President Barack Obama's message to Kenyans on the March 2013 elections.

President Barack Obama's message to Kenyans on the March 2013 elections.

Ni ujumbe mzito kwa wakenya, wanatakiwa wawe wana urusha kila mara hasa katika kipindi hiki wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Kwa heri.
 
dah hivi kusema 'habari yako' na 'kwa heri' ndo Obama kaongea kiswahili?!!! kwa hiyo heading nilijua hotuba nzima iliyolengwa kwa wakenya kaitoa kwa kiswahili! asante kwa kunilazimisha kutazama sura ya Obama asubuhi subuhi na kuacha shughuli zangu za maana zaidi
 
Lovely message from OBAMA. Kenyans must receive and live it through this elections moments.
 
Tumeshuhudia siasa za demokrasia za marekani kwa ndani na wanaoitisha amani!! amani!! amani!! ndio wakati mwingi nyuma ya pazia hujenga na kupanga miundo mbinu za ghasia na vurugu wakiikwepa minyororo ya ICC. Si ajabu Obama hotuba yake ni utangulizi ya ile papa 'mtakatifu' aliyosalia kuhotubia siku zilizosalia
 
Obama ni mswahili na kiswahili kusema ukweli ni utambulisho wa uafrika wetu.
 
CULTURAL IMPERIALISM,ndio wale akiambiwa kazi nzuri na bosi Mzungu basi siku hiyo halali kwa furaha,lakini same words akiambiwa na bosi mswahili anaona ni kawaida.Utamsikia kwenye pombe hata bosi Mzungu kanikubali kazi zangu......
 
Ni kweli kuwa Obama kuongea maneno mawili hakujakipandisha chart kiswahili, lakini ni kweli pia viongozi wetu hawajaonyesha mwamko unaotakiwa kukienzi, kukikomaza na kukisimamia kiswahili kama lugha inayofaa kuliendeleza taifa kwa mtazamo wa kukifanya kuwa moja ya lugha za kimataifa

Sio viongozi tu hata sie watz wenyewe, ukienda vijijini mtu akizungumza kiswahili badala ya local language anaonekana anaringa na ukija mjini ambako ili mtu aonekane mjanja akiongea kama anahijiwa kwenye chombo cha habari anachanganya na kizungu ili aonekane yupo mahiri. Kichekesho ukimpa kipindi au mada aendeshe kwa kiingereza mtu huyo huyo atahamia kwenye kiswahili kwa kuja na hoja ILI KILA MTU ANIELEWE ITABIDI NIZUNGUMZE NA KISWAHILI (matokeo yake watz wengi hatujui kiswahili kwa ufasaha wala hicho kiingereza), unakuta mtangazaji anatamka Tangia badala ya Tangu, nilikuambiaga, huwaga (hapa wasukuma na wanyamwezi nao wamewaambukiza wengi kwenye matumizi ya "ga")

Naungana na wewe kwa SERIKALI KUHAKIKISHA VYOMBO VYOTE VYA HABARI KAMA VINAENDESHA VIPINDI VYA KISWAHILI BASI KITUMIKE KISWAHILI MOJA KWA MOJA NA WALE WANAOITWA KUHOJIWA WAONGEE KISWAHILI PASIPOKUUNGANISHA NA KIINGEREZA MAANA IMEKUWA NDIO MTINDO SASA UNLESS KAMA ANAEHOJIWA HAJUI KISWAHILI, nina imani kwa kufanya hivi tutakifikisha mbali kiswahili chetu
 
President Obama’s Message to the People of KenyaFebruary 5, 2013

Habari yako.- Over the years, I have been greatly moved by the warmth and spirit – the strength and resolve – of the Kenyan people. And I’ve been grateful for my connection to Kenya, and the way you’ve welcomed me and my family to your beautiful country – from my father’s village in Alego, to bustling Nairobi.

In my visits, I’ve seen your progress. Kenya has lifted people from poverty, built an emerging democracy and civil society, and sustained a spirit of hope in the face of great difficulty. After the turmoil of five years ago, you’ve worked to rebuild communities, reform institutions and pass a new constitution.

Now, Kenya must take the next step in March, with the first national elections under your new constitution.We all know what makes for successful elections. Kenya must reject intimidation and violence, and allow a free and fair vote. Kenyans must resolve disputes in the courts, not in the streets. Above all, the people of Kenya must come together, before and after the election, to carry on the work of building your country.

The choice of who will lead Kenya is up to the Kenyan people. The United States does not endorse any candidate for office, but we do support an election that is peaceful and reflects the will of the people.

This election can be another milestone toward a truly democratic Kenya defined by the rule of law and strong institutions. If you take that step, and reject a path of violence and division, then Kenya can move forward towards prosperity and opportunity that unleashes the extraordinary talents of your people – especially young people. If you continue to move forward, you can build a just Kenya that rejects corruption, and respects the rights and dignity of all Kenyans.

This is a moment for the people of Kenya to come together, instead of tearing apart. If you do, you can show the world that you are not just a member of a tribe or ethnic group, but citizens of a great and proud nation. I can’t imagine a better way to mark the 50th anniversary of Kenyan independence.- And I say to all of you who are willing to walk this path of progress—you will continue to have a strong friend and partner in the United States of America.

