Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo ziko kwenye magazeti mawili, Gazeti la Nipashe la kila Jumapili na gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, pia kuna kipindi cha TV cha KMT, kila Jumapili saa 3:00 usiku na marudio Jumatano saa 9:30 alasiri on Channel Ten, nikiangazia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi makubwa kwa taifa.


Jana niliangalia tukio la uapisho wa wateule wapya, Ikulu Dar es Salaam, kwanza nilifarijika sana kuona miongoni mwa waalikwa wa tukio lile, ni Mzee wa Ngomeni, Musa Richard Mwasha kwa jina maarufu la Kuhani Musa, nimefarijika kwasababu mwaliko huu wa Kuhani Musa ni kuonyesha kuwa Kuhani Musa anatambulika na serikali. Huko nyuma niliwahi kushauri Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Pili nimefarijika sana kumuona Rais Samia akitoa sababu za kumteua kila aliyemteua na kumpa majukumu kwa uwazi kabisa. Katika uteuzi niliwahi kuandika Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Enzi za Kikwete, Tanzania tulisaini ule mkakati wa Open Government Partnership, OGP, na kuwa nchi ya pili barani Afrika kusaini baada ya Africa Kusini. Mpango huo uliokuwa unasisitiza ushirikishwa wa umma kwa ukweli na uwazi, truth and transparency, katika kila kitu serikali inachokifanya.

JPM alipoingia, aliufuta mpango mkakati huo, na Tanzania, ikajitoa, hata Bunge live likafutwa, mikutano ya vyama vya siasa ikapigwa marufuku na hata mikutano ya ndani kuzuiwa.

Rais Samia alipoingia, na falsafa yake ya 4R, akafanya mabadiliko mengi makubwa ikiwemo kufungulia mikutano ya siasa.

Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT, Rais wa JMT anaweza kushauriwa na wasaidizi wake, lakini kwenye kufikia maamuzi, rais anafikia uamuzi yeye kama yeye, na halazimiki kufuata ushauri wa yeyote, na hawajibiki kutoa sababu yoyote ya maamuzi yake kwa yeyote.

Powers za rais kuteua na kutengua ni discretional powers, kwa rais kuteua, kutengua au kutumbua at her pleasure bila kutaa sababu yoyote kwa yeyote, na teuzi hizi hazihojiwi na mamlaka yoyote.

Hivyo kitendo cha Rais Samia kuwa open and transparent kwa kueleza sababu za kumtea fulani mahala fulani na kumpa majukumu kwa uwazi, hii ni hisani kubwa na nzuri kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Anachokifanya rais Samia kuwa muwazi, open and transparent sababu za kuwateua wateule wake, ni hisani tuu, tena hata uapisho live mubashara kisha kutolewa hotuba, kumeanza na JPM, zamani hatukuwahi kuwa na hotuba kwenye uapisho, ni kuapa tuu and that was it.

Kitu kizuri zaidi, sio tuu Rais Samia anakuambia kwanini amekuteua, bali anaelekeza uende ukafanye nini!. Mfano RC Makonda amepewa special task Arusha, jiji la kitalii, hivyo anapaswa kwenye kukuza Utalii, ila pia kuna maelekezo mengine ya kuyashughulikia na kuwashughulikia ikiwemo issues za wale machalii wa RChuga na 'cha Arusha'.

Yule RC wa Mara ambaye ni mjeshi, kaelekezwa kwenda kushughulikia kijeshi jeshi kile kilimo cha lile zao, (hakulitaja) ambalo Mara ni maarufu na kulivusha mpakani na nchi jirani.

Hiki anachofanya Ras Samia ni sawa na ile Open Government Initiative, kwa mteuliwa kupewa changamoto openly and transparently, akishindwa ku deliver
The public yote itajua hivyo hiki ni kitu kizuri kwa uwajibikaji.

Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, au kupata taarifa, the right to information act, hivyo wananchi kuelezwa kila kinachowahusu ni haki yao na sio hisani.

Kwa vile Rais Samia ameisha onyesha njia kwa kutuhisania, tuwe watu wa shukrani kwanza kwa kumshukuru kwa hiyo hisani tuu kwanza, kisa sasa tumuombe atupe na haki ya kupata taarifa, asiishie kwenye kutupatia taarifa za uteuzi tuu, tupatiwe na taarifa za sababu za utenguzi kwasababu maofisa hao ni watumishi wa umma, wanaolipwa na fedha za umma, hivyo umma una haki zote za kujua kuhusu utendaji wa wateule hao, na sababu za kutenguliwa kwao na kutumbuliwa.

