Posta Tanzania hongereni kwa huduma nzuri na nafuu

Nchi hii kuna watu fikra sijui hata za karne ya mwaka gani.

Sijui Sanduku linalipiwaje, ila wapo wapo tu yaani utafikiri Posta imekufa.

Imagine hata Hati tu ya kusafiria ambayo ni Tsh 150,000 Uhamiaji wakitoa hata kwa watu 1M tayari ni 15B lakini ndio hivyo hawatoi tu ili kuonesha kama Passport ni kitu cha hadhi kuuuubwa ambacho siyo kila mtu anapaswa kuwa nacho.
 
Dada wa posta Alinambia kufungua box Ni elfu 40, Ila uwe na namba ya Nida.
 
Nipe jina la hio page au link tuifate ila mie malalamiko yangu huyatuma kwa njia ya email nikianzia ngazi yangu ya chini adi makao makuu
 
Nipe jina la hio page au link tuifate ila mie malalamiko yangu huyatuma kwa njia ya email nikianzia ngazi yangu ya chini adi makao makuu
Hiyo mkuu. Ukicomment make sure unatag hiyo user name yao, ndio atarespond kwa haraka.
 
Mkuu Kama ulitumiwa na mtu ilifaa aliyekutumia apeleke malalamiko posta ya huko. Wangemrefund
Nilipata refund
Piga picha hapo ilipo kisha nenda General posta na evidence yako kadai fidia je seller aliku refund au ndio ulipotea tu kiswahili
Nilipata refund ndio maana sikuitilia maanani sana japo ilinipotezea muda na pesa yangu ingetumika kufanya mambo mengine ya maana kwa muda huo walionipotezea
 
Nilipata refund

Nilipata refund ndio maana sikuitilia maanani sana japo ilinipotezea muda na pesa yangu ingetumika kufanya mambo mengine ya maana kwa muda huo walionipotezea
Nlitaka nishangae. Mzigo ukitumwa wenzetu wanaukatia na insurance. Incase upotee lazima wakurefund
 
Ndani ya siku ngapi ukawa na simu yako mkononi?
 
Haha kweli mkuu ndugu ya kanda ya ziwa. Umenena ukweli mtupu. Matumizi mazuri ya akili haya.
 
Hivi mzigo ukipotea unaanzia wapi procedures za malalamiko, je unapeleka mahakamani shitaka la madai au ndani ya offisi husika iliokua na mzigo wako kwanza kabla ya kwenda mbali zaidi,

Sent using Jamii Forums mobile app
Procedure Anafanya aliyekutumia. Aende post office aliyotuma akacomplain wenzetu wanarefund faster tu, coz mizigo inakuwa imekatiwa insurance.
 
Posta wakikaza buti hata ndani ya nchi tu, wanaweza kupunguza idadi ya machinga kwa zaidi ya 60%.
Wanapoteza mapato mengi sana sasa hivi, makampuni binafsi ya usafirishaji wanafanya kazi ambazo wao wangefanya kwa bei nafuu zaidi, kwa mfano, ukituma barua kwa EMS wao wanakutoza Tshs 13,000.00 lakini mtu akipeleka kwenye kampuni ya uchukuzi analipa 5,000.00, kwahiyo na wao wangeshusha gharama huenda wangekusanya zaidi
 
DHL zaidi ni vifurushi/ documents muhimu, vya thamani na haraka. Mtu ananunua protector ya simu anataka kusafirisha na DHL wapi na wapi.
 
Katika shirika ambalo lingeweza kujiendesha vizuri na kutanuka kila mahali ni posta. Hili shirika lingeingizia serikali mapato mengi sana kama wangekuwa wabunifu. Serikali ingefanya kama lilivyokuwa zamani i.e. posta na simu lijihusishe na kusafirisha vifurushi, kutuma na kupokea fedha nk likuwa bonge la shirika.
 
Dah niliumia sana, mbaya zaidi parcel ikawa inaonyesha tayari imefika bongo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijajua hiyo parcel yako kama ulinunua au ulitumiwa zawadi?

Na sijajua ulivyoenda kupokea walikuambia nini na tracking ilikuwa inasoma vipi?

Labda ungeyajibu hayo ungeweza kusaidika.

Mimi mizigo yangu yote status ya location ikishaanza kusoma Tanzania, Iwe ni GPO au TZKAR au popote pale huwa nawafata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…