Mkandara,
- Mkuu, ubadhirifu wa matumizi ni pale pesa inapotumika bila kuwa imeidhinishwa kisheria. Hizo posho zimesainiwa na Raisi mwenyewe na kupitishwa kwenye bajeti na hivyo sio RUSHWA. TAKUKURU hawana uwezo kisheria kuzichunguza.
- Kama wananchi hatuzipendi hizi posho, tunatakiwa kuingia mitaani kupambana na Kikwete kwa kuziidhinisha.
- Hili la TAKUKURU kuwachunguza wabunge ni mbinu tu ya kuwanyamazisha.
Sio lazima kuwa kila kinachopitishwa kisheria hakiwezi pia kuwa ni ubadhirifu. Kigezo cha ubadhirifu ni uhaki wa yaliyopitishwa. Jee hayo yaliyopitishwa kisheria yana harufu ya rushwa au kifisadi? Kama hayo yapo basi sheria hiyo si halali.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo, ungejua yaliyotokea Uingereza. Huko Wabunge walipitisha kisheria kabisa kuwa walipiwe kwa mambo yao binafsi kama vile kutengeneza bustani zao, kulipiwa mortgage ya nyumba zaidi ya moja, kununua vitu vya nyumbani etc na wakawa wakidai matumizi hayo kisheria kwa miaka mingi tu. Hivi juzi juzi tu wananchi wakachachamaa kuwa sheria hizo zilikuwa si za haki na ni zakifisadi. Wabunge waliofanya hivyo, wakalazimika kurudisha fedha hizo ingawa zilipitishwa kisheria na ikasababisha Spika wa Bunge kujiuzulu kwa kutetea ujinga kama huo.
Kwa mtu mwenye busara, kipimo hapa ni jee ni haki mtu mwenye heshima kama Mbunge kuiba fedha za umma kwa kujilipa mara mbili kwa kazi ile ile?
Hayo mengine yote ni justifications zisizokuwa na msingi.