Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.

Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.

Mkuu Kb Ulayaulaya , it's true watu waliowengi humu hawanielewi!. Mimi ni mtu wa kuridhika na madogo tuu, hivyo ninaridhika sana na hao wachache wanaonielewa ndio maana naendelea kuwaandikia.

Japo ni Mwenyekiti wa chama changu, pia ni rais wa nchi, Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, bandiko hili ni kumhusu mkuu wa serikali na sio Mwenyekiti wa chama!.

Sio kila anayepongeza ni chawa!. Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
P
Pascal Mayala wewe ni miongoni mwa Watanzania wachache sana wenye akili lkn,kwa bahati mbaya sana umekuwa ukitumia akili yako vibaya sana kuitetea na kuilinda ccm mitandaoni kwa kuandika upuuzi uliopitiliza.

Suala la Katiba likipelekwa Bungeni wabunge wetu ni watu wenye njaa,ujinga,ushamba na upumbavu kwa 100% maamuzi yao yatatazama usalama wa nafasi zao za ubunge kwa uchaguzi ujao.Kuna kipindi the late Babylon from Chattle alipeleka mswaada wake Bungeni na akawaambia Wabunge "msipoupitisha nalivunja Bunge"

So,hayo yote ni sehemu ya sarakasi za kijinga za ccm!
 
HAKI haiombwi!

Tume huru ya Uchaguzi ni Hadi vifungu muhimu vya Katiba vibadilishwe.

Matokeo ya Urais yahojiwe mahakamani.

Na Rais aondolewe Kinga ya kutoshtakiwa, wote tuwe sawa mbele ya SHERIA.
 
Serikali hii hii ya ccm iruhusu uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi! Yaani Tume ambayo viongozi wake watathibitishwa na Bunge badala ya kuteuliwa na Rais, Wafanyakazi wa hiyo Tume hawatakuwa makada wa chama cha siasa kama ilivyo sasa, Wakurugenzi wa Halmashauri hawatakuwa wasimamizi wa uchaguzi, nk!!

Naomba tu niwe Mtanzania wa mwisho kuamini jambo hilo kutokea.
Hata mimi bado sitaki kuamini
 
Mkuu Tlaatlaah , it's normal, mtu huwezi kuwa na maoni kuhusu kila kitu, sometimes kuna vitu vingine ni unajisomea tuu na huna maoni, ila mimi ninapokuwa sina maoni, I usually save time hata ya kuandika "sina maoni"!.
P
Pamoja sana ndugu yangu Pascal Mayalla, maoni yangu yanatekelezwa hivi sasa.
sinaga shaka na makala zako ambazo huwa zinastaili ya zile nyaraka katoliki..

unanisakazia niseme jambo ila itoshe tu kusema sina maoni
 
AACHE kupapasa MAELEKEZO aliyopewa aliambiwa hivi;-

"Mwakani kuwe na muendelezo wa kuandika katiba mpya,teua Bunge sio lazima wawepo wabunge wote bali wale wenye uwezo, uchaguzi wa serikali za mitaa usubiri hadi katiba mpya ipatikane"

Huo ni mwaka 2021 tarehe 28 MWEZI wa TATU!!
Mkuu NAMBA MOJA AJAYE NCHINI , nakuomba utukumbushe haya maelekezo alipewa na nani?, maana kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hawezi kupewa maelekezo na yeyote!, ila serikali yake inaweza kupewa maelekezo na ilani ya uchaguzi ya chama chake au Azimio la Bunge!.
SASA HAYO Ndio MAELEKEZO anatimiza au anajizima Data!!?
Naomba hiyo Reference ya maelekezo.
Hivi kwanini wanaccm wenzangu hawapendi kufuata maelekezo zaidi ya matakwa yao!!?
Maelekezo ya nani?.
"Kama mhusika hatofuata maelekezo kuhusu katiba itakua too late kwake beyond mwakani"!!yaani huo mwaka 2022!
Ni maelekezo yapi haya?.
Juzi wakaja tena eti"original plan is on,yaani ile plan yao ya FDR!
Msaada please, FDR no nini?.
"Brain Respiratory system shut down" huyu ni de 'levis na ujasusi wake mweusi!!!
Hapa umeniacha gizani!.
Mimi mlipakodi niliepo huku interior na nina hold kadi ya chama tawala nasisitiza hivi kwanini tusifuate maelekezo ya wenye nchi!?
Maelekezo yepi ya wenyenchi wepi?.
kwanini matamanio yetu!!?hivi mnajua upinzani una hongwa hata Mbowe waweza mhonga
Kumbe!
lakini dola haihongwi!!!

