Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Kupokea posho mara mbili mbili kunadumaza Taifa. Kwanini wasipige kelele? Ni kuogopa kuitwa wapinzani uchwara? Mbona hilo wameshaitwa saaana. Kwanza wao ni wabunge, na issue inahusu wabunge. Kama wabunge wa upinzani lazima wataulizwa na waandishi wa habari ni nini msimamo wao. Wakikaa kimya watapakaziwa wanalindana. Halafu hivi kutafuta mawakala si jukumu la mgombea? Sidhani kama ni busara kumhusisha Katibu Mkuu au Naibu wake. Watafanya mangapi? Hilo ni suala la kurugenzi ya Uchaguzi.

Mimi binafsi wabaya wangu wakigombana nitashabikia ili wauwane wasije hata kuafikiana baadaye. Kama ikishindikana nitachochea mpaka watoane macho hata wakija patana wana makovu ya kudumu. Hapo nitajihesabu nimeshinda.

.

"Tatizo hapa ni kutoelewana, mimi nadhani washughulikie Richmond kwanza alafu mambo ya kupokea posho mara 2 au mara 3 yatakuja baadae, kwani suala la posho mara 2 mbona magereza itajaa."
 
Posho yenyewe utakuta ni tshs 40,000, ndo inakomaliiiiwa, while kuna miradi ya million150 kwa siku watu wamekauka!
Aliyosema Pinda kwamba mafisadi si watu wa mchezo ni kweli~!
 
Naona Zito na Dr. Slaa mmesahau ule usemi unaosema, “ukiona ndugu wanagombana, chukua jembe kalime. Wakipatana wewe kavune”. Najua mnajua wazi kuwa wanaopokea posho mara mbili serikalini ni wengi mno ila hili la wabunge limekuja tu kwa sababu watu wengine hawatakiwi humo ndani ya CCM. Mnajua wazi kuwa hili limeibuka tu kwa sababu kundi moja la wanaCCM limeona wenzao wanifaidi serikali ya CCM hivyo wakaamua kuitana mafisadi (japo wote ni mafisadi). Kumbuka Uchunguzi uligundua kuwa Mbunge Chitalilo aligushi vyeti ila serikali ikasema haina interest ya kumpeleka mahakamani. Hamuoni kuwa huu uchunguzi wa TAKUKURUni kiini macho ili kuwanyamazisha vidomodomo ndani ya CCM. Siku Chitalilo akinyanyua tu mdomo utasikia anapelekwa mahakamani. Hivyo ninaamini kuwa sakata la Richmond likipoa, hutakaa usikie lolote kuhusu posho mara mbili na TAKUKURU hiyo hiyo itasema hakukuwa na kosa la kijinai ila ni ukiukwaji mdogo tu wa taratibu za fedha. Na hapo CCM wakipatana usijeshangaa Zito na Dr Slaa wakageuziwa kibao wakaitwa wachonganishi, wapinzani uchwara na/au wachochezi.
Mh. Dr. Slaa na Zito Kabwe, Huku mikoani CHADEMA tunaipenda sana, acheni kuingilia mambo mnayojua kuwa ni kiinimacho. Njooni huku tuandae vijana wa kusimamia kura (mawakala wa uchaguzi mapema). Msikubali kuingilia mambo ambayo unajua kuwa serikali tulo nayo haina utashi wa kisisa wa kushughulikia hili suala la posho mara mbili japo ni wazi kuwa kisheria ni kosa. Kwa wale wasiojua makosa ya Rushwa kuna kosa moja linaitwa “Obtaining advantage without lawful consideration”. Hivyo TAKUKURU wanao uwezo wa kuchunguza na kuwafungulia mashtaka hao walochukua posho mara mbili ila ikitokea issue ya Richmond ikipita bila matatizo ..................
.

Tatizo lako wewe mh.ni ushabiki kwa mwakyembe na sio maslahi ya taifa.Mwakyembe leo akisema tukojoe barbaran,nafiki uko tayari ku support.Ujinga gan huo bwana wewe?
 
