Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Mkandara,
  1. Mkuu, ubadhirifu wa matumizi ni pale pesa inapotumika bila kuwa imeidhinishwa kisheria. Hizo posho zimesainiwa na Raisi mwenyewe na kupitishwa kwenye bajeti na hivyo sio RUSHWA. TAKUKURU hawana uwezo kisheria kuzichunguza.
  2. Kama wananchi hatuzipendi hizi posho, tunatakiwa kuingia mitaani kupambana na Kikwete kwa kuziidhinisha.
  3. Hili la TAKUKURU kuwachunguza wabunge ni mbinu tu ya kuwanyamazisha.

Sio lazima kuwa kila kinachopitishwa kisheria hakiwezi pia kuwa ni ubadhirifu. Kigezo cha ubadhirifu ni uhaki wa yaliyopitishwa. Jee hayo yaliyopitishwa kisheria yana harufu ya rushwa au kifisadi? Kama hayo yapo basi sheria hiyo si halali.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo, ungejua yaliyotokea Uingereza. Huko Wabunge walipitisha kisheria kabisa kuwa walipiwe kwa mambo yao binafsi kama vile kutengeneza bustani zao, kulipiwa mortgage ya nyumba zaidi ya moja, kununua vitu vya nyumbani etc na wakawa wakidai matumizi hayo kisheria kwa miaka mingi tu. Hivi juzi juzi tu wananchi wakachachamaa kuwa sheria hizo zilikuwa si za haki na ni zakifisadi. Wabunge waliofanya hivyo, wakalazimika kurudisha fedha hizo ingawa zilipitishwa kisheria na ikasababisha Spika wa Bunge kujiuzulu kwa kutetea ujinga kama huo.

Kwa mtu mwenye busara, kipimo hapa ni jee ni haki mtu mwenye heshima kama Mbunge kuiba fedha za umma kwa kujilipa mara mbili kwa kazi ile ile?

Hayo mengine yote ni justifications zisizokuwa na msingi.
 
Mpokeaji wa posho ndiye anajua amepokea wapi na wapi! Mtoaji atajuaje kama mpokeaji amepokea posho nyingine? Kwa mfano mtumishi akiitwa kwenye semina aliyemwita atamlipa posho. Endapo mtumishi amelipwa alikotoka hakuna haja ya kulipwa tena mara ya pili! Kumbuka serikali ni ile ile, kwa hiyo haiwezekani ikamlipa mtumishi yule yule kwa kazi moja!

Mtoaji naye anatoa kutoka fungu gani? Suala sio kutojua kuwa mpokeaji keshapata sehemu nyingine. By the way sioni kama hili ni suala la kushughulikiwa na TAKUKURU ila kwa Tanzania yote yanawezekana
 
  1. Kama malipo yote yamefuata sheria na taratibu za malipo, sasa rushwa inatokea wapi?
  2. Kwa hiyo mbadhirifu ni nani, anayelipa au anayelipwa kufanya kazi?
  3. Kama posho ni kubwa, hilo ni suala lingine lakini sio kazi ya TAKUKURU.

Unaposema malipo yamefuata taratibu una maana gani? Mtu kalipwa mara mbili kwa kazi ile ile moja wewe unadai ndio kufuata taratibu! Na unaposema sio kazi ya TAKUKURU unamaanisha nini? Unataka kutuambia anayetakiwa kutekeleza Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11/2007 ni nani? Ukweli ni ukweli tu, hata kama utasemwa na Shetani! Kulipwa posho zaidi ya moja kwenye kazi ile ile ni ubadhirifu wa fedha za umma na ni kinyume cha sheria! It is criminal, to say the least! Naona waheshimiwa hawa hawajaondoa notion ya takrima vichwani mwao! Wameitoa kwenye uchaguzi wameiingiza kwenye "double payment." Hapa dawa ni kurudisha Azimio la Arusha (Azimio la Utu) lililokuwa na Miiko ya Viongozi wa Umma! I think it will be a permanent solution!
 
Mpokeaji wa posho ndiye anajua amepokea wapi na wapi! Mtoaji atajuaje kama mpokeaji amepokea posho nyingine? Kwa mfano mtumishi akiitwa kwenye semina aliyemwita atamlipa posho. Endapo mtumishi amelipwa alikotoka hakuna haja ya kulipwa tena mara ya pili! Kumbuka serikali ni ile ile, kwa hiyo haiwezekani ikamlipa mtumishi yule yule kwa kazi moja!

