Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

Mimi niko upande wa hao BBC. Nawaunga mkono kwa 100%. Muda wa kuitetea au kujipendekeza kwa serikali ambayo haikuchaguliwa kihalali na wananchi haupo.

Kukimbia uchaguzi akuifanyi serikali iliyochaguliwa na wengine isiwe halali.Kumbuka ,Rais upatikana kwa kuchaguliwa kwa kula nasio kwa wingi wa wanachama wa chama flani.
 
Hivi CHADEMA sijui mko na shida gani? Yaani mtu akiisema serikali vizuri au kutetea nchi yake mnaona kama mjinga na chawa ,vipi nyie mnaotukana na kubagaza na kushabikia mabeberu ndiyo wazalendo.?
 
Ndugu Pascal Mayalla,
Nimesoma kwa umakini mkubwa bandiko lako hili la pongezi na ukosoaji kwa Serikali na Vyombo vya Habari. Kama kawaida yako, umejaribu kucheza mchezo wa "kuuma na kupuliza" (calculated diplomacy) ili kufikisha ujumbe wako. Hata hivyo, kuna maeneo makubwa kwenye bandiko lako ambayo yanakinzana kiwango cha kusikitisha, hasa ukitembea kwenye viatu vyako viwili: kama Mwandishi wa Habari/Broadcaster Mkongwe na kama Mwanasheria (Advocate).
Naomba nikuwekee kioo utazame hoja zako zilivyojigonga:

1. Kitendawili cha "Kushauri Serikali Iseme Uongo" vs. Maadili ya Taaluma Yako
Katika bandiko lako, umekumbushia ushauri wako wa nyuma kuhusu matukio ya Oktoba 29 ukisema: “...nilishauri humu PostGE2025 - Ushauri: Tangazeni idadi ya Vifo, na Ikibidi Hata Idadi ya Uongo tuu ili Wanyamaze!.”
Ndugu Pascal, hapa ndipo nilipopigwa na butwaa. Wewe ni Mwanasheria unayejua maana ya "Perjury" (kutoa ushahidi wa uongo) na unajua kuwa misingi ya sheria inasimama kwenye Haki na Ukweli (Fiat justitia, ruat caelum). Wakati huo huo, wewe ni Broadcaster mwenye uzoefu wa miaka 30+ unayejua kuwa kanuni ya kwanza ya uandishi wa habari duniani kote ni Ukweli na Usahihi (Truth and Accuracy).
Je, tasnia ya habari na sheria zinamruhusu vipi mtaalamu nguli kama wewe kuishauri serikali itengeneze "uongo wa makusudi" ili tu kuwanyamazisha watu au mabeberu? Uongo wa serikali kwenye matukio ya umwagaji damu haujawahi kusafisha nchi, badala yake huwa unazika ukweli na kuacha madoa ya kudumu. Kitendo cha kuandika kuwa serikali iseme uongo kinakinzana kabisa na viapo vyako vyote viwili—cha uandishi na cha uwanasheria.

2. Ndoto ya Kurusha Makala ya Serikali Kule Kule BBC
Umeshauri kuwa tujibu mapigo kwa kutengeneza makala kupitia sekta binafsi na “kuzirusha huko huko BBC!”. Hoja hii inaonyesha ama umesahau jinsi mifumo ya vyombo vya kimataifa inavyofanya kazi, au unajisahaulisha kwa makusudi.
BBC inasimamiwa na Mwongozo mkali wa Uhariri (Editorial Guidelines). Hawaruhusu, hawajawahi, na hawatakuja kuruhusu makala inayofadhiliwa au kushinikizwa na serikali yoyote ile (state-sponsored content) ili kusafisha taswira yake ya kisiasa. Huwezi kuwatumia BBC kusafisha kile walichokichunguza wenyewe. Mkakati pekee wa kujibu BBC ni kuruhusu uhuru wa habari ndani ya nchi ili ukweli utoke mapema, sio kusubiri mpaka uchafuliwe ndipo ukaombe airtime BBC kukanusha.

