na za mtoto. Jumapili saa tano ananipigia simu kuwa funguo zi wapi. Nlimuuliza funguo za wapi? Akajibu za home. Nlimwambia pale ni nyumbani kwangu. Yeye akakae na baba twalib.na vitu vyake vipo kwa akina benny.
Amelia sana. Akiomba nimsamehe arudi kwangu. Nami nimemwambia akaishi na huyo baba twalib. Huyu dada alitaka kama kuni control yaani kwa kujua nina wivu basi akaona autumie huo wivu kuniumiza kuwa anaenda kuonana na mzazi mwenzie ili nimpe anachotaka asiende.
Sasa nimemruhusu akakae naye kabisa. Hataki anataka kurudi kwangu. Nami nimeondoka pale home nipo kikazi Arusha. Week mbili ntakuwa huku. Kuna jirani mwingine yeye mtu mzima nimemwambia pale home kama mtu atafungua mlango kwa kuvunja au namna nyingine yoyote anijulishe nipige simu polisi.na kamwambia mkewe hivyo hivyo.
Nadhani singlemother wengi huwa hawaolewi na waliowapa mimba sababu hawana akili. Wana matatizo. Huyu dada mrembo lakini kichwani ni bure kabisa. Halafu anataka aniendeshe. Kwa sasa mtu akitaka nisimsumbue kimapenzi aseme yeye ni singlemother."
Hili ni swali la msingi sana. Sana.Kuna single mother mmoja ananipenda sana, nadhani ananilia timing nimuoe.
Kanuni ni ileile, yaani umzalie mtu bado akuache mimi ndio nikuoe?
Mume mwema kutoka kwa Mungu!!!Habari za Jumapili wakuu! Hongereni kwa Ibada kwa wale mlioenda ibadani[emoji112][emoji112]
Lengo la mada hii, ni kukushauri na kukutia Moyo wewe Single mother uliejikatia tamaa. Mimi ni miongoni mwa single mother. Nilipata ujauzito nikiwa Form 4 nina miaka 17 tu! Nililelewa katika Familia ya kilokole na hata haya mambo ya kujiingiza kwenye Mahusiano ya kimapenzi sikuyataka kabisa but makundi& mzazi ndo vilisababisha hivi (nikipata muda nitaleta mada kuhusu hiki)
Baada ya Kujigundua ni mjamzito niliomba Rehema sana nikatubu Kwa Mungu ninakaendelea na masomo. Namshukuru Mungu mimba haikuonekana hadi Siku najifungua zilibaki siku 3 nianze Necta. Nakumbuka nilijifungua Ijumaa then j3 nikaingia Chumba Cha mtihani nikafanya paper nikatoka na 4 mbaya but Cheti nilipata.
Baada ya Hapo nilinuniwa na Mzee karibu Mwaka,nikaishi Maisha ya tabu sana Kiasi kwamba nilitamani kunywa Sumu nife ila nikawaza, kwani mm ndo nimekuwa wa Kwanza? Nikaamua kutokujichukia na kutokulia tena Nikaamua kuanza kufanya biashara na nikawa najiamini sana kama hakijatokea chochote, then Mzee akashauriwa akanipeleka Chuo but ile Caring haikuwepo!
Namshukuru Mungu nilifanikiwa kumaliza, nikatafuta Kazi na nikaamua kujisimamia mwenyewe,nikajithamini na Nikapata Kibali sanaa!
NINACHOTAKA NIKWAMBIE NI HIKI:- Wewe bado ni wa thamani hata kama una mtoto! Usijirahisirahisishe kwa Wanaume,eti Kisa ulishazaa!! Uthamani wako uko palepale
[emoji2771]Usikate tamaa kwa Maneno yao au Kejeli zao,Focus kuitengeneza ile future uliyoipoteza hapo Awali.
[emoji2771]Mrudie Mungu na uweke tumaini Kwake kikamilifu. Nina Uhakika atakupa Nafasi tena kama hautakuwa na Mchanganyo!! Kuwa na Msimamo Mungu atakupatia wa kwako!
Mwisho, achana na Uzinzi! Subiri Mume mwema Kutoka kwa Mungu (but kama utakuwa serious na Mungu)
Wanaliwa wote wawili na mwanaume mmoja.!!Kuzaa mapema kuna faida kubwa sana huko mbeleni, kama utajipanga vizuri; ukiwa na miaka 36, mtoto anakuwa 18, unakuwa sawa na mtu na dada yake.
Ogopa maradhi; usiogope mimba.