Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.

Huyu ndo Pascal Mayalla niliyekuwa namfahamu siyo huyu wa siku hizi.
Hongera Pascal Mayalla wa zamani kwa kutoa maoni mazuri!

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Tusikenue kwenye badiliko la tume ya uchaguzi

Vipi ,kuhusu mamlaka ya rais na kupingwa mahakamani matokeo ya urais

Pascal mayala

Hili hakugusia kabisa! Kama ndio hakuna haja ya tume huru ,najibu swali lako

Ni kwamba ,tupate kwanza katiba mpya na uchaguzi serikali za mitaa uhairishwe
 
Kama Muswada wa Bima ya Afya kwa wote umekwama na kuwekwa kapuni mpaka leo,suala ambalo ni nyeti linahusu maisha na Uhai wa Mtanzania.
Leo waruhusu Tume huru ya Uchaguzi ambayo itapelekea The Green kupoteza madaraka,sahau!
Katiba mpya ilipigwa mweleka Dodoma mwaka 2014.
Hivi Mkuu unaamini kabisa Mwenyekiti wa CCM ataruhusu hayo masuala,kweli!!
"Ogopa sana watu wanaopenda kuimba na kusikiliza muziki wa taarabu"!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Afu tangu huyu jamaa kutuonyesha kuwa,taaluma yake haimripi baasi yote yakawa hovyo.
Kiufupi sipendi mtu ndumilamuwili.
Na hao anaodai ni wachache wanaomwelewa,kwa Great thinker Kama huyu,hoja yake ni dhaifu.

Kiufupi siasa za Nchi hii CCM haiziwezi,maana imejaa viongozi WAJINGA wengi.
 
Pascal Mayala wewe ni miongoni mwa Watanzania wachache sana wenye akili
Mkuu monde arabe , kwanza asante kuniona nina akili miongoni mwa Watanzania wachache, the reality, mimi ni mtu wa kawaida sana, pili Watanzania wenye akili ni wengi kuliko unavyo wafikiria!.
lkn,kwa bahati mbaya sana umekuwa ukitumia akili yako vibaya sana kuitetea na kuilinda ccm mitandaoni
Kutumia akili kufanya jambo lolote la kheri, ni matumizi mazuri ya akili!.
kwa kuandika upuuzi uliopitiliza.
Hii hoja kuwa mimi naandika upuuzi uliopitiliza, naomba tuu niheshimu mawazo yako.
Suala la Katiba likipelekwa Bungeni wabunge wetu ni watu wenye njaa,ujinga,ushamba na upumbavu kwa 100% maamuzi yao yatatazama usalama wa nafasi zao za ubunge kwa uchaguzi ujao.
Naomba niheshimu mawazo yako ila pia kuhusu baadhi ya wabunge wetu, tuliisha waelezea humu Baadhi ya Wabunge ni Stupid!, Tanzania haina Demokrasia!, Bunge ni Rubber Stamp!- TBC, Watch Now!
Kuna kipindi the late Babylon from Chattle alipeleka mswaada wake Bungeni na akawaambia Wabunge "msipoupitisha nalivunja Bunge"
It's very unfortunately hoja hii sikubahatika kusikia, ukinipatia links yoyote ya hii, nitakushukuru
So,hayo yote ni sehemu ya sarakasi za kijinga za ccm!
Hapa kwenye sarakasi za kijinga za CCM, naomba niheshimu maoni yako, ila ukiona watu wanafanyiwa sarakasi za kijinga mwaka hadi mwaka, then wajinga sio wafanya sarakasi bali wafanyiwa sarakasi!.
P
 
Kwanini ashukuriwe? Sheria zetu sizinaruhusu? kwanini mnadhani ni hisani
 
Ashinde Uchaguzi kihalali sio abebwe na vyombo vya Dola
Mkuu imhotep , hili la kushinda kihalali, nalo neno!, kama nilivyoshauri kwenye bandiko hili, katiba ndio msingi Mkuu wa haki, tatizo lulilopo ni kwa CCM, sio tuu ni chama cha siasa, bali ni chama dola!. CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! hivyo vyombo vya dola kuibeba CCM, kavyo ni kutimiza wajibu wake!. Hivyo dawa ni katiba, iivue CCM udola wake, uwanja wa siasa uwe levelled ndipo kipute kipigwe!.
P
 