3. Ukweli Mchungu: Kama BBC Wamesema Ukweli, Serikali Inakanusha Nini?
Umeandika hapa: “Nimeiangalia hii documentary, kila kilichosemwa ni ukweli mtupu...” na hapo hapo juu ukapongeza tamko la serikali la kukanusha ukisema: “Kwa hatua hii pekee ya Serikali yetu kuujibu upotoshaji wa BBC, ni hatua ya kustahili pongezi za dhati...”
Hapa unajikanyaga waziwazi. Kama kila kilichosemwa na BBC kwenye makala ya Tundu Lissu ni "ukweli mtupu", serikali yetu inapongezwa kwa kukanusha upotoshaji gani? Maana yake unapongeza serikali kwa kukanusha ukweli? Huku sio kusimamia weledi, huu ni mkakati wa kutafuta usalama wako ili usionekane adui wa mfumo, huku moyoni ukijua wazi kuwa BBC wako sahihi na upande wetu ulizubaa kwa kugoma kujibu (Refused to respond).

Hitimisho na Swali la Kizushi Kwako:
Ndugu Pascal, kwenye ukweli, uongo huwa unajitenga. Naomba nikuulize kwa uwazi kabisa: Je, umeandika makala hii kwa uhakika na dhati ya moyo wako, ama leo umeamua kujigeuza kuwa CHAWA wa serikali ili kuepukana na maswaiba na dhoruba ulizozipitia hivi karibuni?
Ukweli ni kwamba, Mayalla mimi niliandika makala ya kukusifu hivi karibuni nikiwa nakuamini kama sauti huru na thabiti, lakini leo kwa bandiko hili naona umewaangusha sana Watanzania wote wanaokuamini na kukuheshimu. Huwezi kuwa mwanasheria anayeshangilia uongo, na huwezi kuwa mwandishi anayependekeza propaganda za kizamani ili kulinda usalama wa kibinafsi.

Wako katika ujenzi wa taaluma,

Mtani wako Kutoka Mto Lumemo Ifakara
 
Mkuu sikuelewagi unaingia na kutoka, au we ndi ndumi la kuwili?
Hata mimi huwa namshangaa kuna muda anakuwa mkosoaji kuna muda anageuka kuwa chawa labda anafanya hivyo kuuza gazeti tu hata kama anachoongea hakina uhalisia.
Maana kwenye uzi wote ameishia kulalamika tu na kusifia sijaona alipochambua huo upotoshaji
 
Waambie CCM kama wanataka kuvuliwa nguo mchana kweupe wajaribu kujibu mapigo...wakumbushe kuwa hii documentary sio mapigo Bali ukweli mtupu alafu ya ukweli huwa sikuzote unajitegemea wenyewe

Tafadhali Sana ebu acheni kujazana UJINGA kwenye ishu kama hizi , siku ambayo mtajifanya mnataka kujibu mapigo zitakuja CNN, ABC news,sky news na wengine na documentary zingine ngumu Sana
 
Nowadays , ukweliii unekuwa upotoshajiii, hongereniiii, ukitumia tu ubongo vzr ili kubaini hali halisi, unaambiwa ni upotoshaji, ila wao wakidanganya hutosikia hawa akina Pascal Mayalla wakisema ni upotoshaji wanakaaa kimya, ila wengine wakiongea ndo mnajitokeza na kusema ni upotishaji, anyway kikubwa mkono uende kinywani no matter what.
 
Mjomba fanya uende pale Michenga. Ukikuta chupa za togwa barabarani, kunywa tani yako. Nitakuja kulipa. Umemjibu shemeji yangu kwa hoja nzito.

Ngoja tumsubiri kama atajitutumua kuja kujibu, au ataingia mitini. Kwa maana ni kitambo tu sasa amegeuka kuwa Ndumilakuwili. Na jambo hili nililigundua mapema sana.
 
