Hali ya migawanyiko na uhasama wa kisiasa miongoni mwa viongozi wapya waandamizi ndani ya Chadema bado inaendelea kushamiri, kiasi kwamba wimbi la kutokuaminia limeongezeka mara dufu baada ya uchaguzi pengine kuliko hata kabla ya uchaguzi wao wa ndani uliomalizika January 2025 katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam.
Hali hiyo isiyo na afya kwa ustawi wa kidemokrasi ndani ya chadema, ina ashiria uwezekano na uelekeo wa kuumizana na pengine kupotezana kabisa hasa kuelekea kwenye hatua za uteuzi wa mgombea urais, madiwani na wabunge kupitia chama hicho.
Tayari kuna hujuma za makusudi kabisa dhidi ya malengo na agenda za uongozi mpya zimeripotiwa na katibu mkuu wa chadema hivi karibuni.
Kwa hali hii tutegemee kuona watu wakipotezana ndani ya chadema wao kwa wao?
Na je,
kiunzi cha uteuzi watakivuka salama au kitazidisha mpasuko na uhasama zaid wa ndani ya chama hicho cha upinzani?π
Mungu Ibariki Tanzania.