Kiukweli napenda sana utashi alionao Magufuli, msukumo na nguvu zake yaani ni mtu ambaye angekua wa kuskliza ushauri na kuufanyia kazi anaweza akaaipeleka Tanzania mbali sana, tatizo lake (kwa maoni yangu) ni aina ya wale wazee ambao hawaambiwi kitu, nakumbuka enzi zetu tukiwa wadogo, tulikua na aina fulani ya wazazi ambaye angekuwasha kibao kisa umejaribu kumshauri au kujibizana naye kwa lolote.
Hawa wazazi walikua wakali kwamba akiamrisha kitu, unaanza kukifanyia kazi hata kama haujakielewa alichokiamrisha, na ukithubutu hata kuhoji au kuomba maelezo zaidi ili uelewe namna gani anataka uifanye anakuwasha kibao kisa haupo makini kwenye kuskliza maagizo.
Ndivyo huwa naiona kwa Magufuli, ni aina hiyo ya kiongozi, yaani akisema kitu, mnapaswa muendane naye kukifanyia kazi, maaelezo na maagizo zaidi mtayapata huko mbele maana kadiri utakavyomhoji ndio utakua unaharibu, na mbaya zaidi jaribu kumbishia ndio utaona balaa yake.
Angekua kiongozi wa kuskliza ushauri na kukubali kukosolewa panapostahiki, kwa kweli angefaulu pakubwa sana katika kuitoa Tanzania, ila kwa sasa ndio kama hivyo, anajikuta akibishia hata mambo ya kitaalam ya Corona.
Yaani pona na nafuu ya Tanzania ni kwamba wako na upinzani dhaifu sana, na pia Watanzania ni watu wenye asili ya unyonge, sio wabishi na wagomvi, kwa kweli rais Magufuli angewaongoza Wakenya nchi ingeishia kwenye umwagikaji mkubwa wa damu, maana desturi yetu na sisi pia wabishi, tutakuhoji hata kwa ukali wako, tutabanana na wewe kwa hali yoyote ile, tutapumuliana, ukienda chini tunakwenda, ukipandisha tunapanda.....najaribu kuwaza hapa ingekuaje kwa kiongozi wa upinzani Tanzania kujiapisha urais kama alivyofanya Raila Odinga hapa kwetu, halaafu tena mbele ya nyomi, maelfu ya watu.....kwa chini ya uongozi wa Magufuli nahisi jamaa wangevurugana mpaka sisimizi hawangekua salama.
Hitler alikua kiongozi mzuri sana kwenye utendaji, yaani alikua mtu wa matokeo tu, hakutaka uzembe wa aina yoyote na Ujerumani ilikua inapiga hatua sana enzi zake, ila tatizo lake kubwa alikua mbishi sana, hakupenda kukosolewa au kushauriwa, aling'ang'ania hadi dakika za mwisho, wakuu jeshini walijaribu kumshauri asishambulie Urusi, wakajaribu kumshauri asitishe vita, yaani mpaka mabomu yanatua Berlin lakini jamaa king'ang'anizi, aking'ata ameng'ata ng'ata ng'ata, hakutaka kuskliza wala nini, na mpaka dakika za mwisho kwa alivyokua mbishi kajipiga risasi kichwani, hakutaka hata dakika moja asikike kwamba amekubali yaishe, kaamua bora ajifie mbali. Ujerumani ikasambaratishwa na kuwa kama shamba....
Ndio hili naliona kwa Tanzania kwenye haya ya Corona, yaani pale Magufuli alisema hatofunga chochote, walahi msitegemee aje kubadilisha hiyo kauli hata mkifa 50%, hehehehe!!! Hivyo haya makelele sijui mara USA, mara WHO, mara CDC hakuna atakayembadilisha kwa hilo, na msitegemee hata huyo Mbowe hana usemi wowote utakaomfanya Magufuli abadilishe msimamo, tafuteni mbinu zingine za kuishi na kirusi lakini msitegemee rais alegeze msimamo wowote.