Kutoka kwa mdau.
-Nimetoka kwenye mkutano wa Dr Edward Hoseah ambao umemalizika muda mchache uliopita katika ofisi za makao makuu ya TAKUKURU Upanga jijini Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo, kwanza Dr Hoseah kaanza kwa kusema "Sijiuzulu ng'o, maana toka asubuhi ninapokea simu za watu wakiuliza kama nimejiuzulu tayari" hayo yalikuwa maneno yake wakati anaingia ukumbi wa mikutano kabla hata ya kusamiliana na wanahabari.
Dr Hoseah anasema "kuna nini mpaka wabunge waogope kuchunguzwa na TAKUKURU? kinachomshangaza ni kuwa hata sheria inayotekelezwa na TAKUKURU imepitishwa na bunge lenyewe tena na wabunge hao hao, iweje leo waanze kulalamika kuwa hawatendewi haki? haki wanayoitaka waheshimiwa wabunge ni ipi?" anahoji Hoseah.
Aidha anasema , barua ya bunge ya tarehe 26/02/2009 iliyokuwa imeelekezwa kwake, ilikitaka chombo chake kufanya uchunguzi ili kujiridhisha maana kulikuwa na minong'ono ya wabunge kulipwa posho mbili, huku wanalipwa na bunge pamoja na taasisi wanayokwenda kuitembelea!
Amewataka wabumge ambao wamekuwa na sifa kubwa ya kupinga vitendo vya kifisadi watoe ushirikiano ili chombo hicho kiweze kuwafanyia 'natural justice' maana katika detection tayari makachero wa TAKUKURU walishapata kila kitu kuhusu posho hizo mbili za wabunge.
Aidha amewataka wabunge ambao wanaona anafanya makosa kuwachinguza, wapige kura ya kutokuwa na imani naye, na yupo tayari kwa lolote litakalotokea, huku akijiganba kuwa TAKUKURU sio mwisho wa maisha yake hata kidogo, "there is life after PCCB" anasema Dr Hoseah-