Robweme
Senior Member
- May 20, 2009
- 178
- 6
Kupokea posho mara mbili mbili kunadumaza Taifa. Kwanini wasipige kelele? Ni kuogopa kuitwa wapinzani uchwara? Mbona hilo wameshaitwa saaana. Kwanza wao ni wabunge, na issue inahusu wabunge. Kama wabunge wa upinzani lazima wataulizwa na waandishi wa habari ni nini msimamo wao. Wakikaa kimya watapakaziwa wanalindana. Halafu hivi kutafuta mawakala si jukumu la mgombea? Sidhani kama ni busara kumhusisha Katibu Mkuu au Naibu wake. Watafanya mangapi? Hilo ni suala la kurugenzi ya Uchaguzi.
Mimi binafsi wabaya wangu wakigombana nitashabikia ili wauwane wasije hata kuafikiana baadaye. Kama ikishindikana nitachochea mpaka watoane macho hata wakija patana wana makovu ya kudumu. Hapo nitajihesabu nimeshinda.
.
"Tatizo hapa ni kutoelewana, mimi nadhani washughulikie Richmond kwanza alafu mambo ya kupokea posho mara 2 au mara 3 yatakuja baadae, kwani suala la posho mara 2 mbona magereza itajaa."