Poteza simu/ Laptop unaweza kununua nyingine lakini mafaili binafsi yakipotea imeisha hio! Tupeane mbinu za kutunza copy za mafaili tukwepe majanga

Poteza simu/ Laptop unaweza kununua nyingine lakini mafaili binafsi yakipotea imeisha hio! Tupeane mbinu za kutunza copy za mafaili tukwepe majanga

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Wanasemaga huwezi kujua thamani ya kitu mpaka kipotee, ukiwa nacho waweza kukichukulia poa lakini kipotee sasa, tena kiwe na attachment yako ya maisha yako, historia, mali zako, elimu, n.k.

Binafsi nkumbuka kuna siku nimeenda jengo flani nikapaki gari huku nimeacha laptop, ile narudi nakuta laptop haipo wahuni washafanya yao kwa mbinu wanazojua wao, acha kabisa wakuu!! nilihisi kuchanganyikiwa maana mafaili kibao kuanzia picha zangu za ukumbusho, videos, documents, vyeti, n.k. zikawa zimeenda MOJA KWA MOJA. very painful!!

Mafaili haya yakienda huwa yameenda kama huna copy zake tunazoita backup, mafaili kama muvi na miziki unaweza kudwnload upy ila mafaili binafsi hio ni ishu nyingine kabisa, hata ukibahatika kukuta simu au laptop yako iliyoibiwa kuna uwezekano mkubwa ishakuwa formatted ama kuflashiwa.

Binafsi nilienda kununua hard disk ya gb 500, ni maalum kwajili ya kutunza data private, huwa siweki muvi wala miziki labda iwe ngumu kuipata

Online naipenda pia lakini changamoto ni kwenye bei za vifurushi, natumia google drive wanaotoa gb 15, nazitumia zaidi kutunzia nyaraka za pdf,

Tujuzane zaidi tafadhali.
 
Wanasemaga huwezi kujua thamani ya kitu mpaka kipotee, ukiwa nacho waweza kukichukulia poa lakini kipotee sasa, tena kiwe na attachment yako ya maisha yako, historia, mali zako, elimu, n.k..
Google drive ndo ninayotumia kuhifadhia
 
Natumia Google drive inshort nime set simu yangu inafanya auto save, nikipiga picha ama kudungua picha yoyote Moja Kwa Moja inakwenda google drive.

Umesema kweli kabisa Kuna document zikipitea ndio imeisha hivyo; Mwaka Jana nimekula hasara sitakaa nisahau maana Kuna document zilipitea TU ndani bila kukua zimeenda wapi.

Kati ya document zilizopotea zilikuwemo za mauziano ya Shamba heka 200, Shamba Lina mgogoro, alieniuzia ameshakufa document nazo hazionekani. Imebidi nitulie tu. Sio Hilo tu no vingi vinaenda kupotea.
 
Clouds kama OneDrive Nina Mwaka Wa kumi sasa natumia bila usumbufu wowote..., External hdd 1TB..., Cd pia uwa zinasaidia sana aisee, Burn vitu vyako muhimu kwenye Cd.. Hutojutia.
 
Cd shida yake inaharibika kirahisi sana

Ni utunzaji tu ndugu yangu, unanunua kibegi tu flan cha kuwekea cd zako unazipanga umo fresh kabisa, alafu unakihifadhi tu.

Niliuona umuhimu wa cd nilipoibiwa begi langu la mgongoni usiku wa saa 9 kupitia dirishani.. Nilipigwa laptop, external, flash zote zilikuwa umo ad wallet. Nikakumbuka vitu muhimu niliviweka kwenye cd, nilishukuru sana we acha tu.
 
Ni utunzaji tu ndugu yangu, unanunua kibegi tu flan cha kuwekea cd zako unazipanga umo fresh kabisa, alafu unakihifadhi tu .. Niliuona umuhimu wa cd nilipoibiwa begi langu la mgongoni usiku wa saa 9 kupitia dirishani.. Nilipigwa laptop, external, flash zote zilikuwa umo ad wallet... Nikakumbuka vitu muhimu niliviweka kwenye cd, nilishukuru sana we acha tu.
Dah noma sana ni njia nzuri ila shida yangu ipo sana kwenye utunzaji inabidi uikague mara kwa mara laa sivyo unaweza kupoteza kote
Njia rahisi sahiv ni online
 
Dah noma sana ni njia nzuri ila shida yangu ipo sana kwenye utunzaji inabidi uikague mara kwa mara laa sivyo unaweza kupoteza kote
Njia rahisi sahiv ni online
Upo Sahihi, lakin unajua kaka, kuna document fulani binafsi si salama sana kuziweka online..
 
Natumia Google drive inshort nime set simu yangu inafanya aoto save, nikipiga picha ama kudungua picha yoyote Moja Kwa Moja inakwenda google drive.

Umesema kweli kabisa Kuna document zikipitea ndio imeisha hivyo; Mwaka Jana nimekula hasara sitakaa nisahau maana Kuna document zilipitea TU ndani bila kukua zimeenda wapi.

Kati ya document zilizopotea zilikuwemo za mauziano ya Shamba heka 200, Shamba Lina mgogoro, alieniuzia ameshakufa document nazo hazionekani. Imebidi nitulie tu. Sio Hilo tu no vingi vinaenda kupotea.
ujinga wa Google Drive storage ndogo yani 15GB la sivyo ununue, mi nna email mbili kwa ajili ya kupata 30GB.
 
Mimi natumia telegram rahisi sana
Mimi mwenyewe nilikua nikitumia hii ila kwasasa imenitoka, kuna wahuni wa huko mbele wamenihack sijui wa nchi gani maana Lugha sio English.

Wamejiunga magroup kibao ambayo siyajui alafu ubaya wameweke 2FA ambayo mimi sikuwa nimeweka hapo awali. Nimepambana kurudisha ikawa ngumu imebidi nikubali kupoteza vitu vyangu vyote nlivyokua nimevisave huko.
 
Back
Top Bottom