Mfano Paul Makonda, baada ya kuteuliwa Mwenezi wa CCM, amefanya wonders katika kipindi kifupi na kurejesha imani ya wananchi kwa CCM, kwa kuwakimbiza viongozi mchaka mchaka, wengi wakitaraji mchaka mchaka huo ungeendelea hadi 2025, katika uchaguzi ujao Makonda aingie Bungeni, na kupewa Wizara nyeti, lakini mara ghafla Makonda kama Mwenezi, akatumbuliwa!.

Mtu yoyote mwenye cheo kikubwa, akaondolewa na kuteuliwa cheo kidogo ni kutumbuliwa tuu!, hivyo Makonda ametumbuliwa uenezi na kupoozwa na u RC, Dr. Bashiru Ali Kakurwa alitumbuliwa uenezi na kupoozwa na ubunge wa kuteuliwa. DGIS wametumbuliwa mara kadhaa na kupoozwa na ubalozi, wengine wakitumbuliwa wanasugua bench, kama Balozi Liberata Mulamula, Prof. Kabudi, William Lukuvi na wengine wengi, the public has the right to know sababu, na sio kusubiria kuhisaniwa.

Kama ilivyo sifa njema kuteuliwa, mtumishi wa umma akiboronga, the public ielezwe kama nilivyo shauri hapa - Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Tena kwa maoni yangu, nafasi za juu zote wakiwemo wakuu wa mihimili, Jaji Mkuu, Spika na wakuu wa zile independent organs zote, nafasi zinapokuwa wazi, zitangazwe, Watanzania wenye sifa waombe, washindanishwe kwa uwazi, tupate the best ndipo rais apelekewe kuteua, na sio huu utaratibu wa sasa wa watu kuokotana, kuteuana na baada ya siku mbili kutenguliwa, haileti picha nzuri sana kwa awamu hii ya Rais Samia.

Nchi nyingi wakiwemo jirani zetu Kenya, Jaji Mkuu, anaomba kazi, wanashindanishwa, wanasailiwa, the best anachaguliwa, ndipo rais anapelekewa kuteua.

Nimalizie kwa kumpongeza tena Rais Samia kwa kutuhisania openness and transparency kwenye teuzi zake, openness hii na transparency hii tuifanye ni haki na sio hisani.

Wasalaam

Paskali
 
Sawa ngosha Pascal Mayalla . Tatizo CCM hawaaminiki
 
Hapo kwenye kutengua na kutoa sababu na kutoa maelekezo ya nini akafanye mteule mpya alianzisha Magufuli huo mtindo na si Samia!
DAS wa Kisarawe Bwana Mwampamba alionja joto la Jiwe na wengine wengi tu wakati wa Magufuli!
 
Nimesoma kichwa cha habari na kujibu.

Wakili huna "Connection" na wakubwa wa CCM ni nini??

Maana Kila mkeka ukitoka HAUMO!!
Mkuu, kaka Pascal Mayalla labda anaponzwa na ukomavu wake (umri na uelewa mpana ukiwemo). Nakumbuka miaka ya 1998-2000 alikuwa akija kutupa Semina ya Maaadili na Malezi Mema pale Don Bosco Upanga viongozi wa TYCS Sekondarini (Jumuiya ya Wanafunzi Wakatoliki). Hakika, kumteua ni kuruhusu critical mind ifanye kazi...na inaweza kuvuka mipaka.
 
Paskal makonda hakuna wonders aliyoifanya wkt akiwa mwenezi ndio mana Ali alihudumu kwa muda mfupi alichofanya ni kuleta taharuki tu.

Kama mama kampa kazi ya kwenda kukuza utalii basi kapewa nafasi ya kubadilika katika aina yake ya uongozi na kumtaka kuwa kind kuliko kuwa aggressive kwenye aina yake ya uongozi

Wote tunajua kazi ya kuvutia watalii ni lazima owe royal na u bow kwa wageni jambo ambalo kama ataliweza basi litambadilisha na kuwa kind kitu ambacho naona kitampa sn shida.

Pia apunguze kujinasibisha kama mpenda sera za jiwe hiyo nayo kwa kiasi fulani chief hangaya haipendi japo hawezi kisema hadharani ajikite zaidi kuwa chawa wa mama kuliko kujifanya mmagufulisi itamcost his career.
 