Buchanan,
  1. Umejuaje kuwa mtoaji ndiye asiyejua kuwa mpokeaji tayari ana posho?
  2. Tokea lini TAKUKURU wakawa ndio wafuatiliaji wa malipo yanayofanywa kwa wabunge ambayo sio siri?
  3. Je huko serikalini hakuna wenye posho mara mbili za kufuatiliwa na TAKUKURU?
 
Nji hiii haina mwenyewe thats the problem, miongozo na mambo yanpelekwa kiubinafsi zaidi, head prefect yupo wapi? anatakiwa aingilie kati na kutoa maamuzi yeye ndo bosi hapa!! asipiganishe na kukaa pembeni na kuwatch!!
 
Nilimwona Spika wetu jana. Hajui kwamba mashirika ya UMMA hayamo kwenye bajeti kubwa ya serikali inayowasilishwa BUNGENI. TANESCO, DAWASA, NSSF,....yana bajeti zao ambazo kimsingi posho za kuwapa waheshimiwa hawa hazipo. Mimi sikutarajia Spika Sitta asiwatetee wabadhirifu wenzake hawa. Uchaguzi wa Spika ni mwakani tu na wengine amewajeruhi kwa namna moja au nyingine katika baadhi ya maamuzi yake yaliyopita. Wabunge wetu wa kamati mbalimbali chai wanapewa, lunch wanaandaliwa tena kwenye mahoteli makubwa tu lakini bado wanachukua bahasha nzitonzito.
Halafu huwa naona polisi wanawashtaki watu wanaowazuia kufanya kazi yao. TAKUKURU hawana kipengere hicho? Maana naona kuna juhudi za makusudi za kujaribu kuuzima uchunguzi huu ambao umelitafuna Taifa hili kwa muda mrefu sasa.
 
Kuna Mihimili mikuu mitatu ya Dola nayo ni

1: Serikali
2: Bunge
3: Mahakama

Mihimili hiyo mitatu ni Sawa kwa maana kila mmoja una Majukumu yake na haipaswi Kuingiliana!

Kila Mhimili wa Dola una Bajeti yake ya Mwaka ambayo inakuwa imeanisha matumizi kwa Mwaka Husika wa Mhimili Husika.

1: Bunge lina Bajeti yake yaani mishahara, posho na stahiki zote za wabunge

2: Mahakama vile vile ina Bajeti yake ya Mwaka

3: Serikali vile vile ina Bajeti yake kupitia wizara zake

Maswali:

1: Posho za Wabunge wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kibunge zinalipwa na nani? Bila shaka ziko katika Bajeti ya Bunge

2: Kamati za bunge zinapotembelea mashirika ya Serikali katika kutimiza kazi zao za Kibunge je Posho zinatoka Katika Bajeti ya Bunge au ya Serikali? Kama Wanalipwa na Bunge na kama vile vile Mashirika hayo yanawalipa je ni kutoka katika bajeti zao ( Mashirika) au! Na kama wanalipwa na Mashirika ina maana Wabunge huwa wanakuwa na bajeti Mbilimbili yaani kutoka Bungeni na Serikali? Je Mfano Bajeti ya Wizara ya mambo ya Nje ina Posho za Wabunge?

Naomba kufahamishwa Wakuu
 
Unaposema malipo yamefuata taratibu una maana gani? Mtu kalipwa mara mbili kwa kazi ile ile moja wewe unadai ndio kufuata taratibu! Na unaposema sio kazi ya TAKUKURU unamaanisha nini? Unataka kutuambia anayetakiwa kutekeleza Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11/2007 ni nani? Ukweli ni ukweli tu, hata kama utasemwa na Shetani! Kulipwa posho zaidi ya moja kwenye kazi ile ile ni ubadhirifu wa fedha za umma na ni kinyume cha sheria! It is criminal, to say the least! Naona waheshimiwa hawa hawajaondoa notion ya takrima vichwani mwao! Wameitoa kwenye uchaguzi wameiingiza kwenye "double payment." Hapa dawa ni kurudisha Azimio la Arusha (Azimio la Utu) lililokuwa na Miiko ya Viongozi wa Umma! I think it will be a permanent solution!

