Huu ndio ukweli unatakiwa kusema na kanisa. Mungu awabariki waliowezesha kutamkwa hadharan kwa ukweli huu.
Neno lake linatosha kuliponya kanisa na kizazi hiki na kuondoa uvumi uliokuwepo kuwa kanisa liko nyuma juu ya ushetani ule kwa mgongo wa haki za binadamu.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE
Tangu mwanzo Papa hakuwahi kuunga mkono eti ndoa za jinsia moja. Alisema wazi kuwa ni dhambi. Akafafanua kuwa hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kubariki dhambi.
Alichokuwa amekemea, na ambacjo watu wengine wakageuza na kusema kuwa eti Papa amebariki ndoa za jinsia moja, ni pale alipozuia kuwatenga hawa watu. Alisema wazi kuwa pamoja na hayo matendo yao yasiyokubalika, bado ni wanadamu, Mungu anawapenda kama viumbe vyake, Kanisa liwapokee kwa nia ya kuwapa mafundisho ya kuwabadilisha. Alikemea tabia ya kuweka sheria kali dhidi yao maana kuna baadhi ya mataifa, hao watu, adhabu yao ni kifo. Hicho ndicho alichokipinga.
Kusaini waraka maalum wa kichungaji unaotamka wazi jambo hili haliruhusiwi na kupata baraka za Kanisa, ni kuweka msisitizo, na kuzuia kabisa wale waliotaka kutumia kauli yake kama njia ya kuruhusu mambo hayo kukubalika ndani ya KANISA.
Hata kama Serikali zote za Dunia, zikasema jambo hilo ni halali, Kanisa ni lazima lisimame katika mafundisho yake. Ikifika hapo, Kanisa linene kwa kauli iliyo thabiti, kama alivyonena Joshua:
Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.