Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

Wanabodi

Hili ni bandiko la pongezi kwa serikali yetu ikifanya jambo lolote zuri la kustahili pongezi, tuipongeze, na ikifanya jambo lolote baya la kustahili kukosolewa tuikosoe kwa constructive criticism, ukosoaji wa kujenga, sio ukosoaji wa kuzodoa au kubagaza.

Juzi Jumapili tarehe 12 Julai, limepandishwa bandiko hili humu jf BBC News Africa: Tundu Lissu: A Fight Too Far?

Thanks for this, kuendeleza ile the jf spirit of being the first to know, na kitendo and kutuletea humu kumeifanya sisi Watanzania wa kawaida kuiona na mamlaka zetu to respond.

Jana Jumatatu tarehe 13 Julai Serikali yetu imejibu mapigo Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi

Kwa hatua hii pekee ya Serikali yetu kuujibu upotoshaji wa BBC, ni hatua ya kustahili pongezi za dhati, ila tunapobagazwa kupitia chombo fulani, tujibu mapigo kwa kutumia chombo kile kile.

Hii sio mara ya kwanza kwa BBC kutubagaza, huko nyuma BBC iliwahi kutubagaza nikauliza humu GE2020 - Uongo na Upotoshaji huu wa BBC London kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni una maana gani? Sio mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa ki-BBC?

Mfano tumebagazwa kwa TV documentary kupitia BBC, kanusho letu lisiishie hivi vyombo vyetu vya madafu, tukanushie kule kule BBC. Sio tunabagazwa BBC, kisha tunakanushia TBC!.

Tanzania tuna balozi zetu nchi zote za kibeberu, tukibagazwa na BBC, Balozi wetu London atinge BBC kujibu mapigo, kama alivyofanya Balozi Matinyi akiwa Sweden Pongezi Balozi Wetu Sweden, Mobhare Matinyi. Alichofanya Kiigwe na Kifanywe na Balozi Zetu ZoteView attachment 3628853

Ni muda mrefu nimekuwa nikashauri likitokea jambo lolote la ku attract international media attention, nimeshauri lets be proactive rather than reactive kwa kulizungumzia kwa ukweli na uwazi ili kuwa preempt mabeberu, wasio tutakia mema, na sio kusubiria mpaka tunabagazwa tunachafuliwa ndipo tunakuwa reactive kwa kujibu mapigo, by that time the damage has already been done!.

Niliwahi kuuliza humu Thread 'Tanzania ni Tunachafuliwa Au ni Wachafu?, Uongo Ukisemwa Sana, Usipokanushwa, Unageuka Ukweli!. Kwanini Tumenyamazia Uchafuzi Huu?!, Tunyamaze Tuu au?' Tanzania ni Tunachafuliwa Au ni Wachafu?, Uongo Ukisemwa Sana, Usipokanushwa, Unageuka Ukweli!. Kwanini Tumenyamazia Uchafuzi Huu?!, Tunyamaze Tuu au? View attachment 3628854

Nimeiangalia hii documentary, kila kilichosemwa ni ukweli mtupu, mwisho wa documentary wameweka disclaimer kuwa waliwatafuta upande wa pili, ili ku balance their story, we refused to respond, hivyo as far as balance is concerned, ukimtafuta mtu wa kubalace akagoma kutoa ushirikiano, BBC kama media, Wametimiza wajibu wao, wame published one sided documentary na wamebalance.

Kwenye taarifa ya serikali serikali yetu wamesema hatutanyamaza, nashauri, sio tuu tujibu mapigo, bali tujibu mapigo kwa documentary ya kuusema ukweli, Tanzania tunazo media zenye uwezo wa ku produce documentary za ukweli na kuzirusha huko huko BBC!.

Baada ya kutokea kilichotokea October 29, nilishauri humu PostGE2025 - Ushauri: Tangazeni idadi ya Vifo, na Ikibidi Hata Idadi ya Uongo tuu ili Wanyamaze!. Gazeti la “The Sun” limeiita Tanzania HOUSE OF BLOOD

Nikashauri tena, Ushauri Kwa Serikali Yetu, Ili Kuisafisha Tanzania Kimataifa, Tumieni Dekio la Scapegoat Mop, Kusafisha Madoa ya Damu ya October 29!.

