Poultry farm Manager (Msimamizi wa Shamba la Mradi wa ufugaji wa Kuku wa Nyama)

Poultry farm Manager (Msimamizi wa Shamba la Mradi wa ufugaji wa Kuku wa Nyama)

CASSIUS

Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
36
Reaction score
5
Anahitajika mtaalamu wa kilimo na mifugo mwenye elimu ya kuanzia ngazi ya stashahada mwenye ujuzi na uzoefu kwenye tasnia ya ufugaji wa kuku wa nyama wa kisasa.
Eneo la Mradi: Kazimzumbwi - Kisarawe (Pwani)
Anatafutwa mtu mwenye sifa:-
  • Mwenye ujuzi na uzoefu wa kusimamia na mradi wa ugugaji wa Kuku wa nyama
  • Awe na elimu kuanzia stashahada (diploma) kwenye kilimo na mifugo
  • Kuelewa chanjo, vyakula, magonjwa na tiba kwa kuku
  • Mwenye leseni ya kukagua nyama
  • Ujuzi wa kuendesha na kusimamia mashine za kuchinja na kuchakata kuku
  • Uelewa wa matumizi ya kompyuta
  • Uwezo wa kuongoza na kusimamia watu
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa za mradi
Kwa mwenye sifa hizo awasiliane na Project General Manager kupitia justusaugust@outlook.com kwa ajili ya kumpatia maelekezo zaidi.
 
Nimekaa kwenye mazingira ya ufugaji wa Kuku wa Mayai na wa Nyama (Broilers) kiasi kwamba najua mfumo wake wanavyolishwa,na kuhudumiwa kwa ujumla. Ila sijawahi kusomea Elimu ya Mifugo. Kwa kifupi sina vyeti. Nshaenguliwa by default naona.
 
Tofauti na vyeti, je upo na ujuzi wa kuendesha na kusimamia mashine za kuchinja na kuchakata kuku?
 
Tofauti na vyeti, je upo na ujuzi wa kuendesha na kusimamia mashine za kuchinja na kuchakata kuku?
Mkuu,Naweza kusema ndiyo.
Tulikuwa tunatumbukiza kuku kwenye mashine za kuwanyonyoa per day kuku 1500-2000 kulingana na demand,then wanasafishwa na kufanyiwa packaging tayari kwenda kwenye hoteli hasa hasa kwenye baadhi ya Kampuni za Utalii huko Hifadhini. Nilikuwa Arusha by then. Baada ya COVID kuingia biashara ya Utalii ilisimama sana,kiasi kwamba oda za kuku zikawa hamna. Hivyo naelewa kinaga ubaga kutoka Kuku akiwa bandani hadi anawekwa kwenye mfuko tayari kwa matumizi ya binadamu!
 
Kuna jamaa yangu kasomea Hayo Na anafanyaga kama consultancy ya projects mbalimbali Za Kuku(mtwara,Tanga,kibaha,kisarawe nk.)...inshort jamaa Ni Messi wa Kuku ila Sasa Hana simu kubwa labda ungetoa namba Za kawaida
 
Back
Top Bottom