Tatizo kajikanyaga hata kwenye habari yake soma vuziri. Ukiwa muongo lazima ukumbuke ulichokisema jana ama sivyo utaaibika
 


Kaka wamechukua tena kadi yao ya press?

Huu mwandiko sio wako kabisa
 
Kaka wamechukua tena kadi yao ya press?

Huu mwandiko sio wako kabisa
Mkuu hp4510, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, kwani mwandiko huu wa sasa wa Pascal Mayalla haufanani kabisa na yule mwanahabari nguli na makini tuliyemzoea. Inashangaza na kusikitisha sana kuona mtu anayejua fika ukweli wa vifo na ukandamizaji uliotokea Oktoba 29 leo hii anageuka na kuipongeza serikali kwa kuishambulia BBC inayofichua ukatili huo. Huyu ndiye Mayalla aliyewahi kulizungumzia hili huko nyuma, lakini sasa amekuwa mstari wa mbele kutetea propaganda zinazofunika damu ya Watanzania waliopoteza maisha. Kubadilika huku kwa ghafla kunathibitisha kabisa hoja yako kuwa aidha kalamu yake imenunuliwa, au kadi yake ya 'press' sasa hivi inatumikia maslahi na matumbo ya watu wengine badala ya ukweli na wananchi.
 
Wakili Madeleka na Pascal Mayala ili kuwaelewa unahitaji usiwe na hasira wala mawazo

Na mimi ndio nilichoona wengi hawajamuelewa unatakiwa akili iwe inacharge sana kuelewa hili bandiko na referrences zake.
Mkuu Dr. Mariposa (na Mchalinze): Kufananisha uandishi wa Wakili Madeleka na huu utumbo alioandika Pascal Mayalla kuhusu BBC ni makosa makubwa ya kiuchambuzi. Madeleka anajulikana wazi kuwa anatumia mbinu ya kejeli fumbo (sarcasm) kuumbua mamlaka, na ukiusoma mwandiko wake unajua kabisa upande anaosimamia ni wa kutetea haki za wananchi. Lakini kwa Mayalla hali ni tofauti kabisa; hapa hakuna fumbo wala akili kubwa inayohitajika "kuchaji"—makala yake iko wazi kabisa ikipongeza serikali kwa kutishia chombo cha habari kinachochunguza vifo vya raia wa Oktoba 29. Usijaribu kumtetea kwa nguvu Mayalla kwa kufunika propaganda zake nyuma ya kivuli cha "falsafa ngumu", kwani ameachana rasmi na weledi na sasa anatumia kalamu yake kuhalalisha ukandamizaji wa ukweli unaoonekana kwa macho.
 
Tuwapongeze serikali kwa kukataa kuhojiwa na kisha kuja kulalamika kwa wananchi kuwa hawakupewa nafasi kujieleza......
Pia tuwalaani BBC kwa kusema ukweli bila kuruhusiwa na serikali tukufu.
 

Nakubaliana na ww 💯,
 
Ni aibu Tanzania kusimangwa na Uingereza, Tanganyika ililelewa na Uingereza, haikuwa koloni la Uingereza na tuliishi na Waingereza kama ndugu, wale waliosoma Tabora School miaka ya 50' hata baada ya Uhuru waliweza kumualika Headmaster wao aje kutembelea Tanzania, alikuja. Gavana wa mwisho wa Tanganyika alikuja Tanganyika kwa mwaliko wa Ml. Nyerere, alikuja. Leo tuna viongozi wasioujua ukaribu wa Tanganyika na Uingereza wakidhani Tanganyika ilikuwa koloni la Uingereza hivyo wanajaribu kuionesha ubabe! Wamekosea, Uingereza iliilea Tanganyika kwa kukabidhiwa na League of Nations baadae United Nations kwa makubaliano maalum, hatustahili kuzozana na nchi ambayo haikututawala, Kenya ndio wangefanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…