Buchanan,
  1. Wabunge sio waajiriwa wa serikali, kwa hiyo taratibu za malipo za serikalini sidhani kama zinawahusu.
  2. Taratibu za malipo zimefuatwa bungeni kwa wao kupewa posho zao. Sasa kama huko walikoenda kutembelea nao wana utaratibu wa kuwalipa wanaowatembelea, huo ndio wa kubadilishwa.
Sasa hiyo rushwa inayochunguzwa na TAKUKURU iko wapi?
  1. Mbona Hosea hakufuatilia zile posho na matumizi aliyoidhinisha Lowassa kwa mawaziri kwenda kuhubiri injili ya "sera" za serikali?
  2. Mbona ni mkimya juu ya posho za mawaziri?
  3. Je manunuzi ya mashangingi ya kifahari na helcopta zilizolalamikiwa amepitia mafaili yake?
  4. Mbona Hosea haongelei tena Richmond\ Dowans?
  5. Mbona hatufahamishi juu ya Radargate?
Hakuna anayefurahia kuona wabunge wakilipwa pesa na posho lukuki, wakati kipato cha waTZ kikiendelea kudidimia, lakini hiyo sio rushwa maana taratibu zilifuatwa.

Malipo makubwa na posho kibao za Wabunge ziliidhinishwa na serikali ya Kikwete ili kuwafunga midomo. Sasa kama wabunge wamegoma kufunga midomo, basi wasibadili sheria na kuyafanya yawe rushwa?

Kikwete asitugombanishe na wabunge wetu wakati huu wanapokwenda kuiweka kiti moto serikali yake juu ya Richmond. Kama hizo posho hazikubaliki na serikali, basi waziondoe kisheria na sio kuwachanganya wananchi.
 
alidiriki kuuita posho hizo kuwa ni TAKRIMA kutoka kwa watu wenye upendo juu yao anashida gombea ubunge mwakani na wewe uzipate. Takrima imefutwa kwan ni rushwa, sasa Spika anadai wanapewa Takrima, oh god.
 
Buchanan,
  1. Umejuaje kuwa mtoaji ndiye asiyejua kuwa mpokeaji tayari ana posho?
  2. Tokea lini TAKUKURU wakawa ndio wafuatiliaji wa malipo yanayofanywa kwa wabunge ambayo sio siri?
  3. Je huko serikalini hakuna wenye posho mara mbili za kufuatiliwa na TAKUKURU?

Kujua au kutokujua is a matter of logic kama wewe unavyojaribu kutumia logic kwamba mtoa posho anajua! Kujua au kutokujua kutajulikana baada ya investigation! It doesn't matter TAKUKURU wameanza lini kufuatilia suala hili! Kinacho-matter ni uhalali wa malipo mara mbili kwa kazi moja! Na haijalishi kwamba wanaofanya wako serikalini, bungeni au popote! Ubadhirifu wa fedha za umma ni ubadhirifu tu! Hawa waheshimiwa wabunge wetu tulishaanza kuwaamini, lakini kwa hili wamechemsha! Bila aibu Spika anaitaja takrima ambayo Mahakama ilishafuta vifungu vya Sheria ya Takrima ambavyo walivipitisha wenyewe wabunge! Nina shaka hata wewe ni mfaidika wa ubadhirifu wa "double payment" otherwise kwa nini unawatetea!
 
Hahahahahaaa!
Kwanini Watanzania tunachanganywa???? hoja ya posho imewekwa purposely kufukia uozo wa kashfa za Richmond, EPA, Kiwira, TICTS N.K. Ona members wa JF tulivyochanganywa hapa, hakuna kingine kinachoongelewa zaidi ya posho za wabunge ambazo Mkandara ameainisha hazidi milion 6 kwa mwezi wakati tumeacha kuzungumzia trilion za EPA, RICHMOND, IPTL, RADA,NDEGE YA RAIS, amkeni acheni kuchanganywa na Ka-Hosea, kajilinda, na kwa kiasi inaelekea katashinda maa the move has shifted from fundamenta and crtical issues to minor. Acheni posho tuendeleze libeneke la kashifa kubwa
 
alidiriki kuuita posho hizo kuwa ni TAKRIMA kutoka kwa watu wenye upendo juu yao anashida gombea ubunge mwakani na wewe uzipate. Takrima imefutwa kwan ni rushwa, sasa Spika anadai wanapewa Takrima, oh god.