Ngoja nisubiri safari hii itakuaje tena coz nasikia JAL 1 is done 2 and 3 are next!

Haya SASA!!
Naomba ufafanuzi wa JAL?.
P
 
Mkuu NAMBA MOJA AJAYE NCHINI , nakuomba utukumbushe haya maelekezo alipewa na nani?, maana kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hawezi kupewa maelekezo na yeyote!, ila serikali yake inaweza kupewa maelekezo na ilani ya uchaguzi ya chama chake au Azimio la Bunge!.

Naomba hiyo Reference ya maelekezo.

Maelekezo ya nani?.

Ni maelekezo yapi haya?.

Msaada please, FDR no nini?.

Hapa umeniacha gizani!.

Maelekezo yepi ya wenyenchi wepi?.

Kumbe!

Naomba ufafanuzi wa JAL?.
P
Sitokupa ushirikiano kwenye hilo mkuu!najua unajua!!

TEC kupitia kanisa wameshaanza maandamano yao kolabo KWA mdude nyagali baada ya waraka kusomwa KWA siku 30!!?

Msalimie Dr.Mpango !!
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi kuhusu Maslahi ya Taifa, ambazo ni kuhusu jambo lolote la Kisiasa, Kiuchumi au Kijamii . Bandiko la leo ni pongezi kwa Rais Samia na serikali yake, kukubali kubadili sheria ya uchaguzi, na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi!. Swali ni Jee Tuanze na mabadiliko ya katiba kwanza ndipo turekebishe sheria au turekebishe tuu sheria, kisha tuingie kwenye uchaguzi Mkuu na katiba hii hii, kisha baada ya uchaguzi wa 2025 ndipo sasa tushughulikie mchakato wa katiba mpya?.

Nilipata fursa kuhudhuria kongamano la siku 3 la vyama vya siasa nchini, lililoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kujadili ripoti ya Kikosi Kazi cha Rais Samia, na mapendekezo yake kuelekea chaguzi za serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu wa 2025, uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, JNICC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Naomba nianze kwa kutoa maoni yangu, kwanza nampongeza Rais Samia kuunda kikosi kazi kutathmini hali ya siasa nchini, nakipongeza kikosi kazi kwa kazi nzuri, naipongeza serikali yetu kwa kukubali mapendekezo ya kikosi kazi, kukubali kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi na kurekebisha Tume ya Uchaguzi kuunda Tume huru na Shirikishi ya uchaguzi.

Kama ulitaka kikubwa, ukapewa kidogo, shukuru kwanza kwa hicho kidogo ulichopewa kisha endelea kuomba kile kikubwa!.

Mzizi wa matatizo yetu yote ya uendeshaji wa siasa zetu, uko kwenye katiba, kwanza ndipo tuje kwenye sheria.

Kufanya mabadiliko ya sheria bila mabadiliko ya katiba, ni sawa na kula bila kunawa, au kuvaa nguo nzuri bila kuoga, ukila bila kunawa bado utashiba tuu, ila matokeo!. Ukivaa nguo nzuri bila kuoga, utapendeza tuu, ila...

Hivyo tunaipongeza serikali yetu kukubali kubadili sheria ya uchaguzi na kutupatia tume huru ya uchaguzi, ila nashauri tuanze kwanza mabadiliko ya katiba ndipo twende kwenye sheria!.

