Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Wakulu, hapo Hosea hajasema chochote kipya ambacho hatukijui..walau kwa duru za hapa JF!


Niwaulize ndugu zangu waandishi, je mlimuuliza maswali magumu au ndo mlienda, mkasikiliza 'hotuba' ya Hosea akisema 'hatajiuzulu', na pengine na kabahasha ka kaki (this time sio mara mbili) na kuondoka kisha kesho mtaripoti "Hosea alishukia bunge"?
 
labda anatangaza kujiuzulu


kabla ya jumatano hajasulubiwa


HAJAJIUZULU MTU, Tena ametema mbovu sana kwa nyie mnaosema atajuuzulu.
Kwa ufupi alichosema ambacho nimekipata kutokwa kwa waliokuwa huko ni kuwa; hatojuzulu na kwamba yeye anachunguza 'posho mbili' kwa maagizo ya bunge kwa vile ndilo lilolomwandikia barua tarehe 26/02/2009 kuomba yeye kama TAKUKURU achunguze suala hilo.

Amedai sheria anayotumia kuwachunguzia wabunge 'Posho mbili' ilipitishwa na bunge lenyewe tena na wabunge hao hao wanaogoma kuhojiwa

Pengine la kuvutia katika mkutano huo Dr Hoseah alipoingia tu alianza kwa kusema "Sijiuzulu ng'o, maana toka asubuhi ninapigiwa simu za watu wakiuliza kama nimejiuzulu".

Dr Hosea amemalizia kwa kuwawambia (kama Sitta alivyosema waende majimboni) 'Wabunge ambao wanaona yeye anafanya makosa kuwachinguza, wapige kura (Bungeni) ya kutokuwa na imani naye, na yeye yupo tayari kwa lolote litakalotokea, huku akijiganba kuwa TAKUKURU sio mwisho wa maisha yake hata na kutamba "there is life after PCCB".
 
Ama kweli Hosea hana kazi... yaani kazi yote ya kuwaita waandishi wa habari ni kuwambia yale ambayo tayari tunayafahamu..
1.Barua imeandikwa na katibu wa bunge, hakuna report ya bunge lenyewe kupitisha kazi hiyo ifanyike. Spika wa Bunge amekana kuelewa lolote husiana na uchunguzi huo, nilitegemea Hosea amekuja kuhakikisha hilo. Kama kuna sheria kwa nini asiitaje wazi! sheria sio ombi la barua ya katibu.
2. Hosea anaposema anawaomba Wabunge wanaopigana na Ufisadi watoe ushirikiano ana maana gani?..Ni kina nani hao.
3. Mwakyembe amekataa kuhojiwa kwa simu akitaka kuwepo na record ya mahijiano na sii kuhojiwa kiholela kwa masaa 3..
Inajulikana wazi wabunge wanaopinga Ufisadi ni 11 tu, iweje malalamiko ya Wabunge hawa wachache iwe sababu ya Hosea kudai hajali akiondolewa PCCB na kwamba - there is life after PCCB!
Hivi kweli anaifanya kazi hii ili kuendesha maisha yake au ni jukumu alokabidhiwa. Inaonyesha kama vile watu Bongo wanafanya kazi ili waishi, na ndio maana hawana vision hata kidogo nje ya kujitajirisha wao.
 
Akiwa ametangaza kukutana na waandishi wa Habari kesho saa 4 asubuhi, Mkurugenzi wa TAKUKURU Edward Hosea anatarajia kutangaza kuachia ngazi. Kikao hicho pia atakitumia kurusha makombora kwa wabaya wake akiwepo adui namba moja Dr. Mwakyembe.

Serikali inatarajia kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kesho Jumanne, kujiuzuru kwa Hosea itakuwa ni sehemu ya utekelezaji au hatua mojawapo katika kutekeleza maazimio ya bunge.

Tusubiri hiyo kesho tushudie.
 
Mbona unatuchanganya mkuu wangu, kichwa cha mada tofauti na yaliyomo.
 
Mbona unatuchanganya mkuu wangu, kichwa cha mada tofauti na yaliyomo.
mh we acha tu yani mi nikajua ndo tayari kesha tangaza kumbe tusubiri Kesho! kama ni kweli mambo mswano kazi ipo!
 
Mbona unatuchanganya mkuu wangu, kichwa cha mada tofauti na yaliyomo.
Post yake ni ya saa 10.05pm leo wakati kuna thread humu zinazungumzia mkutano wa Hosea na waandishi umeshaisha na Hosea kasema hajiuzulu ng'o, yeye kang'ang'ania TETESI TETESI!
 
Nilitaka kushangaa eti Ngosha ajiuzulu nani kasema?
 
Si ujua tena wabongo tunapenda kutafuniwa na hata kumezewa!

yale yale ya uvivu wa kujituma..unakuta mtu na familia yake usiku wanampigia simu mchungaji awasalie/awaombee wanataka kulala..hahaaaa
 
Kwa sababu ni tetesi ngoja na ibaki kama tetesi- Dkt bado anaitajika Pccb.
 
Kutoka kwa mdau.


Aidha amewataka wabunge ambao wanaona anafanya makosa kuwachinguza, wapige kura ya kutokuwa na imani naye, na yupo tayari kwa lolote litakalotokea, huku akijiganba kuwa TAKUKURU sio mwisho wa maisha yake hata kidogo, "there is life after PCCB" anasema Dr Hoseah-

Hosea,
Kama wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani nawe, sio kwa sababu ya posho mbili, ila kwa sababu ya taasisi yako unayoiongoza kuwasafisha mafisadi na wezi wa Richmond...naona kama unataka kudivert issue ili ionekane wabunge wanataka kulipiza kisasi kutokana na majukumu yako.
 
Back
Top Bottom