Ndio mambo ya "Spidi na Viwango" hayo!
 
Kuna Mihimili mikuu mitatu ya Dola nayo ni

1: Serikali
2: Bunge
3: Mahakama

Mihimili hiyo mitatu ni Sawa kwa maana kila mmoja una Majukumu yake na haipaswi Kuingiliana!

Kila Mhimili wa Dola una Bajeti yake ya Mwaka ambayo inakuwa imeanisha matumizi kwa Mwaka Husika wa Mhimili Husika.

1: Bunge lina Bajeti yake yaani mishahara, posho na stahiki zote za wabunge

2: Mahakama vile vile ina Bajeti yake ya Mwaka

3: Serikali vile vile ina Bajeti yake kupitia wizara zake

Maswali:

1: Posho za Wabunge wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kibunge zinalipwa na nani? Bila shaka ziko katika Bajeti ya Bunge

2: Kamati za bunge zinapotembelea mashirika ya Serikali katika kutimiza kazi zao za Kibunge je Posho zinatoka Katika Bajeti ya Bunge au ya Serikali? Kama Wanalipwa na Bunge na kama vile vile Mashirika hayo yanawalipa je ni kutoka katika bajeti zao ( Mashirika) au! Na kama wanalipwa na Mashirika ina maana Wabunge huwa wanakuwa na bajeti Mbilimbili yaani kutoka Bungeni na Serikali? Je Mfano Bajeti ya Wizara ya mambo ya Nje ina Posho za Wabunge?

Naomba kufahamishwa Wakuu
NU,
Posho hulipwa na mwajiri wako tu na kwa case ya Wabunge ni ofisi ya BUNGE, kwa Mzee Kashilila. Unapolipwa na asiye mwajiri wako anakuwa ametoa taarifa kule ulikoajiriwa ili kuzuia ulipwaji mara mbili kwa shughuli hiyo moja. Ndio utaratibu na Wabunge wetu wanaujua sana. NJAA za WANASIASA WETU mbaya. Watoto wetu mashuleni wataendelea kukalia mawe tu kwa madarasa ambayo hayatamaniki.
 
Asante sana Ndugu yangu Kadi ya Mwituni

Kutokana na Maelezo ya jana ya Spika inaonyesha anafahamu suala wa Watumishi wake ( Wabunge) Kulamba Posho kutoka kwa Chombo ambacho siyo mwajiri wa Wabunge ( Serikali) aidha kwa kutaarifiwa au kwa njia yeyote ile. Ina maana Spika alikuwa na wajibu ya kutowalipa Watumishi wake kwa sababu wameshalipwa pesa vile vile kama wabunge walikuwa wameshalipwa pesa kabla ilikuwa ni Wajibu wa wabunge Ku declare kwa Serikali ( Nazungumzia mashirika) kwamba wameshalipwa na Mwajiri wao ( Yaani Mbunge) lakini inaonekana hawakufanya hivyo, so hawawezi kukwepa huu Uchunguzi.
 
Hahahahahaaa!
Kwanini Watanzania tunachanganywa???? hoja ya posho imewekwa purposely kufukia uozo wa kashfa za Richmond, EPA, Kiwira, TICTS N.K. Ona members wa JF tulivyochanganywa hapa, hakuna kingine kinachoongelewa zaidi ya posho za wabunge ambazo Mkandara ameainisha hazidi milion 6 kwa mwezi wakati tumeacha kuzungumzia trilion za EPA, RICHMOND, IPTL, RADA,NDEGE YA RAIS, amkeni acheni kuchanganywa na Ka-Hosea, kajilinda, na kwa kiasi inaelekea katashinda maa the move has shifted from fundamenta and crtical issues to minor. Acheni posho tuendeleze libeneke la kashifa kubwa

Mkuu tupo pamoja.
Hosea kalikuza jambola posho mara mbili utafikiri kuna mtu kaua! what is posho mbili by the way, especially when compared with the hundreds of billions of kodi za wavuja jasho wa Tanzania. Hosea anataka kuua nzi kwa kutumia mizinga!!