Pendekezo la pili, ni tufanye uchaguzi wote kwa siku moja, na kusimamiwa na Tume moja huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar wanaweza kufanya chaguzi 5 kwa siku moja, Tanzania hatuwezi kushindwa kufanya chaguzi 4 kwa siku moja!. Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!

Hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 halafu uchaguzi Mkuu 2025, kwa sasa tufanye mabadiliko ya katiba na sheria, halafu 2025 tufanye chaguzi zote 4 kwa siku moja, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Madiwani na serikali za mitaa.

Kongamano hilo lilifunguliwa na Rais Samia ambaye ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia mikutano ya hadhara kutoa hoja na fikra zenye tija zinazolenga kuimarisha utendaji serikalini.

Aidha, Rais Samia amevitaka vyama vya siasa kutumia mikutano ya hadhara kujitangaza ili kukua kisiasa na kuutumia uhuru wa kujieleza kutoa mawazo mbadala yatakayoendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Rais Samia pia amesema uhuru wa kutoa maoni kusisababishe kudhalilisha watu
wengine, kuibua hisia za kidini, ukabila au kubaguana kwa misingi yoyote ile.
Vile vile, Rais Samia amesisitiza kutumia uhuru huo vizuri bila kuingilia haki na
uhuru wa watu wengine pamoja na kufuata sheria, kanuni na taratibu.

“Katika shukrani nisisahau Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wakiongozwa na Jaji Mutungi, Jaji Mutungi saa zingine ananipigia simu usiku we mama wee hii kazi uliyonipa nimekwama hapa na hapa, umeaminiwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nenda na kazi yako, ukikwama fedha niambie lakini mengine fanya kazi yako, kwa hiyo nakushukuru umefanya kazi yako na mmefikia pazuri”, alisema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa Serikali imepokea ripoti ya kikosi kazi ambapo Serikali imeyapitia mapendekezo hayo kupitia vikosi kadhaa vilivyongalia mambo kadhaa yanayohitaji wataalamu hususan yanayohusu sheria na Bunge likalo, itapeleka marekebisho ya sheria kadhaa ikiwemo sheria ya uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Rais Samia amesema kuwa Kikosi kazi kimetoa mambo mazuri ambayo serikali kupitia wataalam wake kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi waliopendekezwa wamefanya mapitio ya mapendekezo hayo na kuja na namna bora zaidi ya utekelezaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demeokrasia ya vyama vingi vya siasa, Prof. Rwekaza Mkandara akiwasilisha taarifa ya ripoti yao ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Ally Mwinyi kwa juhudi zao za za kuwaletea Watanzania na Wanzanibar maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hususan kuboresha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulika na masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa ratiba ya utekelezaji itaanza na mabadiliko ya sheria kadha ambazo zitapelekwa Bungeni kwenye Bunge lijalo la October/November ili zifanyiwe mabadiliko.

Kwa vile msingi mkuu na matatizo makuu ya uendeshaji wa siasa zetu yako kwenye katiba, katiba ndio kichwa cha yote na mengine yote ni kiwiliwili.

Kwa vile kuna mchakato wa katiba mpya utakaanza hivi karibuni, lakini kwa minaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na uchaguzi Mkuu wa 2025, tuanze na mabadiliko ya katiba hii hii iliyopo kwa kuibadilisha kwa hati ya dharura, ndipo tuje kwenye mabadiliko ya sheria za uchaguzi na kurekebisha Tume ya Uchaguzi tuunde Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Paskali
Kiukweli hakuna logic ya kufanya chaguzi mbili za nchi nzima in a span of a year.

Sema CCM huwa wanapenda sana kutengeneza magap ya kutumia pesa za umma hovyohovyo.

Kubadilisha sheria za uchaguzi pekee haitatosha kama hatuna adabu ya kufuata hata hizi mbovu zilizopo.

Uvunjifu wa sheria hufanywa na watu wenye naksi ya utu na ukosefu wa maadili.

