Inawezekana, lolote likisemwa kuhusu nchi yetu siwezi kukataa inawezekana post zikawekwa na kuondolewa ghafla. Labda walijisahau wakawapangia watu wa kilimo vituo vya ualimu na waliwa wakapelekwa vituo vya afya! Ni kawaida kwa Tz. Kama matokeo ya mitihani ya na rudiwa kupikwa sembuse ajira?
ualimu mkuupost za nini!?
Wadau nauliza ni kweli post za ualimu zimeshatoka na nicheki website ipi kama zimetoka mana kuna mtu ananisumbua
Nime kaa chumbani na rafiki yangu, mara akatumiwa sms post zimetoka waambie na wenzako, tembelea MOE, jamaa mbio mpaka kwenye simu lakin kutazama hakuna...
Tukaona labda kwa simu haionyeshi, washa PC nako hamna kitu, tulipo mpigia jamaa akaapia mara mbili mbili ni kweli yamewekwa na sio mtu wa matani !!
Akasema tumpe jina arudi cafe, ile anarudi akasema wamesha yatoa !!
Kwa hiyo mnao subiri mkae chonjo!!
jamani walimu,msiwe wagumu kuamini mbona ndo miezi ya post hii,pia nashukuru sana walimu wa siku hizi hawapo tayari kubweteke na viela hivi kidogo,ombi langu kwa walimu ukipata kazi mara moja anza ujasiriamali.