Mpingamkoloni
Member
- Feb 14, 2021
- 13
- 33
Mfumo wa ununuzi wa TANePS pamoja na changamoto zake, ulikuwa mfumo mwepesi kujisajili na kuutumia. Changamoto zilizoifanya TANePS iondolewe, ni hizo hizo zinaikumba NEST kwa sasa.
Mfano ilikuwa inalalamikiwa kwamba mfumo wa TANePs ulipokuwa na hitilafu za kiufundi, ilipaswa kuitafuta kampuni iliyotengeneza mfumo iliyokuwa nje ya Tanzania, jambo ambalo binafsi siamini kama ni shida kwa ulimwengu wa sasa, haya sasa lakini sasa NEST imetengenezwa Tanzania, lakini ukiwasiliana na NEST customer care 0736494948 sawasawa na maelekezo yao ya emails, utapiga simu siku nzima bila kupokelewa.
Usajili wa kampuni zilizokuwa zimesajiliwa TANePS na baadhi kulipia annual fees ulipaswa uwe kwa migration na si kujisajili upya. Wazabuni wengi hadi sasa hawajasajiliwa NEST, ingawa walikuwa wanatoa huduma TANePS na kwenye taasisi za serikali.
Usajili uliokuwa unafanyika TANePS kwa siku moja au mbili tu, kwenye NEST unatumia zaidi ya mwezi. Mfumo uko complicated bila sababu. Biashara yenye leseni tatu au nne, mfumo utahitaji uweke leseni zaidi ya mia ambazo uhalisia ni duplication, maana kibali ni kilekile.
Kwenye mfumo wa NEST hawajaweka kibali cha Pharmacy Council, ambacho hicho pia ni kibali cha mojawapo ya biashara.
Pia taasisi nyingi za serikali sasa zinashindwa kufanya manunuzi ndani ya NEST kwa sababu bado vitu havijakaa sawa, na yamkini havitakaa sawa.
Bahati mbaya siamini kama mfumo wa NEST utabadirika, maana waliotengeneza ni watu, ambao huwezi kuwabadirisha wanachoamini.
Fanyeni mfumo uwe simple kujisajili, iwe simple kuutumia, watumieni wataalam toka sekta mbalimbali, hadi taasisi nunuzi na wazabuni, ili wawape ushauri mboreshe mfumo.
Migration ya kutoka TANePs kwenda NEST mlifanya kwa kukurupuka sana. Mlitakiwa mhame hatua kwa hatua.