Je wasimamizi wa sheria hawa wasio na utu na maadili na wenyewe tutawatia utu na maadili ?
 
Nimeacha kusoma bandiko lako baada ya kuona eti Samia karuhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Mkuu Rufiji dam , kuna popote kwenye bandiko hili nimezungumzia mikutano ya vyama vya siasa!.
Samia ni nani juu ya katiba na sheria.
Kumbe wewe hujui kuwa rais wa JMT ndiye katiba, ndiye sheria!, Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
Usiandike kitu huku unawaza uteuzi.
Duh...!, yamekuwa haya!. Mtu niko almost 60!, niwaze teuzi for what?. Unanijua vizuri mimi and what I do?. Hiki ninachofanya compared na ningeteuliwa popote, what is more beneficial kwa nchi yangu?.
P
 
Sitokupa ushirikiano kwenye hilo mkuu!najua unajua!!
Amini usiamini sijui!
TEC kupitia kanisa wameshaanza maandamano yao kolabo KWA mdude nyagali baada ya waraka kusomwa KWA siku 30!!?
Mimi pia Mkatoliki mwenzako ila ni Mtanzania zaidi kuliko Ukatoliki wangu ndio maana tumeliomba kanisa Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? na kuwafungua macho Wakatoliki kuwa Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?
Msalimie Dr.Mpango !!
Salaam zangu za kupindua meza zitamfikia ili baada ya Samia ni zamu ya Mkristo ila this time sio lazima awe Mkatoliki!,ili kuifuta ile kanuni ya siri kuwa akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!.
P
 
Amini usiamini sijui!

Mimi pia Mkatoliki mwenzako ila ni Mtanzania zaidi kuliko Ukatoliki wangu ndio maana tumeliomba kanisa Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? na kuwafungua macho Wakatoliki kuwa Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu?

Salaam zangu za kupindua meza zitamfikia ili baada ya Samia ni zamu ya Mkristo ila this time sio lazima awe Mkatoliki!.
P
"Sio lazima awe mkatoliki" nadhani operation thunderstorms atatufaa a.k.a mkono wa baunsa au sio!!?
 
Hapa ni sawa na kujenga matumaini kwa shetani kwamba atatengeneza mazingira mazuri kwa watakatifu kwenda peponi. Kamwe haitatokea!

Rais Samia anatumia ujanj wa danganya toto unaotumiwa na mama asiyekuwa na chakula cha kuwalisha watoto wake. Anaweka jungu lililojaa mawe jikoni na kuanza kulichochea kuwaaminisha watoto kuwa chakula kipo na kitaliwa kitakapoiva.
 
Kama ulitaka kikubwa, ukapewa kidogo, shukuru kwanza kwa hicho kidogo ulichopewa kisha endelea kuomba kile kikubwa!.
This is rubbish! This is the only language fit for such a statement!. Haramia, jizi, fisadi kapora nguo zako. Anaanza kukupa vest, then unasema kuwa nimepata kidogo nashukuru kwanza angalau kwa vest, suruali na shati vitakuja baadaye1 Una akili kweli?
 
Pascal Mayala wewe ni miongoni mwa Watanzania wachache sana wenye akili lkn,kwa bahati mbaya sana umekuwa ukitumia akili yako vibaya sana kuitetea na kuilinda ccm mitandaoni kwa kuandika upuuzi uliopitiliza.

Suala la Katiba likipelekwa Bungeni wabunge wetu ni watu wenye njaa,ujinga,ushamba na upumbavu kwa 100% maamuzi yao yatatazama usalama wa nafasi zao za ubunge kwa uchaguzi ujao.Kuna kipindi the late Babylon from Chattle alipeleka mswaada wake Bungeni na akawaambia Wabunge "msipoupitisha nalivunja Bunge"

So,hayo yote ni sehemu ya sarakasi za kijinga za ccm!
Kazi kweli kweli
I have no comment !
 
Kuna baadhi ya mambo Hua anayashughulikia vizuri mfano hili ila mengine anakwama sana
 
Back
Top Bottom