Pongezi Serikali Yetu Kutonyamazia Upotoshaji wa Media za Mabeberu Kutubagaza, Let's Be Proactive Rather Than Reactive, Tuwaambie Ukweli Wote!.

Watoto wako watasikitika sana siku wakija kusoma hizi post zako.

Jitahidi kuwahurumia mkuu
 
SASA SI NA NYIE WASHAWISHINI TBC (UKWELI NA UHAKIKA) WATENGENEZE YA KWAO? MBONA MNATUKERA KWA KUWABAGAZA BBC, KOSA LAO NI NINI? MNATUKERA WASHABIKI WA BBC NA CNN NA ALJAZIRA MJUE ,KHAAA
 
Mkuu makala zako ni nzuri ila naona kama unajisahau unafikiri kila mtu kasoma Ilboru kama wewe.

Jitahidi kuandika makala straight.

Watu wajuwe msimamo wako sio kuuma uma na kupuliza.
 
P. Umegeuka tembo anayejificha kwenye ukoka but ccm wachache wenye macho ya ubongo wanakuona na kukulebo kama huyu siyo mwenzetu na ndio maana husongi mbele!
Badili aina yako ya uandishi na uonyeshe rangi yako halisi. Epuka ile dhana ya ku- hit around the bush ili uweke heshima.
 
Andiko refuuu lakini pumba tupu. Kwa hiyo ukweli kuwa Lissu alipigwa risasi na anateswa na CCM utafutika?
 
Binafsi sijawahi kuielewa tafsiri na maana yako ya neno "Uzalendo" ni ipi hasa..

Nevertheless, nimeingalia hiyo documentary yote juu ya historia ya unyanyasaji na ukatili aliotendewa Tundu Lissu na tawala zote za serikali ya CCM kuanzia kwa Mkapa mpaka sasa chini ya Samia Suluhu Hassan mwanzo mwisho kwa matoleo yote mawili yaani lile la Kiingereza na ile iliyotafsiriwa kwa Kiswahili..

Sijaona upotoshaji wowote. Sijaona lililo la uongo hata moja...

Kwa ufupi ni kuwa, yote ambayo yamekuwa documented kwenye documentary hiyo yote ni kweli tupu na ushahidi ukiambatanishwa...

Kumbuka documentary hii inamhusu Tundu Lissu na mapito ya maisha yake kisiasa. Sio ya kazi na shughuli za Serikali...

Serikali inaingizwa kwa namna inavyomtendea si kwa sbb ni mkosaji au mvunja sheria za nchi bali kama mtu aliyekataa ku - compromise na "status quo". Hilo ndilo linalowaudhi hawa watu wabaya wa serikali hii. Hawataki kusemwa vibaya wakati ni wabaya...!!

Mfano;

✓ Je, ni uongo kwamba Tundu Lissu amekamatwa mara nyingi kuanzia kwa Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia na kushitakiwa kwa kesi za uchochezi na mara zote serikali ikishindwa kwa kukosa ushahidi wa kumtia hatiani...?

✓ Je, ni uongo kuwa Tundu Lissu alipigwa risasi na watu ambao ushahidi wa wazi wa kimazingira unaonesha kuwa walikuwa wakitekeleza agizo la mtu mkubwa mwenye mamlaka makubwa ndani ya serikali ya ku - dictate nini kifanywe na kipi kisifanywe na vyombo vyenye mamlaka ya kuchunguza jinai..?

✓ Je, kwani ni uongo kuwa mpaka sasa hakuna uchunguzi wowote wa kipolisi uliofanyika dhidi ya jaribio lile la mauaji la mtu huyu licha ya kwamba lilifanyika mchana kweupe wa saa sana, katikati ya mji mkubwa wa Dodoma, kwenye majengo ya serikali maalumu kwa viongozi wa hadhi ya juu na yanayolindwa masaa 24 na Polisi wenye silaha pamoja na kufungwa camera za ulinzi (CCTV)? Unadhani kwanini kimya badala unaona majigambo ya uongo na ulaghai mtupu ya viongozi wa serikali dhidi ya haki za watu? Huo ndio Uzalendo..?