Hata kama wabunge wote, say wako 400 wakalipwa posho ya pili say shs 200,000 ni shs 80 million na hata kama wametembelea mashirika 10 itakuwa 800 million. What is 800 million ukifananisha na mamia ya mabilioni waliyotuibia? Hosea are you serious. kweli unafaa ku hold hiyo nafasi?! huwezi hata kufanya priorities. hata kama wabunge watakuwa wamefanya kosa, wakati huu ni wa kujua nini kimeendelea kwenye EPA, RICHMOND, IPTL, RADA,NDEGE YA RAIS, BOT TWIN TOWERS, KAGODA na wahusika wamewajibishwaje siyo kutuletea habari za vijiposho visivyo na msingi.

By the way ni wabunge waliodai hiyo posho au ni watendaji wa hayo mashirika walioamua kuwapa posho wabunge? mbona waliopokea hiyo posho ndiyo wameshikiliwa bango sana waliotoa wako wapi?

Hosea, hiyo posho ndiyo umeiona leo wabunge ambao ni wabaya wako kupokea? Rudi nyuma miaka kumi iliyopita, wabunge hawakuwa wanapokea hizo posho? Ofisi yako ilikuwa wapi? Je ni uzembe? kwa nini usiwe wa kwanza kuwajibika?
 
Hata kama wabunge wote, say wako 400 wakalipwa posho ya pili say shs 200,000 ni shs 80 million na hata kama wametembelea mashirika 10 itakuwa 800 million. What is 800 million ukifananisha na mamia ya mabilioni waliyotuibia?

By the way ni wabunge waliodai hiyo posho au ni watendaji wa hayo mashirika walioamua kuwapa posho wabunge? mbona waliopokea hiyo posho ndiyo wameshikiliwa bango sana waliotoa wako wapi?

Mkuu Jibaba

Come out of the Box and think Globally kaka, Hivi unajua ni kwa nini Wabunge wanatembelea hayo Mashirika au unafikiri wanakwenda Kunywa Chai na Kupiga Soga na Wakurugenzi wao?

Nitakupa Mfano mmoja, Wabunge wameenda Sehemu fulani kufuatilia ishu ya sumu katika maji kutokana na shughuli wanayoifanya katika eneo husika wanafika Pale wanakibidhiwa Vibahasha What do you think ripoti yao itakuwaje? Huo ni Mfano tu kaka
 
Nafikiri tatizo sio wabunge..na hata TAKUKURU kuwahoji wanafanya makosa....ila ni sheria na taratibu zilizo wekwa ndo inabidi zibadilishwe. Nakumbuka kipindi wanapitisha bajeti ilionekana kuna pesa nyingi sana ilitengwa kwaajili ya kuwalipa mawaziri na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kama takrima ilipigiwa kelele sana na wapinzani hadi ikaondolewa...Nawasihi waungwana wenzangu tupambane na sera na sheria zenye kuwanufaisha wachache. We unafikiri mtu anapogombea u-mbunge anagombea kwa maslahi ya nani? kwaajili yake na familia yake na sio kwaajili ya manufaa ya umma. Mwenye kubisha na aseme na atoe mfano wa kiongozi aliye-gombea kwaajili ya umma.
 
wewe una lako jambo!

Inawezekana nina langu jambo! lakini sioni sababu ya kuendelea kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa. Kama kweli kuna jambo ambalo kwa mtazamo wangu naona halijakaa sawa kwa nini nisiseme. Siwezi kumsifia kwa kila kitu anachofanya kwa sababu tuu amekuwa anaongoza vinavyoitwa vita vya ufisadi. Tuwe realistic wakati mwingine. thats why mzee Ben, pamoja na wizi wote aliofanya, bado ninanguvu ya kusimama na kutetea machache mazuri aliyofanya. Na huyu Mkuu Spika, Pamoja na mengi mazuri aliyofanya, bado ninanguvu yakuweza kusimama na kusema kuna namna simwelewi anavyopeleka mambo yake.
 
Kuna mtazamo ambao Tanzania inataka kuuchukua ambao ni hatari. Kwamba Mwakyembe kafanya mazuri, basi mazuri daima, na kama Flani kafanya mabaya basi kafanya mabaya daima. I guess this is not correct at all. Sita has being a good speaker in records but that does not give him absolute perfection. there is piont missing somewhere and so people must stand and talk. Sifa za kila wakati zinaweza kumpoteza kisiasa!
 
Back
Top Bottom