Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Pongezi Rais Samia kwa Kutuhisania Openness and Transparency Kwenye Uteuzi, Mnaonaje Ifanyike Kwenye Utenguzi na UtumbuzI Iwe ni Haki na Sio Hisani?

Nikisema wenye dhamana waliotokana na utaratibu ulikubaliwa na jamii unaona kama kweli ulikuwepo wakati wa utumwa?
Unadhani kipindi ambacho kiliona kwamba matabaka ni sawa na wengine wanazaliwa kuwatumikia wengine au wengine wana damu ya uongozi katika jamii husika utumwa haukuwa ndio utaratibu ?

Kwamba wewe babu yako kama alikuwa ana madeni au mfalme kaamua kumlaani kwamba vizazi na vizazi vyake vitakuwa watumwa haukuwa utaratibu ?

Au unadhani all Laws are Just ?!! Au unadhani Majority are Always Right -Argumentum ad populum
 
Wanabodi,.

Kwa vile Rais Samia ameisha onyesha njia kwa kutuhisania, tuwe watu wa shukrani kwanza kwa kumshukuru kwa hiyo hisani tuu kwanza, kisa sasa tumuombe atupe na haki ya kupata taarifa, asiishie kwenye kutupatia taarifa za uteuzi tuu, tupatiwe na taarifa za sababu za utenguzi kwasababu maofisa hao ni watumishi wa umma, wanaolipwa na fedha za umma, hivyo umma una haki zote za kujua kuhusu utendaji wa wateule hao, na sababu za kutenguliwa kwao na kutumbuliwa.

Kama ilivyo sifa njema kuteuliwa, mtumishi wa umma akiboronga, the public ielezwe kama nilivyo shauri hapa - Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Nimalizie kwa kumpongeza tena Rais Samia kwa kutuhisania openness and transparency kwenye teuzi zake, openness hii na transparency hii tuifanye na haki na sio hisani.

Wasalaam
Paskali
Watanzania tufike mahali tu demand the right to information wakati wa utumbuzi, mfano mpaka leo, sijawahigi kujua, kwanini Balozi Liberata Mulamula alitumbuliwa, sasa January Makamba nae ametumbuliwa, natamani kujua sababu. Sihitaji kujua sababu ya Nape kutumbuliwa itakuwa ni mdomo umemponza kwa ile kauli ya Waswahili ya "mzaha mzaha, hutumbua usaha", lakini kwa Byabato ana kosa gani?.

Nashauri tumsaidie Rais Samia, asifanye kitu kinachoitwa " bad karma accumulation" bila kujijua, japo uteuzi na utenguzi is at the pleasure of the appointing authority, ukimtumbua mtu bila haki, kwa namna inayomdhalilisha, huyo mtumbuliwa akiumia, ana develop bad karma ya maumivu yake, hiyo bad karma inahifadhiwa katika akiba ya karma accumulation ya aliyesababisha maumivu hayo!, hivyo hii accumulation ina pile up, ikifikia kuwa the pile is big enough hadi furushi hilo la karma likawa halibebeki, then hilo zigo la karma, litamuelemea mbebaji sometimes linaweza kumponza na ... ndio maana nimewashauri viongozi wetu wateuliwa Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
P
 
Wanabodi,

Hivyo kitendo cha Rais Samia kuwa open and transparent kwa uwazi, hii ni hisani kubwa na nzuri kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Tanzania tuna sheria ya haki ya kupata habari, au kupata taarifa, the right to information act, hivyo wananchi kuelezwa kila kinachowahusu ni haki yao na sio hisani.

Kwa vile Rais Samia ameisha onyesha njia kwa kutuhisania, tuwe watu wa shukrani kwanza kwa kumshukuru kwa hiyo hisani tuu kwanza, kisa sasa tumuombe atupe na haki ya kupata taarifa, asiishie kwenye kutupatia taarifa za uteuzi tuu, tupatiwe na taarifa za sababu za utenguzi kwasababu maofisa hao ni watumishi wa umma, wanaolipwa na fedha za umma, hivyo umma una haki zote za kujua kuhusu utendaji wa wateule hao, na sababu za kutenguliwa kwao na kutumbuliwa.

Nimalizie kwa kumpongeza tena Rais Samia kwa kutuhisania openness and transparency

Wasalaam

Paskali
habari.
Naomba mwenye kujua jina na hata picha ya mume wa rais samia anisaidie tafadhali
Kuulizia jina la mke wa mtu au mume wa mtu ni kuingilia the right to privacy ya mtu, ila kwa upande wa Rais wa JMT, mke wake au mume wake, yaani first lady na 1st gentleman nao pia ni paid by taxpayers money, hivyo the taxpayers have the right to public and private info za rais wao, hivyo nitakupatia info zote,kuanzia majina yake matatu, majina ya wenzi wao na majina ya watoto wao wote。 nisubirie nikutafutie。

Sawa
 
Wanabodi,

Zawadi yangu kwa Birthday ya Mama nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
HBD Rais Samia!.
P
 
Back
Top Bottom