Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.

Mimi nina mashaka inaundwa tume huru ya aina gani. Ninamashaka sana kama muundo wa tume hiyo huru inapojadiliwa kwenye bunge hili la chama kimoja.
Lazima watatengeneza tume huru yenye muundo wa kuegemea upande mmoja. Hii itakua ni kuwazubaisha watanzania.
Isipokua kwa muundo wa aina yoyote ila inaleta picha ya kule tunakoelekea hata kwa miaka kadhaa mbele tunaweza kupata kile watanzania wanachokilia..ila kwa sasa naamini hata ikiundwa tume huru bado itakua ya ccm.
 
Msemaji mkuu wa Serikali.
 
Kwanini ashukuriwe? Sheria zetu sizinaruhusu? kwanini mnadhani ni hisani
1. Amefufua mambo ya upatikanaji wa katiba mpya, mambo ambayo mtangulizi wake alisema siyo kipaumbele chake na hatukumfanya chochote, hata alipozuia mikutano ya kisiasa na UKUTA mkwara mmoja tu wa "mtapigwa hadi mchakae" ulitosha kuzima ukuta. 2. Hata leo samia akiamua kufuata nyayo za magu hakuna mtanganyika wa kuandamana kupinga, sana sana watamwachia Mungu. 3. Marekebisho ya muundo wa sheria za uchaguzi haya yote raisi ameyaridhia na alikuwa na uwezo wa kuwaminya wapinzani kama magu alivyofanya 2020 na wanakondoo wa tanganyika tusingemfanya chochote na ccm chama dola kingeshinda au kushindishwa kwa kishindo.
 
Sasa haki yetu tushukuru kitu gani mkuu
 
Vikosi kazi vya nini? Tunayo katiba pendekezwa iliyo tokana na bunge la katiba, kwanini tusianzia hapo, tuendelee. Nafahamu mapungufu yake ni pale Ukawa walipojitoa CCM ika hodhi mchakato mzima na kuja na katiba pendekezwa, hilo ndio lilikuwa kosa. lakini tungeanzia kuchakata maoni ya Tume ya warioba na Bunge la katiba likae tena tupate katiba.
CCM wakiachiwa wanaharibu makusudi, na hao ndio kikosi kazi.
 
Shida ya wewe wakili msomi (Adv),Freelance Journalist, Columnist n.k Pascal Mayalla unapenda sana siasa zakujipendekeza ili uteuliwe ndiyo mana kabla ya uhai wa marehemu Jiwe alikuchana laivu ..eti wewe ni mganga njaa unawazia tumbo lako tuu.
 
Swali ni Jee Tuanze na mabadiliko ya katiba kwanza ndipo turekebishe sheria au turekebishe tuu sheria, kisha tuingie kwenye uchaguzi Mkuu na katiba hii hii, kisha baada ya uchaguzi wa 2025 ndipo sasa tushughulikie mchakato wa katiba mpya?.
Katiba ni 'sheria mama' kwamba zingine zote zinatengenezwa kwa kuiakisi.

Haiwezekani kupata Tume huru ya uchaguzi bila kugusa Katiba kwasababu Tume ya uchaguzi ipo kikatiba.
Kuanza na Sheria ni kuweka viraka . Watu wenye akili na weledi huanza na msingi na hapa ni Katiba! period
Hakukuwepo sababu ya kuunda kikosi kazi.

Tume ya Nyalali na mapendekezo yake yapo. Tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Balozi Amina Salum, Tume ya Mzee Warioba.

Tume hizi ziliundwa na kwenda kwa Wananchi kuchukua maoni.

Tume ya Mkandara imepewa hadidu za rejea na SSH halafu imeita watu wawili watatu ikamaliza na kusema ni maoni ya Watanzania.

Pasco, unafahamu ukweli huu na kwamba kilichofanyika ni ghiliba tu, Tume ya Prof Mkandara ni upuuzi wa kupoteza muda , pesa na kudanganya watu.

Kwa bahati mbaya Prof Mkandara ni wale wale akina Prof Bana n.k, ni machawa tu kama chawa wengine.
Kama ulitaka kikubwa, ukapewa kidogo, shukuru kwanza kwa hicho kidogo ulichopewa kisha endelea kuomba kile kikubwa!.
Tanzania ni mali ya Watanzani si mali ya mtu au kikundi cha watu.
Haki haiombwi inadaiwa. Hao wanaotoa hiyo haki si wafalme au malkia ni watumishi wanaolipwa na kodi zetu.

With all due respect haya mawazo ya kupewa hata haki yako ni very archaic and pathetic
Rais Samia amesema kuwa Kikosi kazi kimetoa mambo mazuri ambayo serikali kupitia wataalam wake kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi waliopendekezwa wamefanya mapitio ya mapendekezo hayo na kuja na namna bora zaidi ya utekelezaji.
Tunarudi pale pale, Rais anajipongeza kwa kufanya ghiliba. Tume ya Nyalali, Kisanga, Amina, Warioba zipo, kulikuwa na haja gani ya kuunda kikosi kazi ambacho kimehoji watu wasiozidi 2000 eti ndio Watanzania.

Anachokifanya SSH ni kukwepa suala la Muungano , kutumia katiba ya sasa kubaki madarakani.

Zama zimebadilika na tunaweza kuona nini kinatokea kwa generations za nchi nyingine.

Yanayotokea kwa Omar Bongo ni haya haya ya kudhani Wananchi ni wapumbavu na kila siku watabaki hiyo.
Bila katiba mpya SSH atakuwa na wakati mgumu sana. Hii ni generation tofauti.
Tazama chawa anavyofanya kazi. Mambo ya uchumi yanahusu vipi? Haya ya kuwaletea maendeleo yanatoka wapi? Prof anaongea ' kuleta maendeleo kama wagombea udiwani'

Rais aliomba kazi akifanya kazi yake hakuna hisiani ni wajibu. Tuna matatizo ya prof Tanzania, yaani akina Benson na Mkandara ni ''protoype '' ya elimu na kielelezo cha kushuka kwa elimu yetu

Sorry Pasco, I'll call a spade a spade !

JokaKuu
 
umeisoma miswada ? wa tume ya uchaguzi ikoje? Kuna tume huru pale?
 
Mambo yameanza!, mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni haya...
.... loading

P
 
sasa ulisifia nini Pascal? CCM hawawezi kuachia nchi kwa uchaguzi..........nilijua na nimetoa harsh comment kwako maana kwa level yako unajua fika kuwa ccm haiwezi kuleta tume huru maana wanajua ikiwepo wanaondoka....
Tatizo la Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru ila ilikuwa sio shirikishi!, kwenye muswada huu bado sijauona huo ushirikishi, hivyo huu ni mvinyo ule ule wa zamani ila kwenye chupa mpya!.

P
 
Tatizo la Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru ila ilikuwa sio shirikishi!, kwenye muswada huu bado sijauona huo ushirikishi, hivyo huu ni mvinyo ule ule wa zamani ila kwenye chupa mpya!.

P
Nilitegemea rais asiwe na ushiriki wowote ktika kuteua commissioners wa tume na kama ulivyosema uwe shirikish
 
Hakuna mwana CCM hata mmoja anayethubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi.
Wewe Paskali huwezi kuthubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi, hususan kwenye 'forum' za CCM.
Duh...!, Mkuu fundimchundo , karibu bandiko hili, jee hapa ninadai nini?.
P
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…