-Kwaheri

Kiswahili


RIsala kwa Wananchi wa Kenya

Habari yako.- Kwa miaka mingi, nimeguswa- na- ukarimu na moyo – nguvu na ukakamavu – wa watu wa Kenya.-- Na ninashukuru kwa uhusiano wangu na Kenya, na jinsi mlivyonikaribisha mimi na familia yangu katika nchi yenu nzuri – kutoka Alego, kijiji cha baba yangu, mpaka Nairobi, mji wa harakati nyingi.

Katika ziara zangu, nimeona maendeleo yenu.- Kenya imenyanyua watu kutoka kwa umaskini, imejenga demokrasia inayoibuka na vyama vya kijamii, na kudumisha moyo ya matumaini palipo na changamoto nyingi. Baada ya msukosuko wa miaka mitano iliyopita, mmefanya bidii ya kujenga upya jamii, kufanya mageuzi kwenye taasisi na kupitisha katiba mpya.

Sasa, lazima Kenya ichukue hatua nyingine mwezi wa Machi, kwa uchaguzi wa kwanza wa kitaifa chini ya katiba yenu mpya.Sisi sote tunajua kinachofanikisha uchaguzi.- Lazima Kenya ikatae vitisho na ghasia, na iruhusu kura huru na ya haki.- Lazima Wakenya wasuluhishe migogoro mahakamani, sio barabarani.- Na zaidi ya hayo, lazima wananchi wa Kenya waungane, kabla na baada ya uchaguzi, ili kuendelea na kazi ya kujenga taifa.Chaguo la nani atakayeongoza Kenya ni juu ya wananchi wa Kenya.-

Amerika haiidhinishi mgombea uchaguzi yeyote, lakini tunaunga mkono uchaguzi wa amani na ambao unaashiria matakwa ya wananchi.Uchaguzi huu unaweza kuwa tukio jingine la ufanisi kwa nchi ya Kenya iliyo na demokrasia halisi na inayoendeshwa kwa utawala wa kisheria na taasisi zilizoimarika.- Mkichukua hatua hiyo, na kukataa mkondo wa ghasia na mgawanyiko, basi, Kenya inaweza kusonga mbele na kupata neema na nafasi zitakazokuza vipaji maalum vya wananchi wenu – hasa vijana.-

Mkiendelea kusonga mbele, mnaweza kujenga Kenya inayosimamia usawa na inayokataa ufisadi, na huku ikiheshimu haki na hadhi ya Wakenya wote.Huu ni wakati wa wananchi wa Kenya kuungana pamoja, badala ya kugawanyika.- Mkifanya hivyo, mnaonyesha dunia kwamba nyinyi si jamii ya kikabila tu, bali wananchi wa taifa kuu na lenye fahari.-

Siwezi kufikiria njia bora ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Kenya.- Na ninawaambia nyinyi nyote mlioridhika kufuata njia hii ya maendeleo – mtaendelea kuwa na rafiki na mshirika imara nchini Amerika.-- Kwaheri.
 
Mjaluo ana fujo huyu, haya bhana Kiswahili kinashika chati tu kila kukicha.
 
Lakini huyu rais hajafanya ziara rasmi kwa Kenya tangu awepo madarakani kama rais wa Dunia.
 
Lakini huyu rais hajafanya ziara rasmi kwa Kenya tangu awepo madarakani kama rais wa Dunia.

Anasema yeye ni rais wa marekani na yupo responsible kwa raia wa marekani na si Kenya. Kufanya ziara nchini kenya ni pale atakapopenda tu
 
ni pale atakapopenda au ni uamuzi wa white house,??
 
Hivi wewe ina imaani kabisa kuwa rais wa marekani ni rais wa dunia!. mimi binafsi simchukulii kama rais wangu huyo dicteta namba moja wa dunia
 
Leo nimesikia Obama akiwatakia watu wa Kenya Uchaguzi mwema na wenye fanaka alianza na HABARI ZENU na mwisho kumalizia KWAHERI.Nikajiuliza kumbe wenzetu wa Kenya wapo juu sana kwa lugha ya kiswahili tofauti na ss hapa Bongo ambapo asilimia 100% ni matumizi ya kiswahi sikjawahi kusikia hotuba hata moja ya kiongozi wa nje kwa Tanzania akiweka neno la kiswahili zaidi ya kingereza.Kweli nimekubali Wakenya wapo Juu na lugha ya kiswahili ni yao BIG UP wakenya ss tunalala,ETI bila kingerzea no maendeleo sasa OBAMA kaonyesha kiswahili ni lugha ya Kenya BAKITA VIP!!!!!!

Hujamsikia George Bush alipozuru Tanzania? alisema "Mambo" na mwishowe akasema "asante sana".

Sioni cha ajabu Obama kusema Kiswahili wakati baba'ke ni Mkenya nitaona ajabu kubwa sana kama Obama hajui Kiswahili.
 
Back
Top Bottom