Ripoti ya Jaji Chande ilipotoka nikashauri PostGE2025 - Kwenye ukweli uongo hujitenga!, Baada ya idadi ya Vifo 518 kutolewa; Je, tuwashitaki wazushi waliotuchafua kwa Uzushi wa Maelfu ya Vifo?

Sisi kama Watanzania na media zetu hatukutimiza wajibu wetu kikamilifu PostGE2025 - Kilichotokea Oct 29, Pamoja na Media ya TZ Kutotimiza Wajibu Wetu Kikamilifu, Bado Tuna Wajibu! Kwanini Hatutimizi Wajibu Wetu Baada ya Tukio?

Mpaka akatokea mtu baking wa nje kuja kutusaidia What Happened in Oct. 29: Pongezi Balile wa TEF Kwa Uzalendo, Ila Tanzania Tunatia Aibu!. Tutategemea Wageni Mpaka Lini?!. Tujenge Uwezo wa Ndani!.

Hitimisho
Tanzania tutaendelea kusemwa vibaya na hizi documentaries za mabeberu mpaka lini?, mimi kwa vile nimefanya kazi kwenye media ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 30, naomba kusema ukweli mchungu, kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya umma, kuanzia Idara ya Habari Maelezo, TBC, Daily News, hazina watu wa kujibu mapigo BBC, CNN, DWTV, Al Jazeera au SABC, lakini kwenye sekta binafsi Waandishi hao tunao, na vyombo vya kutengeneza hizo documentaries tunavyo ila lazima viwezeshwe!.

Tufike mahali Watanzania tujisikie aibu kufanyiwa kila kitu na wageni, hadi documentaries tunafanyiwa na wageni sisi kazi yetu ni kukanusha tuu!, vitu vingine ni vitu vidogo vodogo ambavyo wenyewe tunaviweza!. Ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli, maendeleo endelevu, hatuwezi kuendelea kwa kuwategemea wageni ndio watuletee maendeleo!, maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe, kwa kujengewa uwezo wa ndani wa kujiletea maendeleo, hivyo hata hiki kilichotokea nchini kwetu ile October 29, baada ya kuweka mapendekezo yangu ya nini kifanyike, sitegemei kusikia sisi media ya Tanzania, tukiemdelea kusimangwa na kutukanwa kuwa hatujafanya lolote!. Tuwezesheni tufanye kama nilivyo shauri hapa

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.

Mzee Pasco
uzalendo ni kunyamazia maovu sio?
Kuzeeka bila hekima na busara ni hatari
 
Very soon na huyu Pascal Mayalla namuweka kwenye ignore list, "huwezi kuwa unawazodoa waajiri wako ambao ni wananchi, unawa-harass, unawa-mistreate alafu utegemee wao wawe positive na constructive. Huelewi unataka nini ndugu mwandishi wa level ya chini kabisa. Inawezekana kweli ukawa unaelimu ya Ilboru, ila hakika haijakukomboa bado". Imebidi niji-quote mwenyewe.

Kusoma Ilboru na kusomea sheria UDSM kulipaswa kukupa ukombozi wa kifikra, siyo kukugeuza kuwa mkalimani wa mabavu ya dola dhidi ya wananchi. Ni aibu kwa msomi wa kiwango chako kuacha kutetea haki za wananchi walioajiri serikali, na badala yake unajigeuza kuwa ngao ya kuhalalisha unyanyasaji. Elimu yako haijakukomboa kama bado hujaelewa kuwa mwanahabari anasimama na umma, sio na rungu la watawala. Rudi shule ukajifunze unyenyekevu!

Hivi Pascal, ule mzigo wa kutakiwa kuthibitisha maneno yako na Bodi ya Ithibati (JAB) bado haujakufundisha adabu ya kitaaluma? Mwanasheria mzima unaruka ruka kati ya uchambuzi wa kina na umbea wa kisiasa. Unapoteza hadhi ya uandishi mkongwe kwa sababu ya njaa ya kutaka kukumbukwa na mfumo. Hakika wewe ni mwandishi wa kiwango cha chini kabisa uliyebakiza 'uchawa' kama mtaji wako wa mwisho. Wananchi wamekushtukia, ignore list inakuhusu!

