Possi: Dubai ina uwezo wa kuingia mikataba imekasimiwa kwa mujibu wa Article 120 – 123, ya katiba ya Umoja wa Jumuia za Falme za Kiarabu

Possi: Dubai ina uwezo wa kuingia mikataba imekasimiwa kwa mujibu wa Article 120 – 123, ya katiba ya Umoja wa Jumuia za Falme za Kiarabu

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
330
Reaction score
962
Utangulizi:
Ni ukweli usiopingika kuwa kulingana na unyeti wa rasilimali bandari kwa taifa na ukizingatia kuwa ni lango kuu la uchumi, na maswala ya ulinzi na usalama. Na zaidi sana kuwa mchakato wa kuridhia mkataba wa aidha kuuzwa (opion ya wapingaji) au kupangishwa (opinion ya wa wasiopinga) ulishamalizika na kuridhiwa na Bunge (JMT) lakini sintofahamu katazi kwenye vichwa vya wengi au wachache (kadili kila mtu aonavyo) zimeendelea hivyo episodi za ufafanuzi ndio sarakasi za kila siku kutoka kwa wajuvi wa mikataba; kama vile, wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi wa dini, mapandikizi, machawa na wengine wengi, lakini Leo episodi hiyo imemnyanyua Naibu Katibu Mkuu wa wizara husika, kuendelea na ufafanuzi wa serikali dhidi ya wapotoshaji (wananchi). Kwa nafasi yake kama mwanasheria mbobezi, amejikita kwenye vifungu vya sheria, nami sina budi kuwashirikisha kama ifuatavyo:

Uwezo (Capacity) wa kuingia Mkataba;
Uwezo (capacity) ni takwa la kisheria, "ya sheria za mikataba ya kimataifa ya Vienna ya 1969" (Vienna Convention on the Law of Treaties, (VCLT)). Hivyo ukisoma ibara ya 6 ya sheria hizo, inaeleza ili nchi iwe na uwezo lazima iwe “ state” neno state limetafsiriwa na kuelezwa vizuri kwenye ibara ya 1 ya "Montevideo convention on rights and duties of states ya 1933";

Ufafanuzi wa Swali aliloulizwa na ITV

Je, Dubai ni nchi?


Akijaribu kufafanua kuhusu kwa nini Tanzania imeingia mkataba na Dubai Emirates (Emirate Member) na badala ya Umoja wa Jumuia za Falme za kiarabu (the United Arab Emirates), kama nchi? Naibu Katibu amesema.

Kama ilivyo Tanzania na Zanzibar, Dubai pia kuna mambo imekasimiwa katika maswala ya Uwekezaji na Biashara, akinukuu ibara mfuatano za katiba hiyo yaani ibara za 120–123 ya katiba yao. Ambazo zimejumuisha mambo ya Muungano wa Umpja wa Jumuia za nchi za falme za Kiarabu. Kuwa Dubai kama mshika wa Jumuia anaruhusiwa kuingia kwenye mikataba ya kimataifa kama hiyo waliyoingia nayo.

Je, ibara hizo zikoje?
Nimejaribu kusoma sehemu ya saba (part seven) yaani ibara 120 -125 ya katiba yao, na kurejea mara kadha wa kadha sijaona sehemu yeyote ambazo Umoja wa Jumuia za falme za kiarabu kama nchi imekasimu maswala ya uwekezaji na biashara, au mahusiano ya kimataifa (foreign relations) kwa falme husika (emirate member).

Mambo ambayo Falme (member emirates) inaweza kuingia kwenye mikataba:
Uhusiano wa nchi na nchi (foreign relation) au (diplomatic relations), ni Kati ya mambo 19 yaliyoanishwa kwenye ibara ya 120. Ni hivyo moja kati ya mambo hayo ni uhusiano wa kimataifa, (foreign relation), kama inavyosomeka kwenye ibara 120 (1) ya katiba yao.

Kwa lugha nyepsi tunasema mambo ya mahusiano kati ya the United Arab Emirate na nchi nyingine yapo chini ya Umoja ya Jumuia ya Falme za kiarabu kama nchi, na si washiriki wake (emirate members) na inasisitizwa Zaidi katika ibara za 124 na 125 za katiba yao.

Isipokuwa (exception ) ni ibara 123 vikisomwa kwa pamoja na ibara ya 120 (1) ya katiba yao imetoa ridhaa ya ya makubaliano ya sehemu ndogo , (limited agreement) ya ndani kwa falme husika, na yenye asili ya kiutalawa ( administrative in nature), yasiyo ya kufungamanisha nchi, ya yanaweza kufanyika kwa nchi Jirani na Jumuia za kikanda za maeneo yao ya karibu.

Mahusiano yote, yanaridhiwa na Umoja wa nchi za falme za kiarabu yanayohusisha mahusiano ya kimataifa lazima yatoke kwa nchi hiyo, yaani the United Arab Emirates, hii ni kwa mujibu wa ibara 124 na 125 ya Katiba yao ya mwaka 1996.

HITIMISHO:
ndio maana ukisoma instrument iliyotumika kumpa ridhaa mkurugenzi wa bandari yaani, Chief Executive Officer of Ports, Customs and Free zone, Mr. Ahmed Mahboob Musabih, haielezi ridhaa hiyo imetoka Dubai Emirates au the United Arab Emirates. wote wametamkwa na hakuna kiongozi yeyeto aliyetajwa kumpa mamlaka hayo, wakati ya Tz ipo very straight, imetolewa na Rais wa JMT, anliyepokea ni Waziri.

 

Attachments

Back
Top Bottom