JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Baada ya kuanza msimu vibaya kwa kupoteza mechi mbili mfululizo, Manchester United imeamka na kuipa Liverpool kipigo cha magoli 2-1 katika mtanange wa Premier League kwenye Uwanja wa Old Trafford.
United haikupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo, ilipata magoli yake kupitia kwa Jadon Sancho na Marcus Rashford dakika ya 16 na 53 huku goli la Liverpool likifungwa na Mohamed Salah dakika ya 81.
Kocha wa Man United, Erik ten Hag aliwaweka benchi Cristiano Ronaldo na Harry Maguire katika mchezo huo.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kucheza mechi tatu bila ushindi wowote msimu huu.