Pascal Mayalla, kalamu yako imeoza. Umepoteza sifa ya kuwa sauti ya wasio na sauti na sasa umekuwa msemaji wa mabavu ya dola. Shule ya Ilboru na digrii ya sheria ya UDSM zimetumika vibaya sana kukuzalisha wewe. Hakuna tija ya kukusikiliza mtu unayewazodoa wananchi wanaoteseka ili ufurahiwe na watawala. Umeshuka hadhi, na hapa ndio mwisho wa kukufuatilia. Bye!
Ndio maana Msukuma, namkubali Ingawa Yuko mboga mboga!
 
Hivi tunaweza kuwa wanahabari kama Andrew Neil wa Times Radio zamani alikua BBC. Angalia anavyo mbana huyu mwanasiasa Michael Gove pia Waziri wa serikali ya Boris Johnson. Unauliza swali likikwepwa unapiga follow up wakati nduyu yetu Mayalla aliuliza swali nzuri hakujibiwa na akaitwa jina lake maana yake ni njaa akaridhika na watanzania wakaimba mampambio ya kumsifu Mayalla. nadhani nilikua peke yangu nilizikataa zile sifa.


View: https://www.youtube.com/watch?v=uSxY0zY58Uo
 
Ndugu Pascal Mayalla,
Nimesoma kwa umakini mkubwa bandiko lako hili la pongezi na ukosoaji kwa Serikali na Vyombo vya Habari. Kama kawaida yako, umejaribu kucheza mchezo wa "kuuma na kupuliza" (calculated diplomacy) ili kufikisha ujumbe wako. Hata hivyo, kuna maeneo makubwa kwenye bandiko lako ambayo yanakinzana kiwango cha kusikitisha, hasa ukitembea kwenye viatu vyako viwili: kama Mwandishi wa Habari/Broadcaster Mkongwe na kama Mwanasheria (Advocate).
Naomba nikuwekee kioo utazame hoja zako zilivyojigonga:

1. Kitendawili cha "Kushauri Serikali Iseme Uongo" vs. Maadili ya Taaluma Yako
Katika bandiko lako, umekumbushia ushauri wako wa nyuma kuhusu matukio ya Oktoba 29 ukisema: “...nilishauri humu PostGE2025 - Ushauri: Tangazeni idadi ya Vifo, na Ikibidi Hata Idadi ya Uongo tuu ili Wanyamaze!.”
Ndugu Pascal, hapa ndipo nilipopigwa na butwaa. Wewe ni Mwanasheria unayejua maana ya "Perjury" (kutoa ushahidi wa uongo) na unajua kuwa misingi ya sheria inasimama kwenye Haki na Ukweli (Fiat justitia, ruat caelum). Wakati huo huo, wewe ni Broadcaster mwenye uzoefu wa miaka 30+ unayejua kuwa kanuni ya kwanza ya uandishi wa habari duniani kote ni Ukweli na Usahihi (Truth and Accuracy).
Je, tasnia ya habari na sheria zinamruhusu vipi mtaalamu nguli kama wewe kuishauri serikali itengeneze "uongo wa makusudi" ili tu kuwanyamazisha watu au mabeberu? Uongo wa serikali kwenye matukio ya umwagaji damu haujawahi kusafisha nchi, badala yake huwa unazika ukweli na kuacha madoa ya kudumu. Kitendo cha kuandika kuwa serikali iseme uongo kinakinzana kabisa na viapo vyako vyote viwili—cha uandishi na cha uwanasheria.

2. Ndoto ya Kurusha Makala ya Serikali Kule Kule BBC
Umeshauri kuwa tujibu mapigo kwa kutengeneza makala kupitia sekta binafsi na “kuzirusha huko huko BBC!”. Hoja hii inaonyesha ama umesahau jinsi mifumo ya vyombo vya kimataifa inavyofanya kazi, au unajisahaulisha kwa makusudi.
BBC inasimamiwa na Mwongozo mkali wa Uhariri (Editorial Guidelines). Hawaruhusu, hawajawahi, na hawatakuja kuruhusu makala inayofadhiliwa au kushinikizwa na serikali yoyote ile (state-sponsored content) ili kusafisha taswira yake ya kisiasa. Huwezi kuwatumia BBC kusafisha kile walichokichunguza wenyewe. Mkakati pekee wa kujibu BBC ni kuruhusu uhuru wa habari ndani ya nchi ili ukweli utoke mapema, sio kusubiri mpaka uchafuliwe ndipo ukaombe airtime BBC kukanusha.

