Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
- Thread starter
- #81
Sungura tupo kuongea kitu kimoja mkuu . Sema tu kua tatizo ni mitazamo ambayo inagongana huku ikiwiaana sehemu na sehemu. Tokana na maelezo yako naona upo pamoja na Zakumi, kua lawama zote abebe Kiongozi for s/he is the one wholly responsible .
Tukitolwa mfano wa gari uliotoa.. Kumbuka kua hata magari nayo sio madereva wote waweza endesha, kwa kuzingatia hilo hilo gari dogo unakuta kua kuna dereva; tena ni derevaq mzuri . ambae anaendesha automatic tu! Ukimletea manual, unakua umem Knock out! Hivo basi mtu anapokua kiongozi peke yake haitoshi . Dereva kama dereva anakua tu analiongoza lile gari . What matters katika uendeshaji salama na ulio reliable katika gari ni injin, matairi na mafuta .. Kwa muktadha huo Viongozi na watu wake wote wanatakiwa kuwajibika ipasavo. Kikubwa huyo kiongozi ahakikishe ni dereva mtunzaji (sio rough!); na pia kuahakikisha entities zote za muhimu katika hilo gari zaenda sawa kabisa ahakikishe mafuta ya kutosha, ahakikishe oil kwenye injini ni safi na ahakikishe kua tairi zipo katika hali nzuri na tire bolts zimekazwa vilivo
Nikija nchi ya Ruanda, hio ni moja ya nchi I am so proud of katika a group ya hizi za developing nations . Sa ingine genuinely hata hua najiuliza kua viongozi wetu (hasa JK) kama kamtembelea Kagame na kumuuliza how has he done it? After a short while of such development katika sector nyeti za maendeleo ya nchi .. Hata hivo tujiangalie wa Tanzania . Nidhamu zetu zipo vipi makazini? Wenzetu Warundi, Wakenya wakija makazini wapo vipi attitude yao towards work? Tukipata jibu hapo tunapata jibu tatizo sio viongozi peke yao Tatizo ni pana zaidi ya Viongozi kua Responsible and good Leaders .
AshaDii,
Kwenye thread "Kwanini watanzania ni maskini?" Niliambiwa kuwa ninailinda "The Status Quo" pale niliposema kuwa wananchi nao wanatakiwa kuchukua wajibu wao katika utekelezaji wa mambo. Je inakuwaje kwenye thread hii nimepabadilika na kuanza kukosoa uongozi?
Threads hizi mbili zinafanana. Lakini kuna tofauti za kimsingi. Kwenye "kwanini Watanzania ni masikini" kuna sababu nyingi za kueleza. Tupo masikini kwa sababu ya hali ya hewa, rushwa, ukoloni, sera mbovu, uongozi mbovu na mambo mengine. Au kuna sehemu nyani wanakula mahindi na kufanya watu wawe masikini.
Katika thread hii tunaangalia process ya kujitoa kwenye umasikini. Baada ya kuzijua sababu, tunatakiwa tuchukue hatua. Je ni hatua gani? Tanzania hatua hizi zinachaguliwa na viongozi, hivyo wao ndio wenye kubeba lawama pale wanaposhindwa.
Mfano wako wa Rwanda ni ushahidi mkubwa kuwa process ya maendeleo inahitaji viongozi wawe makini. Kwani wao ndio wata-instill the right attitudes kwa watu wao.