Posho yenyewe utakuta ni tshs 40,000, ndo inakomaliiiiwa, while kuna miradi ya million150 kwa siku watu wamekauka!
Aliyosema Pinda kwamba mafisadi si watu wa mchezo ni kweli~!

TSh 40,000 x wabunge 322 x siku 100 za kupokea posho Jibu lake ngapi? Hapa nimefanya 'hypothetical calculation' usije ukaniuliza kwani wabunge wote wanapokea posho kwa siku nilizotaja! Ninachotaka kukuonyesha ni kwamba posho zinazopokelewa na wabunge ni kubwa ukizingatia wingi wao na frequency ya kuchukua hizo posho! Hesabu yake ni zaidi ya milioni 200 kama huna habari! Mchezo huu unasemekana umezoeleka mno mpaka baadhi ya Kamati za Bunge huandika barua in advance ili waandaliwe 'takrima' ya posho, tena kwa kutaja kiasi, pindi wanapoenda kushughulikia jambo fulani! Hii imeshakuwa sio African/traditional hospitality kama Spika Sita anavyotaka tuamini!
 
Nakuambeni nyie wapinga ufisadi nji hii kazi ipo! unafikiri maaduni watakuwa mafisadi kumbe la, majirani zenu wenyewe
 
"Tatizo hapa ni kutoelewana, mimi nadhani washughulikie Richmond kwanza alafu mambo ya kupokea posho mara 2 au mara 3 yatakuja baadae, kwani suala la posho mara 2 mbona magereza itajaa."

Kama kungekuwa na sheria ya kuwavua watu uraia, saa hizi tuko kwenye process ya kuwavua mafisadi ndani na nje ya CCM warudi walikotoka babu zao. Tungefilisi mali, nyanganya passport na kuwaambia waanze, Lowasa tungemtolea mpaka wa Kenya aelekee Ethiopia, Mkapa tungemtolea kusini atafute alikotoka babu yake, Rostam Azizi tungempandisha Air India arudi kwao.
 
TSh 40,000 x wabunge 322 x siku 100

Ukiongeza na mshahara wa 7,000,000 x 322 x 12 = hawa jamaa hawatupi value for money kikazi.

Halafu wanalilia mishahara iongozwe na nchi yetu ni maskini. Mi hata siwaelewi wanao watetea hii mijitu milafi tu. Yaani hata sijui ni percent gani ya bajeti inaishia kwenye matumbo ya hawa watu.

Huyu Mwakyembe si mtu mzuri inavyo onekana anajua madudu yake na anajua kama jamaa watamlamba kwa unafiki wake kujifanya mpiganaji kumbe ni fisadi tu. Hana lolote anajifanya ataki kuhojiwa ili akamatwe alafu apewe public sympathy ni sungura mjanja huyu. Kumbe na yeye tunasikia alikua anagombania tender za umeme huko singida. Nadhani Richmond ni personal vendetta tu kwake wacha wam-malize tu fisadi mwingine. The less we have them the better.
 
Kasyabone,

Homeboy wako wa Rungwe yaani Mwakyembe kwa kweli ana hali mbaya.

Tulisema hapa mapema kuwa tunagahamu mengi juu yake, mkaja hapa na kupiga vigelegele vya Kinyakyusa. Sasa yanaanza kutimia. Ningelikuwa Mwakyembe ningelisema "mwakani singombei tena....." Walau wangelimpa kupumzika. Tatizo yeye alijifanya Mpalestina sana kwa kurusha Mawe na wakati huo kumbe mwenyewe anaishi nyumba ya kioo.
 
Zitto, mimi naona umekuwa mkweli hata kama na wewe uliwahi kupokea, huwezi kujustify kosa la double allowance. Endelea kuwakaba hivyo hivyo mpaka waone aibu, si wanajifanya wao ni wasafi bwana, tuone huo usafi wao. Wakishapokea allowances zao mara mbili mbili wankimbilia jimboni kutoa msaada wa bati moja kwa shule then wanajifanya kutekeleza ilani ya chanma cha mapinduzi!
No! we cannot be fooled always acha waumbuke.
 