HAKI haiombwi!
Mkuu Rabbon , ni kweli haki haiombwi, wala haki sio hisani, bali ni stahiki na stahili inayopaswa kutolewa na isipotolewa, haiombwi bali inadaiwa!. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
na Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
Tume huru ya Uchaguzi ni Hadi vifungu muhimu vya Katiba vibadilishwe.
Ni kweli, naunga mkono hoja.
Matokeo ya Urais yahojiwe mahakamani.
Hili ni la kwenye katiba mpya.
Na Rais aondolewe Kinga ya kutoshtakiwa, wote tuwe sawa mbele ya SHERIA.
Hili hapana!.
P.
 
Mkuu natumai umesoma sheria na una uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo

Hili jambo umeliweka hapa ni kana kwamba tunaishi kwa kudra na nchi yetu inamilikiwa na aliye juu kiuongozi na siyo umiliki wa wananchi.

Tume Huru ya Uchaguzi siyo hisani
Katiba Mpya siyo hisani mkuu.
Haki yetu inadai uwajibikaji wa wenye dhamana. Hivyo ondoa ktk mawazo kwamba Mama anatutendea hisani na tunapaswa kumshukuru.

Tutambue wajibu wetu wa kujitambua
 
Pamoja sana ndugu yangu Pascal Mayalla, maoni yangu yanatekelezwa hivi sasa.
Asante.
sinaga shaka na makala zako ambazo huwa zinastaili ya zile nyaraka katoliki.
Duh...!
unanisakazia niseme jambo ila itoshe tu kusema sina maoni
No sikukazii kusema jambo, miongoni mwa haki, pia kuna haki ya kunyamaza, the right to remain silent.
Tena mimi ni mwalimu wa somo la kujifunza kunyamaza Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
 
Mkuu natumai umesoma sheria na una uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo
Mkuu Msanii , kwanza asante kwa utambuzi huu, ni kweli nina uwezo sio mkubwa wa kuchanganua mambo, uwezo wangu ni wa wastani tuu, na wala sio kwa sababu ya kusoma sheria, ni exposure tuu ya miaka 30 newsroom!. Wako wanasheria manguli wabobezi na wabobevu ila ndio waliotufanyia Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Hili jambo umeliweka hapa ni kana kwamba tunaishi kwa kudra na nchi yetu inamilikiwa na aliye juu kiuongozi na siyo umiliki wa wananchi.
Hapana, nimesema tuwe watu wa shukrani kwa madogo ili tupatiwe makubwa!. Japo haki ni stahiki kuna vitu Rais Samia anavifanya kwa hisani tuu. Samia ameingia madarakani akakuta hakuna issue yoyote ya katiba mpya kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo ameunda kikosi kazi kwa hisani tuu, lazima tuseme asante Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Tume Huru ya Uchaguzi siyo hisani
Tume ya uchaguzi iliyopo ni tume huru ila sio Shirikishi, Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais
Katiba Mpya siyo hisani mkuu.
Kwa vile haipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, kitendo cha Samia kuanzisha mchakato ni kwa hisani tuu!
Haki yetu inadai uwajibikaji wa wenye dhamana. Hivyo ondoa ktk mawazo kwamba Mama anatutendea hisani na tunapaswa kumshukuru.
Natambua haki sio hisani Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
Tutambue wajibu wetu wa kujitambua
Naunga mkono hoja, Watanzania wanatakiwa wasaidiwe kuelimishwa ili wajitambue na kutambua haki zao. Hii kazi mimi nimeianza kwa kujitolea Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

- Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?

P
 
Nilianza kusoma majibu yako nikiwa nimetuna sana lakini hadi mwisho wa passage nimeelimika kiasi fulani.

Kuna baadhi ya hoja zangu umezidadavua ktk majibu yako kwangu. Bado nahisi tunahitaji sasa kuondokana na hili suala la HEWALA x 2 kwani ndilo linalojenga jamii ya kuishi kwa hisani kila jambo ambalo ni haki na wajibu.

Nashukuru yes
 
Sidhani kama jamaa watakubali levelling.....
 
Asante, niliwahi kuuliza Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…