Poromoko la bei la Gari aina ya Nissan Dualis

Poromoko la bei la Gari aina ya Nissan Dualis

Naaaam! Tatizo wabongo hawawezi kukiri kama gari aliyonunua inamtesa hadi atakapoiuza... Utasikia tu ukitunza itadumu sasa kutunza gari sio kama kunywa orojo! Kila mbongo gari yake hainywi mafuta, kila mbongo gari yake haimsumbui [emoji23][emoji23]
Ukweli ni kwamba hakuna gari lisilosumbua hapa Tanzania....mazingira ya barabara mbovu, vipuri feki, elimu duni, mafundi wasio na ujuzi, uchumi mbovu wa mtu binafsi....hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya kila gari lisumbue...[emoji38]

Hii hoja watu wanayoisemea"ukiitunza vizuri itadumu.."Ni sahihi kabisa....

Barabarani kwa sasa zaidi ya 75% ya magari yametengenezwa mwaka 2005 kwenda mbele.....

Ni gari gani la mwaka 2005 kuja mpaka miaka hii ya leo lisilohiyaji matunzo mazuri..??????

Mnataka kutuaminisha kuwa IST isipotunzwa itadumu, passo isipotunzwa itadumu, Clugger isipotunzwa itadumu, Tako la nyani, crown zisipotunzwa zitadumu eti kisa ni Toyota..?????

haya mambo ni mepesi sana kuyaelewa, tatizo watu wengi wanaongea kuhusu magari kwa akili za ushabiki wa Simba na yanga, Chadma na ccm..[emoji6][emoji38][emoji38][emoji38]

Nakazia Tena, Hakuna gari lililoundwa kuanzia mwaka 2005 na kuendelea lisilohitaji kutunzwa vizuri...

Ukiangalia magari mengi ya miaka hii iwe ni Nissa, Toyota,subaru, Bmw,VW ni mabati laini, alluminium, interior ni plastic bag kwa asilimia kubwa, umeme mwingi, sensors kibao...

Umewahi kujiuliza ni kwa nini wamiliki wa Toyota ndiyo wanaongoza kwa kutafuta gear box na engine used...?[emoji38][emoji38]Kwa sababu ya ile tabia ya mazoea eti Toyota hazichagui oil, ATF zinawekwa za bei rahisi rahisi tu kwa sababu wanajifariji Service ya Toyota ni bei rahisi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu ila hata hao wenye uwezo wa kumiliki wanawake namba 1 kuna muda wanalia lia maana maisha nayo hayo constant muda wote... Nilikuwa nasoma reviews za audi A4 hata wazungu ambao tunawaona hawana shida wanalia nayo na hasa gharama za matengezo ta engine maana ndio tatizo kubwa
Mkuu nakubaliana na wewe...
Magari ya Ulaya yanaongoza kwa kuletea watu vichomi..

Ila mtu mwenye kipato chake cha kati au kikubwa, hawezi kulalamika kuwa gari za Japani ni kichomi..[emoji38][emoji38]

Sasa ukisikia mtu analalamika Nissan ni kichomi, huyo amelazimisha maisha ya kuwa na gari..[emoji3]Muda wake ulikuwa bado..

Huyu atafute tu Starlet au Vitz old model au Carina Ti zote namba A au B ambazo atauziwa M 2 au 3 ili ajifunze kuzoea gari....akishazoea ndiyo aje atafute gari..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumiliki Nissan ni kama kumiliki demu Masaki [emoji23]!!! Mizinga ni malaki mpaka mamilioni on the spot.
Ila kwa sie wa Toyota ni kama kumiliki demu Tabata tu..Spoku ni za elfu 20 mpaka laki! Zikizidi hapo ni mara chache mno.
Nissan watu wanatishana tu, spea za bei rahisi siku hizi zipo japo si nyingi kama toyota..na nimefunga mara kadhaa bei kama zile zile za toyota

Kero kubwa ya Nissan kwa sasa ni haziuziki kwa bei nzuri kama toyota...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss wangu alikuwa nayo, Hii Dualis. Bodaboda akaparamia side mirror. Acha wee, aliipata kwa 300k.
Akaiuza, alieuziwa akaua GB kwa kusahau kufuata mashart ya service

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
Side mirror hela ya kawaida ni arround 250K - 400K.

Tena hizo ni Toyota. Kwa duallis kuwa na hiyo bei mbona mnashangaa??
 
Pajero ni aina ya ndege huko S. America
Na ni mtaalam wa puli kwa wahispania.
Screenshot_2020-11-06-07-05-58-1-1.jpg
Screenshot_2020-11-06-07-06-07-1.jpg
 
Kweli kumiliki gari ndogo sio mchezo wakati daladala Side mirror ni elfu 12
Side mirror hela ya kawaida ni arround 250K - 400K.

Tena hizo ni Toyota. Kwa duallis kuwa na hiyo bei mbona mnashangaa??
 
Sasa na msimu huu wa mvua madimbwi kibao mimaji inajaa barabarani ndio uburuze Nissan Nyanya yako imagine lile li njia la mnazi mmoja linalonyoosha hadi mfugale kunajaaga mimaji pale mbele. Lazma utubu tu 😂😂😂

Juzi nimeburuza Toyota langu mle hadi nikalionea huruma japo halijakorofisha. Maji yalikuwa usawa wa bonet nikawaza je mtu wa Nissan, Benz, Bmw au Audi atatoboa kweli bila dashboard kumeremeta 😂😂😂
Kila mtu ananunua Gari kwa mahitaji yake mwenyewe (wengine wanatafuta luxury nyie kwa ajili ya kubebea simenti/tofali) so usipangie watu wote wanunue Toyota wakati wao wanataka Luxury.
 
Back
Top Bottom