Naaaam! Tatizo wabongo hawawezi kukiri kama gari aliyonunua inamtesa hadi atakapoiuza... Utasikia tu ukitunza itadumu sasa kutunza gari sio kama kunywa orojo! Kila mbongo gari yake hainywi mafuta, kila mbongo gari yake haimsumbui [emoji23][emoji23]
Ukweli ni kwamba hakuna gari lisilosumbua hapa Tanzania....mazingira ya barabara mbovu, vipuri feki, elimu duni, mafundi wasio na ujuzi, uchumi mbovu wa mtu binafsi....hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya kila gari lisumbue...[emoji38]
Hii hoja watu wanayoisemea"ukiitunza vizuri itadumu.."Ni sahihi kabisa....
Barabarani kwa sasa zaidi ya 75% ya magari yametengenezwa mwaka 2005 kwenda mbele.....
Ni gari gani la mwaka 2005 kuja mpaka miaka hii ya leo lisilohiyaji matunzo mazuri..??????
Mnataka kutuaminisha kuwa IST isipotunzwa itadumu, passo isipotunzwa itadumu, Clugger isipotunzwa itadumu, Tako la nyani, crown zisipotunzwa zitadumu eti kisa ni Toyota..?????
haya mambo ni mepesi sana kuyaelewa, tatizo watu wengi wanaongea kuhusu magari kwa akili za ushabiki wa Simba na yanga, Chadma na ccm..[emoji6][emoji38][emoji38][emoji38]
Nakazia Tena, Hakuna gari lililoundwa kuanzia mwaka 2005 na kuendelea lisilohitaji kutunzwa vizuri...
Ukiangalia magari mengi ya miaka hii iwe ni Nissa, Toyota,subaru, Bmw,VW ni mabati laini, alluminium, interior ni plastic bag kwa asilimia kubwa, umeme mwingi, sensors kibao...
Umewahi kujiuliza ni kwa nini wamiliki wa Toyota ndiyo wanaongoza kwa kutafuta gear box na engine used...?[emoji38][emoji38]Kwa sababu ya ile tabia ya mazoea eti Toyota hazichagui oil, ATF zinawekwa za bei rahisi rahisi tu kwa sababu wanajifariji Service ya Toyota ni bei rahisi...
Sent using
Jamii Forums mobile app