3. Ukweli Mchungu: Kama BBC Wamesema Ukweli, Serikali Inakanusha Nini?
Umeandika hapa: “Nimeiangalia hii documentary, kila kilichosemwa ni ukweli mtupu...” na hapo hapo juu ukapongeza tamko la serikali la kukanusha ukisema: “Kwa hatua hii pekee ya Serikali yetu kuujibu upotoshaji wa BBC, ni hatua ya kustahili pongezi za dhati...”
Hapa unajikanyaga waziwazi. Kama kila kilichosemwa na BBC kwenye makala ya Tundu Lissu ni "ukweli mtupu", serikali yetu inapongezwa kwa kukanusha upotoshaji gani? Maana yake unapongeza serikali kwa kukanusha ukweli? Huku sio kusimamia weledi, huu ni mkakati wa kutafuta usalama wako ili usionekane adui wa mfumo, huku moyoni ukijua wazi kuwa BBC wako sahihi na upande wetu ulizubaa kwa kugoma kujibu (Refused to respond).

Hitimisho na Swali la Kizushi Kwako:
Ndugu Pascal, kwenye ukweli, uongo huwa unajitenga. Naomba nikuulize kwa uwazi kabisa: Je, umeandika makala hii kwa uhakika na dhati ya moyo wako, ama leo umeamua kujigeuza kuwa CHAWA wa serikali ili kuepukana na maswaiba na dhoruba ulizozipitia hivi karibuni?
Ukweli ni kwamba, Mayalla mimi niliandika makala ya kukusifu hivi karibuni nikiwa nakuamini kama sauti huru na thabiti, lakini leo kwa bandiko hili naona umewaangusha sana Watanzania wote wanaokuamini na kukuheshimu. Huwezi kuwa mwanasheria anayeshangilia uongo, na huwezi kuwa mwandishi anayependekeza propaganda za kizamani ili kulinda usalama wa kibinafsi.

Wako katika ujenzi wa taaluma,

Mtani wako Kutoka Mto Lumemo Ifakara
Wewe jamaa ni noma!Una madini!Mwaga tuelimike.
 
Mkuu hp4510, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, kwani mwandiko huu wa sasa wa Pascal Mayalla haufanani kabisa na yule mwanahabari nguli na makini tuliyemzoea. Inashangaza na kusikitisha sana kuona mtu anayejua fika ukweli wa vifo na ukandamizaji uliotokea Oktoba 29 leo hii anageuka na kuipongeza serikali kwa kuishambulia BBC inayofichua ukatili huo. Huyu ndiye Mayalla aliyewahi kulizungumzia hili huko nyuma, lakini sasa amekuwa mstari wa mbele kutetea propaganda zinazofunika damu ya Watanzania waliopoteza maisha. Kubadilika huku kwa ghafla kunathibitisha kabisa hoja yako kuwa aidha kalamu yake imenunuliwa, au kadi yake ya 'press' sasa hivi inatumikia maslahi na matumbo ya watu wengine badala ya ukweli na wananchi.
Jana alitoa bandiko la tuvumiliane hapa Jf na maelezo kibao, kumbe analake jambo!Ndio utumbo huu wa Leo.
 
Ninachojua P.anafanya makusudi, kupima upepo, Maana Kwa maelezo yake katika bandiko lake flani kaelezea kwamba ametokwa sana nje ya Nchi za wenzatu!Hivyo anajua mambo vizuri!
 
Kumuaminisha mtu asiye na chongo wala ubovu wowote wa macho mchana kweipee ati unamlazimisha aamini kwamba hio ni usiku wa manane na hilo jua ni mwezi uliochangamka kiukweli utaishia kupata taabu mwenyewe
 
Back
Top Bottom