Kupokea posho mara mbili mbili kunadumaza Taifa. Kwanini wasipige kelele? Ni kuogopa kuitwa wapinzani uchwara? Mbona hilo wameshaitwa saaana. Kwanza wao ni wabunge, na issue inahusu wabunge. Kama wabunge wa upinzani lazima wataulizwa na waandishi wa habari ni nini msimamo wao. Wakikaa kimya watapakaziwa wanalindana. Halafu hivi kutafuta mawakala si jukumu la mgombea? Sidhani kama ni busara kumhusisha Katibu Mkuu au Naibu wake. Watafanya mangapi? Hilo ni suala la kurugenzi ya Uchaguzi.

Mimi binafsi wabaya wangu wakigombana nitashabikia ili wauwane wasije hata kuafikiana baadaye. Kama ikishindikana nitachochea mpaka watoane macho hata wakija patana wana makovu ya kudumu. Hapo nitajihesabu nimeshinda.

.
Japo si mwanasheria lakini nadhaNi hawachukuwi posho mara mbili.Kwa sababu hawalipwi mara mbili kwa kazi moja ya kuwakilisha wananchi na ofisi ya spika.Hizi za semina ni kazi zingine kabisa. si kazi zinazohusu wananchi wao.kama wizara wanatengewa pesa za semina ambazo zinawalipa hata waajiriwa wa umma ambao ni waandaaji wa semina kwa nini wabunge wasilipwe kama wajumbe.Ukiondoka ofisini kwako kwa kazi lazima ulipwe.Hata rais akienda marekani au kutembelea mikoa analipwa japo ndo kazi yake. posho mara mbili Ni MBINU ZA TAKUKURU, MAFISADI NA PINDA KUTAKA KUUA HOJA HALALI YA RICHMOND. please get out of this dirt path, Tanzanian already know their enemies; MAFISADI. HATUDANGANYIKI TENA. SANA SANA NI KULETEA CCM MATATIZO YA KUUZIKA.BORA MTOKE MADARAKANI.
 
Kasyabone,

Homeboy wako wa Rungwe yaani Mwakyembe kwa kweli ana hali mbaya.

Tulisema hapa mapema kuwa tunagahamu mengi juu yake, mkaja hapa na kupiga vigelegele vya Kinyakyusa. Sasa yanaanza kutimia. Ningelikuwa Mwakyembe ningelisema "mwakani singombei tena....." Walau wangelimpa kupumzika. Tatizo yeye alijifanya Mpalestina sana kwa kurusha Mawe na wakati huo kumbe mwenyewe anaishi nyumba ya kioo.
Mzee hapa naona na wewe unadandia maada na kushabikia. unayoyafahamu yapi? cha msingi hapa wewe huna lolote unalolifahamu. Waulize walioenda kujitangaza kuwa watagombea wanapoulizwa wameifanyia nini kyela wanakimbia. nitaeleza kwa kirefu kidogo siku za usoni kwani kuna mtu mwingine wanakalibia kumtuma akapime upepo kwake utaendaje. japo naye alikuwemo kwenye kinyanganyiro ambacho mwakyebe alikuwa kidedea. sasa ebu endeleeni na ushabiki halafu nitawatafuta siku za mbeleni kuwapa pole kwa kushindwa kwa jitihada zenu. mtu safi ni safi tu. hata yesu ni alikuwa nabii safi lakini walimpiga mawe, walimwita mwizi, muongo na mkuu wa mapepo kabla ya kujua ukweli wake.
 
