Precision air washusha flight fare

bhageshi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2010
Posts
264
Reaction score
101
Katika hali ya kuonesha ushindani katika biashara ya usafiri wa anga unaongezeka siku hadi siku, kampuni ya ndege ya Precision nayo imeshusha gharama za usafiri kwa mteja wa Precision Air, sasa waweza kutoka mwanza kwenda DAR kwa sh 98000 tu na kwenda na kurudi kwa sh 149000 tu. Awali return ticket ilikuwa Sh 275,000/- and above. Nadhani kwa style hii fast Jet waboreshe huduma zao maana they are very rude in caring customer, mizigo hawataki, samaki hawataki lakini mbaya zaidi hata hawatangazi vitu visivyoruhusiwa kuchukuliwa unajiaandaa na samaki wako unafika airpot wakati wa checking wanakuambia huu mzigo hatuchukui pata picha inayotokea baada ya kupewa taarifa hiyo juu ya mzigo wako tena kitoweo....
 
Ushindani wa biashara na itashuka zaidi ya hapo!
 
mtoa mada wewe issue ni samaki tu? watz kwa tumbo bwana tutafika kweli?
 
mtoa mada wewe issue ni samaki tu? watz kwa tumbo bwana tutafika kweli?

Chezea sato smile....!!!!!!!, hebu tembelea JNIA uone ndoo zinavyopokelewa. hata hivyo, sababu ni nyingi sana to consider when you want to travel na kila mmoja ana uhuru wa kufikia maamuzi atumie usafiri upi. myself, fast jet hawajanishawishi tangu nitumie usafiri huo kwa mara ya kwanza na ya mwisho labda nipate dharula ambayo sitapata ticket kwa flight ya precision
 
Tofauti ya laki kwa kutobeba samaki inafaa. Samaki pakia cargo kwenye lory kisha wewe jichane kwenye fastjet kwa bei poa na masharti kibao.
 
ahaaaa.ulikuwa na ndoo ngapi za sato mkuu.mimi nasafiri kwa fuso mie nasafiri na chochote nipendacho
 
ahaaaa.ulikuwa na ndoo ngapi za sato mkuu.mimi nasafiri kwa fuso mie nasafiri na chochote nipendacho

mmmmmmhhhhhh ya kweli hayo, unaijua fuso wewe trafic wa barabarani hawatakuacha mpaka viozee njiani, labda ni ile fuso full kiyoyozi. mie nilikuwa na ndoo moja tu ya 20Kg Fast jet wakanichomolea ikabidi nimkabidhi driver aliyenisindikiza airport arudi nao
 
ahaaaa pole mkuu ila fast jet wameleta ushindani.sema wanasahau ukimwamsha alielala utalala wewe!
 
Boda boda za Kenya Airways
Huwezi kuita Boeing 737-300 bodaboda wewe punguani. Watu tunapanda days in days out na kufika salama wewe unaita bodaboda. Hii nchi imejaa machizi wengi sana. KQ wanahisa PW about 40% nyingine ni za watanzania. Ni aibu ya hali ya juu Mtanzania mwenzio kaanzisha biashara imeshine hadi kuvutia mtaji wa kibiashara kutoka nje wewe unaita bodaboda. PW imeajiri watanzania kibao pale ambao isingekuwepo ungekuwa unagombania nao nafasi chache za ajira zilizopo. Utaishia kuajiriwa maisha yako yote ukiwa na hii mentality ya kiujima ujima. Hongera PW kwa kushusha nauli, hapo mmetusave 50,000 nzima na samaki tunapakia kilo 30. Tutaendelea kuwaunga mkono so long huduma yenu itakuwa poa na tutawaponda mkija na huduma mbovu kama za ATCL. Pia tunashukuru ujio wa Kikwete ooh sorry FASTJET maana ndio imesababisha hawa jamaa kushusha bei
 
Mijitu inawaza kula tu siuamie hotelini.Watu tunangalia gharama za ticket wewe unaangalia samaki
 
Mijitu inawaza kula tu siuamie hotelini.Watu tunangalia gharama za ticket wewe unaangalia samaki

Ulipajuaje hotelini wewe mpaka umepataja kama hukuenda kwa ajili ya kula au ulipelekwa... whatever, katika biashara kuna vivutio vingi tu kwa mteja kuvutika na hivyo sioni tatizo, gharama gani za fast jet hao ukikata leo kama unasafiri kesho utaniambia. kikubwa wameleta ushindani kama nilivyosema na hivyo wengine nao wanaamka na vivutio kibao.
 
teh teh huyu jamaa bana sielewi mada ni samaki au bei za ticket lol

Mkuu mada precision kushusha bei. hiyo samaki ni mzigo ambao kwa mujibu wa sheria za usafiri wa anga kimataifa, abiria unaruhusiwa kuchukua mzigo usiopungua kilogram 30. hawa fast jet hawataki, labda wahusika wa kusimamia sheria hii hapa bongo wamelifumbia macho kwa sababu wanazojua wao
 

Hahahaha tena mimi nimeaply post huko chezeya ajira wewe
 

Mkuu nimeongea na customer care ya Precision Air mda mchache uliopita na majibu waliyonipa ni kwamba.
Kwa sasa wana promotion ya route ya Dar-Mwanza ambayo bei zao ni Tsh 199,000/= (Return ticket) na Tsh 139,000/= (One way ticket). Embu tufafanulie kidogo hizo bei zako umezipata wapi mkuu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…