Poromoko la bei la Gari aina ya Nissan Dualis

Nissan hazina tatizo zaidi ya gharama. Ni gari za gharama kuzitunza hilo ndo tatizo lake. Na watanzania wengi wanataka watreat nissan kama toyota rav 4 old model lazima ikusumbue.

NISSAN NI GHARAMA KUMILIKI HILO NDILO TATIZO HAKUNA TATIZO LINGINE.
 
Hahahah kigari cha Nissan kinataka hela tu. Ukiwa uko njema bank hakitakusumbua, service kwa wakati tu.
Kabisa boss. Unanunua bei chini gari ila Kinataka kikiua gearbox ununue gearbox kwa bei pungufu kidogo ya bei ya gari.
 
Gari 6M gearbox 2.5M patamu hapo.
Kabisa. Hapo 2.5m umenunua Tandale iliyovuliwa kwenye gari nyingine.

Ukiagiza +V.A.T inakimbilia 3.5m ukimlipa na fundi juma inafika 4m hapo bado fundi juma hajakosea kukuungia nyaya zikapiga shoti control box ikafa inayouzwa dola 250 dubai.

KAMA HUNA PESA ZA KUITUNZA NISSAN NUNUA TOYOTA RAV 4 3S 1998 UTAKUJA KUNISHUKURU.
 
Wale majamaa wanapiga hela sana. Aisee mie nina engine ya nissan bluebird sylphy QG18DE na gearbox yake ya N16 nimeivua kwenye gari ya ndugu yangu iliungua moto upande wa nyuma. Ni jino moja tu inawaka. Inafunga kwenye Wingroad, Sunny, Primera na Sentra.

Naitaftia mteja kama una contact za jamaa yeyote ambaye atakuwa interested nimuuzie hata kwa bei pungufu maana Ilala inauzwa laki 9 na gearbox yake ni laki 5!
 
KAMA PESA ZA KUITUNZA NISSAN HUNA, NIKIMAANISHA OIL YAKE YA GEARBOX LITA MOJA NADHANI 40,000 YA ENGINE 65,000 KAMA HUNA PESA ZA KUNUNUA SENSOR ORIGINAL, KAMA FUNDI WAKO NI FUNDI ANATEMBEA NA TESTA, KAMA UNANUNUA GARI HUKU UKIWAZA KULIUZA MBELENI ACHANA NA NISSAN.

NUNUA TOYOTA TENA TOYOTA RAV 4 3S 1998. UTAKUWA UPO KAMA KWENYE SUFURIA ILA UTAFURAHIA MAISHA. HAZINA GHARAMA, ZINADUMU NA ZINAUZIKA HARAKA.
 
Nimescreen short hii ntakujulisha.
 
Hahaa mkuu hapo utakuwa upo kwenye sufuria unamaanisha nini?
 
Nissan Dualis ni CVT ukiweka ATF lazima Gear Box ife
Na hapa ndio wengi wanachemka. Nilimchana ndugu yangu juzi kwenye gari yake Rumion, nikamwambia utauwa gari hiyo. Hiyo oil sio yake.....

Yeye kakazana lakini si ni Total hii, nikamwambia shida sio kampuni ni aina ya oil. Nikamwambia atafute oil yake.....
 
Hii comment itumike kama sehemu ya viambatanishi vya joining instruction pale kwenye chuo cha udereva na ufundi Veta na NIT na kwingineko....
 
Kimsingi hizo gari zina matatizo kadhaa, mosi ukikosea kuweka Oil yake inakula kwako na ukijitusu uweke transmission oil ambayo sio NS2 umeua gearbox kabisaaaa, ila kwa kuwa comfortable iko poa sana na kingine ni kwenye spea kama umezoea toyota ukiingia mule ni kama cha kike ni bora uendelee na Toyota tu. Ukitaka isikuzingue Oil tumia za kwake injini na gearbox pia service fanya kwa wataalam wa hizo gari sio vijiweni, tatu usiwe mbahili spea zake nyingi OG hivyo na bei imechangamka pia
 
Mshazoea Toyota, endeleeni nazo, sio kuleta unafiki kwa nisaan, namiliki nisaani Mwaka wa 5 huu, na wala haina kwere.
Unapeleka Nissan kwa fundi gonga, karithi ufundi Toka kwa mjomba wake. Unategemea nini!?
si unajua watu na ile mentality ya sizitaki mbichi hizi. kumbe hana uwezo wa kumiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…