Naunga mkono hoja,Nami naongezea mawazo yangu hapo nikianzia na umuhimu wa kupata katiba mpya,katiba hii itatoa ukomo wa nini our no 1 anaweza kuwa na mamlaka ya kuwateua na kuwatengua,Rais awajibike kwa cabinet yake tu ,CEOs wengine wote Bunge lihusishwe kwenye uteuzi na utenguzi,IGP,CDF,mkuu wa tiss etc etc hawa uteuzi wao upitie Bunge na Rais apelekewe majina yaliyopitishwa na Bunge ili ateue,Rais hatakua na uwezo wa kuwafuta kazi bila ya 2/3 ya wabunge kuunga mkono,na sikujua nchi hii ina vyeo vingi mno vya ajabu!JUDICIARY wawe huru wa kujiteua na impeachment Bunge lihusishwe
 
Dkt.Bashiru Ali alitokea kwenye ukatibu mkuu kiongozi kabla ya kuteuliwa ubunge na sio uenezi.

Lukuvi aliteuliwa kuwa mshauri wa Rais siasa ,hasugui benchi.

Ni hayo ndio ya kuangaliwa kaka Mayalla.

Je, ni kiwango gani Cha elimu mtu kuteuliwa kuwa mtendaji mkuu wa taasisi za Serikali au na vigezo vingine ni vipi?
 
Point of correction mkuu Paskali Mayalla, Bashiru alikuwa Chief Secretary (KMK) na akaondolewa kwenda bungeni na sio katibu wa itikadi na uenezi.
Mwenezi wa kwanza aliondolewa na SSH baada ya kuwa mkiti ni Polepole baada ya nafasi ya kujazwa na Shaka na kuachiwa ubunge ambao alikuwa nao toka enzi za "Mwamba"

Asante.
 
Dkt.Bashiru Ali alitokea kwenye ukatibu mkuu kiongozi kabla ya kuteuliwa ubunge na sio uenezi.
Kweli hapa Paskali kakosea ingawa pia Bashiru alitokea kwenye Ukatibu Mkuu Kiongozi na kuteuliwa kuwa Mbunge.
Lukuvi aliteuliwa kuwa mshauri wa Rais siasa ,hasugui benchi.
Lukuvi yupo benchi. Ushauri Kwa Rais siyo kazi ya Kila siku!
 
Mama akukumbuke.
 
Wacha nichangie kwanza kwenye hii paragraph
Kwa maoni yangu naona mfumo tulionao Sasa ni outdated kwani ni Rais ndo anachagua nani awe wapi na nani wapi Sasa obvious atachagua watu ambao anawajua tu Sasa mkuu wa nchi anafahamiana na watu wangapi Kwenye li nchi lenye watu zaidi ya 60million ?

Kiukweli anawajua watu wachache sana na ndio maana tunaona Kila siku majina ni yale yale tu mtu anaboronga huku anawekwa bench after sometimes Rais anahitaji kuteua watu wengine Sasa anawatoa wapi ? na kichwani mwake ana cycle ile ile ya watu wale wale walio haribu sehemu nyingine

Tunaishia kuona watu wakibadirishwa nafasi hata kama uwezo mdogo mfano ni hizi tengua teua za Kila mara na watu wanao tenguliwa na kutuliwa ni wale wale walioshindwa sehemu zingine

Ndo anao wajua Sasa afanye nini ?


Kiukweli katika mifumo ya kitaifa Bado tuna shida kubwa sana maana nashindwa kuelewa kwamba kwenye hili linchi eti wenye uwezo ni Hawa kinamakonda, kina happy na wengine wa aina hiyo


Tunapaswa kuweka mfumo watu waombe kazi watakua wengi watachujwa tuanakua na chance ya kupata watu best wacha Sasa tunapata watu wenye uwezo mdogo kwenye nafasi kubwa ndo maana Kila siku teua tengua

Mambo yanaenda hovyo hovyo tu karibu Kila idara, Kila sehemu, Kila ofisi mambo ni hovyo tu kumejaa upendeleo, rushwa na mambo mengi mabaya



Kwa Sasa niishie hapa nitarudi ikibidi
 
Makonda ni muhalifu TU anayetakiwa kuwa Gerezani. Ndio mahali pake.
 
Hapo kwenye kutengua na kutoa sababu na kutoa maelekezo ya nini akafanye mteule mpya alianzisha Magufuli huo mtindo na si Samia!
DAS wa Kisarawe Bwana Mwampamba alionja joto la Jiwe na wengine wengi tu wakati wa Magufuli!
Bila kumsahau kangi lugola. Magufuli kila aliyemteua alisema kilichofanya ateuliwe na alipotengua alitoa sababu za utenguzi. Uchawa ukaanza rasmi.
 
 
Mikutano ya ndani kuzuiwa? Kwamba enzi za JPM kulikuwa na mgao wa umeme?
Kama teuzi zinatafutwa kwa uchawa namna hii basi mzee Mayala unazeeka vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…