Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.

Pascal Mayala wewe ni miongoni mwa Watanzania wachache sana wenye akili lkn,kwa bahati mbaya sana umekuwa ukitumia akili yako vibaya sana kuitetea na kuilinda ccm mitandaoni kwa kuandika upuuzi uliopitiliza.

Suala la Katiba likipelekwa Bungeni wabunge wetu ni watu wenye njaa,ujinga,ushamba na upumbavu kwa 100% maamuzi yao yatatazama usalama wa nafasi zao za ubunge kwa uchaguzi ujao.Kuna kipindi the late Babylon from Chattle alipeleka mswaada wake Bungeni na akawaambia Wabunge "msipoupitisha nalivunja Bunge"

So,hayo yote ni sehemu ya sarakasi za kijinga za ccm!
 
HAKI haiombwi!

Tume huru ya Uchaguzi ni Hadi vifungu muhimu vya Katiba vibadilishwe.

Matokeo ya Urais yahojiwe mahakamani.

Na Rais aondolewe Kinga ya kutoshtakiwa, wote tuwe sawa mbele ya SHERIA.
 
Hata mimi bado sitaki kuamini
 
Mkuu Tlaatlaah , it's normal, mtu huwezi kuwa na maoni kuhusu kila kitu, sometimes kuna vitu vingine ni unajisomea tuu na huna maoni, ila mimi ninapokuwa sina maoni, I usually save time hata ya kuandika "sina maoni"!.
P
Pamoja sana ndugu yangu Pascal Mayalla, maoni yangu yanatekelezwa hivi sasa.
sinaga shaka na makala zako ambazo huwa zinastaili ya zile nyaraka katoliki..

unanisakazia niseme jambo ila itoshe tu kusema sina maoni
 
Mkuu NAMBA MOJA AJAYE NCHINI , nakuomba utukumbushe haya maelekezo alipewa na nani?, maana kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hawezi kupewa maelekezo na yeyote!, ila serikali yake inaweza kupewa maelekezo na ilani ya uchaguzi ya chama chake au Azimio la Bunge!.
SASA HAYO Ndio MAELEKEZO anatimiza au anajizima Data!!?
Naomba hiyo Reference ya maelekezo.
Hivi kwanini wanaccm wenzangu hawapendi kufuata maelekezo zaidi ya matakwa yao!!?
Maelekezo ya nani?.
"Kama mhusika hatofuata maelekezo kuhusu katiba itakua too late kwake beyond mwakani"!!yaani huo mwaka 2022!
Ni maelekezo yapi haya?.
Juzi wakaja tena eti"original plan is on,yaani ile plan yao ya FDR!
Msaada please, FDR no nini?.
"Brain Respiratory system shut down" huyu ni de 'levis na ujasusi wake mweusi!!!
Hapa umeniacha gizani!.
Mimi mlipakodi niliepo huku interior na nina hold kadi ya chama tawala nasisitiza hivi kwanini tusifuate maelekezo ya wenye nchi!?
Maelekezo yepi ya wenyenchi wepi?.
kwanini matamanio yetu!!?hivi mnajua upinzani una hongwa hata Mbowe waweza mhonga
Kumbe!
lakini dola haihongwi!!!

Ngoja nisubiri safari hii itakuaje tena coz nasikia JAL 1 is done 2 and 3 are next!

Haya SASA!!
Naomba ufafanuzi wa JAL?.
P
 
Sitokupa ushirikiano kwenye hilo mkuu!najua unajua!!

TEC kupitia kanisa wameshaanza maandamano yao kolabo KWA mdude nyagali baada ya waraka kusomwa KWA siku 30!!?

Msalimie Dr.Mpango !!
 
Kiukweli hakuna logic ya kufanya chaguzi mbili za nchi nzima in a span of a year.

Sema CCM huwa wanapenda sana kutengeneza magap ya kutumia pesa za umma hovyohovyo.

Kubadilisha sheria za uchaguzi pekee haitatosha kama hatuna adabu ya kufuata hata hizi mbovu zilizopo.

Uvunjifu wa sheria hufanywa na watu wenye naksi ya utu na ukosefu wa maadili.

Je wasimamizi wa sheria hawa wasio na utu na maadili na wenyewe tutawatia utu na maadili ?
 
Nimeacha kusoma bandiko lako baada ya kuona eti Samia karuhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Mkuu Rufiji dam , kuna popote kwenye bandiko hili nimezungumzia mikutano ya vyama vya siasa!.
Samia ni nani juu ya katiba na sheria.
Kumbe wewe hujui kuwa rais wa JMT ndiye katiba, ndiye sheria!, Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
Usiandike kitu huku unawaza uteuzi.
Duh...!, yamekuwa haya!. Mtu niko almost 60!, niwaze teuzi for what?. Unanijua vizuri mimi and what I do?. Hiki ninachofanya compared na ningeteuliwa popote, what is more beneficial kwa nchi yangu?.
P
 
Sitokupa ushirikiano kwenye hilo mkuu!najua unajua!!
Amini usiamini sijui!
TEC kupitia kanisa wameshaanza maandamano yao kolabo KWA mdude nyagali baada ya waraka kusomwa KWA siku 30!!?
Mimi pia Mkatoliki mwenzako ila ni Mtanzania zaidi kuliko Ukatoliki wangu ndio maana tumeliomba kanisa Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? na kuwafungua macho Wakatoliki kuwa Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?
Msalimie Dr.Mpango !!
Salaam zangu za kupindua meza zitamfikia ili baada ya Samia ni zamu ya Mkristo ila this time sio lazima awe Mkatoliki!,ili kuifuta ile kanuni ya siri kuwa akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!.
P
 
"Sio lazima awe mkatoliki" nadhani operation thunderstorms atatufaa a.k.a mkono wa baunsa au sio!!?
 
Hapa ni sawa na kujenga matumaini kwa shetani kwamba atatengeneza mazingira mazuri kwa watakatifu kwenda peponi. Kamwe haitatokea!

Rais Samia anatumia ujanj wa danganya toto unaotumiwa na mama asiyekuwa na chakula cha kuwalisha watoto wake. Anaweka jungu lililojaa mawe jikoni na kuanza kulichochea kuwaaminisha watoto kuwa chakula kipo na kitaliwa kitakapoiva.
 
Kama ulitaka kikubwa, ukapewa kidogo, shukuru kwanza kwa hicho kidogo ulichopewa kisha endelea kuomba kile kikubwa!.
This is rubbish! This is the only language fit for such a statement!. Haramia, jizi, fisadi kapora nguo zako. Anaanza kukupa vest, then unasema kuwa nimepata kidogo nashukuru kwanza angalau kwa vest, suruali na shati vitakuja baadaye1 Una akili kweli?
 
Kazi kweli kweli
I have no comment !
 
Kuna baadhi ya mambo Hua anayashughulikia vizuri mfano hili ila mengine anakwama sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…