✓ Je, sio kweli kuwa na sasa Samia Suluhu Hassan na serikali yake amemfungulia Tundu Lissu mashitaka ya uongo Ili kujaribu kummaliza kwa kumuua?

✓ Je, sio kweli kuwa Samia Suluhu Hassan na CCM yake wanaitumia mahakama kama egemeo tu ili kufanya ushenzi wao dhidi ya mtu huyu. Ndio maana yeyote anayeharibu kuiongelea na kukosoa mwenendo wa hovyo, usio haki wa kesi hii, hayawani hawa utawaona wanasema "oh Rais hana mamlaka ya kuingilia mahakama, tunafuata utawala wa sheria, jambo hilo liko mahakamani, tuiachie mahakama itende wajibu wake". Lakini huo ni unafiki tu, reality ni kuwa mahakama yote imeshikwa "makende" na huyohuyo Samia na yeye ndiye anaye dictate nini kifanyike huko mahakamani. Kesi ya Tundu Lissu ni ya Samia, mahakama haitafanya lolote bila maelekezo yake..!!

#Kwa hiyo: Hakuna cha uongo ktk documentary hii. Yote ni kweli.

Aidha ktk documentary hii, Serikali walifikiwa Ili watoe maoni yao ktk masuala kadhaa yaliyo ktk documentary hiyo, walikataa na nunukuu ya BBC inasema:

".. BBC ilituma maombi kadhaa kwa serikali Ili itoe maoni yake ktk masuala kadhaa inayoihusu yaliyo ktk makala (documentary) hii. Serikali ilituomba tufanye mahojiano ya pamoja kwa wakati mmoja na Waziri wa Mambo ya ndani, Spika wa Bunge na Waziri wa nchi...

BBC tulikataa kuwahoji wote watatu pamoja kwa wakati mmoja kwa sababu jambo hilo kihanari lisingewezekana. Mwisho, hata baada kufanya juhudi zote, serikali ilikataa kabisa kutoa maoni yake..."

BBC wanaendelea kusema kwamba Serikali ya Tanzania hapo kabla mwezi Januari, 2026 iliiambia BBC kuwa, nanukuu;

"....Rais Samia alimkaribisha Tundu Lissu ambaye alikuwa uhamishoni kurejea Tanzania na kuendelea na shughuli zake za kisiasa. Hata hivyo, hakuna aliye juu ya sheria. Kesi ya Tundu Lissu haiwezi kujadiliwa kwa kuwa suala hili liko mahakamani..."

KWA HIYO: Serikali hii chini ya Samia Suluhu Hassan ndiyo ya waongo. Kila kitu kilicho kinyume chao, Ili kujiosha basi hujitetea kwa kusema uongo na ulaghai wakimfanya kila mtu mjinga na mpumbavu kama walivyo wao. Wananchi wameshawajua. Jumuiya za kimataifa wamewashawatambua kuwa hii ni serikali ya kijinga. Sasa watavuna walichopanda. Mwisho u karibu. Hawataweza kuwa kama Yoeri Kaguta Museveni wa Uganda ambaye ndiye anawafundisha ujinga na upumbavu. What is working in Uganda, can't work in Tanganyika kwa sbb hawa ni watu wawili tofauti, waliowekwa kwa makusudi tofauti...!
 
Kutonyamazia na kusema ukweli ni vitu viwili tofauti kabisa, kwa generation ya leo tunajua nani mpotoshaji huna haja ya kuandika mabandiko mareefu kutetea tumbo kwanza hamna msomaji wa riwaya za hivi siku hizi! Tweets tu na texts ndo dunia ya kisasa inasoma, tupo bize sana na kila kona kuna habari mpya msituchoshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…