Mimi nazidi kuwashangaa wale wote wanashabikia huu uchunguzi kwa sababu tu wanaoelekea kubanwa ni wabunge wa sisiemi. Hoja ya msingi ingekuwa kama kweli kupokea na kusaini posho ya dereva au ya kikao ni rushwa au vitu vya namna hii ni rushwa. Maana nilidhani Takukuru wanawajibika kuona vitendo vinavyoelekea kwenye rushwa ambavyo vinasababisha kupindishwa kwa maamuzi na kuleta madhara ya utawala mbovu(bad governance). Lakini pamoja na ukweli kwamba sipendi hata kumwona mtu anayekumbatia siasa za kisisiemi, sikubaliani na mkakati uliobuniwa kudhibiti posho mbili. Mbona ni rahisi mno kulikabili hili bila ya kutumia muda mwingi, raslimali watu na posho!! Unajua hata hao TAKUKURU watapewa maji, chai, sambusa na posho ya chakula cha mchana wakati wanahoji wabunge,.tena watapewa magari maalumu na posho ya kujikimu kama itabidi watoke Dar kwenda Dodoma....Acheni kumfilisi Mama Tanzania!!!

My take ni hivi; kwanza tabia ya posho imejikita sana kote kwenye maofisi ya serikali. Ukiwa CEO wa shirika la uma, unatakiwa uhudhurie vikao vyote vya Bodi, Kamati kibao. Pmoja na ukweli unapata mshahara mzuri, responsibility allowance, dereva, mlinzi, magari(MAGARI 2,3 AU Zaidi), kila kikao unalipwa posho. Mashirika maskini yanalipa Laki 3 tu lakini yale manono manono hadi milioni kwa kikao. Na wanasaini kupokea pesa hizo. Na hizi ni nje ya gharama za caterers, wale wanaoleta chai, chapati, kuku, sambusa, matunda, maji, soda nk.....

Sio hivyo tu, hata Muungwana na wenziwe wakitembelea vijiji hupewa takrima ya bei mbaya kwa bei za vijijini, wanaweza wakachinjiwa mbuzi, wanaweza wakapewa malazi bure,,,,yote haya....kama TAKUKURU wanataka kuhoji, wamhoji serikali, sio wale wanaonufaika, yaani serikali ndiyo imetaka kuwamotisha viongozi wake pamoja na wabunge ili wawe YES MEN!
 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dr Edward Hosea, kesho saa nne asubuhi anakutana na waandishi wa habari ofisni kwake
 
kunani tena au ndo mkutano wake aliotoka Rwanda?!!!!!!!!
 
Anaweza kuibuka na mpya, au ndio kuendeleza libeneke na watunga sheria ama kujisafisha? Lakini anaweza kuibua upya sakata la mafisadi papa ama kutekeleza amri za mafisadi kutafuta mchawi mwingine baada ya Mwakyembe?
 
Hakika mwaka huu tutaona mengi .Sasa yeye anakimbilia kwa hao jamaa tena ? Bahasha zao kesha andaa ili waandike vyema ama anawaita mkono mtupu wasipo andika na wao wamezoea bahasha atamlaumu nani ?
 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dr Edward Hosea, kesho saa nne asubuhi anakutana na waandishi wa habari ofisni kwake

Mhhh! Sijui ataongea nini huyu, labda kapewa talking points na Ikulu, vinginevyo akitaka kuonyesha ubavu wake dhidi ya Wabunge ambao ameshindwa kuuonyesha dhidi ya mafisadi basi hili sakata kati ya Wabunge na TAKUKURU linaweza kuzidi kuwa kubwa zaidi.
 
Nafikiri hosea, mwakyembe, sitta, sendeka tuwaita ma-celebrety siyo viongozi..lol..kazi kuuza habari bila tija..huu upuuzi mtupu..kila kitu politics
 
unajua sometimes mi napoteza uelewa hapa..kwani hawa wanaopokea posho mara mbili wanaitwaje?au sio mafisadi?na huyu wa kupeleka marisiti ya 2m kwa ajili ya kununua dawa pale namanga pharmacy anaitwaje?

Iam getting tired na hizi issues za mafisadi ni bora tujadili mambo mengine
 
Back
Top Bottom