Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

Kwa akili zako zinazoingia na kutoka ulidhani mtapangia mpaka BBC na media zote za nje nini waandike na nini wasiandike

Na bado si alienda ule upande mwingine pinzani wa hizo Media,serikali haramu itapigwa virungu kiasi kwamba haitaweza kusimama wala kulala.
 
Mkuu hata wewe ni Chawa?mbona BBC Wapo Sawa na wanatusaidia kwa sababu vyombo vyetu vya usalama vimetekwa.
 
Very soon na huyu Pascal Mayalla namuweka kwenye ignore list, "huwezi kuwa unawazodoa waajiri wako ambao ni wananchi, unawa-harass, unawa-mistreate alafu utegemee wao wawe positive na constructive. Huelewi unataka nini ndugu mwandishi wa level ya chini kabisa. Inawezekana kweli ukawa unaelimu ya Ilboru, ila hakika haijakukomboa bado". Imebidi niji-quote mwenyewe.

Kusoma Ilboru na kusomea sheria UDSM kulipaswa kukupa ukombozi wa kifikra, siyo kukugeuza kuwa mkalimani wa mabavu ya dola dhidi ya wananchi. Ni aibu kwa msomi wa kiwango chako kuacha kutetea haki za wananchi walioajiri serikali, na badala yake unajigeuza kuwa ngao ya kuhalalisha unyanyasaji. Elimu yako haijakukomboa kama bado hujaelewa kuwa mwanahabari anasimama na umma, sio na rungu la watawala. Rudi shule ukajifunze unyenyekevu!

Hivi Pascal, ule mzigo wa kutakiwa kuthibitisha maneno yako na Bodi ya Ithibati (JAB) bado haujakufundisha adabu ya kitaaluma? Mwanasheria mzima unaruka ruka kati ya uchambuzi wa kina na umbea wa kisiasa. Unapoteza hadhi ya uandishi mkongwe kwa sababu ya njaa ya kutaka kukumbukwa na mfumo. Hakika wewe ni mwandishi wa kiwango cha chini kabisa uliyebakiza 'uchawa' kama mtaji wako wa mwisho. Wananchi wamekushtukia, ignore list inakuhusu!

Pascal Mayalla, kalamu yako imeoza. Umepoteza sifa ya kuwa sauti ya wasio na sauti na sasa umekuwa msemaji wa mabavu ya dola. Shule ya Ilboru na digrii ya sheria ya UDSM zimetumika vibaya sana kukuzalisha wewe. Hakuna tija ya kukusikiliza mtu unayewazodoa wananchi wanaoteseka ili ufurahiwe na watawala. Umeshuka hadhi, na hapa ndio mwisho wa kukufuatilia. Bye!
 
we mzee siku wakishtukia kalamu yako ina maana gani.....safari hiyo watakuletea zengwe kubwa zaidi ya lile.
 
wewe ni wa kugongwa "ignore" tu
 
Pascal wachache sana watakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…