Anafaamika kwa wengi kama dikteta aliyeitawala zaire,wengine humuona kama mtu katili
Lakini mbali na kuwa rais,mobutu alikua na maisha binafsi ,moja ya watu waliopata kumfahamu mobutu kama mtu na sio rais tu ni mfanyakazi wake wa ndani aliyeitwa Ayo kayitani
Alifanya kazi kwa mobutu kama mlezi wa watoto wa mobutu wakati mobutu akiwa na mkewe wa kwanza aliyeitwa marie anttoinette
Hivi sasa ana umri zaidi ya miaka 65, alianza kufanya kazi kwa mobutu akiwa na umri wa miaka 15 tu,pale ambapo mobutu alienda kuwatembelea wazazi wa mkewe na kumuona binti huyu ambaye aliishi mtaa mmoja na wazazi wa mke wa mobutu,
Mobutu alipomuona akasema"mke wangu akija atamchukua"
Ayo kayitani alichukuliwa na kwenda kuishi mount ngaliema yalipokuepo makazi ya rais wa zaire
Alipofika nyumbani kwa mobutu alikuta mobutu ana watoto 6 tayari ambao ni manda,niwa,malu,konga ,diako na djamba. Wengine wakubwa walikua ulaya tayari(mobutu alipenda watoto wake waishi nje ya Afrika)
Ayo aliwalea watoto watatu wa mobutu ambao ni djamba,diako na mdogo kuliko wote kongolu(niliyemzungumzia juzi)
Ayo anasema hata katika maisha binafsi,mobutu aliyeitawala zaire toka november 24 1965 alikua mtu wa hasira mno na mwenye wivu kwa mkewe
Mobutu alikua akimpa kipigo kizito mkewe kutokana na wivu wa kimapenzi
Ayo anadai .jioni moja walikuwa sebuleni,mobutu akaenda chumbani na kumuacha na mkewe sebuleni wakiangalia movie
Baadae mke wa mobutu pia akaenda kulala na mfanyakazi wa ndani akaenda chumbani
Baada ya muda akawa anasikia mke wa mobutu akipiga yowe ,aliogopa sana
Siku iliyofuata asubuhi mobutu alienda kazini,ndipo mfanyakazi huyo akaingia chumba cha mobutu na kumkuta mke wa mobutu amevimba mwili mzima hivo akamtafutia miti shamba na kumkanda
MOBUTU BAADA YA KUTOKA OFISINI
Kwa mujibu wa Ayo ,mobutu kila alipotoka kazini alipenda kwenda sebuleni,anavua kofia yake na kuiweka nyuma ya mlango kwenye kiti
Arafu anaangalia TV (mara nyingi anajiona matukio yake mwenyewe)
Na kusoma magazeti
CHAKULA
mobutu alipenda kula nyama za mbugani pamoja na pondu(kisamvu)
Japo alikula kidogo mno kwa kuogopa kunenepa.
Na hakupenda vyakula vya kisasa hasa kuku wa kutoka ulaya waliogandishwa
USHIRIKINA
ayo anasema hakuwahi kumuona mobutu hata siku moja anaumwa
Na mobutu hakuwahi kwenda kanisani wakati ayo akifanya kazi hapo (alipozeeka alianza kwenda)
Siku moja Ayo anasema aliingia chumbani kwa mobutu kufanya usafi,chini ya mto alikumbana na kitu cha kushangaza na kumuogopesha,kilichofanana na kioo
Alimuita mke wa mobutu na kumuonesha,mke wa mobutu akakichukua na alikataa kusema ni kitu gani
Pia kwa mujibu wa pierre jansen,mpwa wa mobutu,mobutu aliwahi kuchoma moto furniture zake za ndani zote kutokana na kuambiwa na mganga zina mapepo
WIVU WA MOBUTU TENA
baada ya kifo cha mkewe wa kwanza,mobutu alioa mchepuko wake wa muda mrefu aliyeitwa bobi ladawa (ilitakiwa aolewe mchepuko aliyeitwa mama 41 lakini siku chache kabla ya harusi akapofuka)
Bobi la dawa aliolewa mwaka 1980 (mobutu alijaribu kumualika papa alipotembelea kinshasa ili awe mgeni rasmi ,papa akakataa)
Sasa kwenye serikali ya mobutu kuna jamaa aliyeitwa nguza karl bond alikuwa waziri
Huyu jamaa alimtongoza mke wa mobutu (haijulikani kama alikubaliwa)
Mobutu alivojua alimkamata nguza na kutaka kumuua kwa risasi badae akaacha na kuagiza nguza afanywe hanithi
Nguza aliingiziwa vyuma kwenye tundu la mkojo na kuwekewa upepo kwenye dushe ,kitu kilichofanya inasemekana awe hanithi na wanadai kuwa hii ilichangia kifo cha huyu jamaa miaka kama 6 au 10 iliyopita
MOBUTU NA WANAWE
mobutu alikuwa mzazi aliyewapenda wanae na alijaribu sana kuwa karibu nao
Aliwahi kuwapeleka paris huko disneyland katika moja ya likizo
Alikuwa mzazi aliyeongea vizuri na wanae
Walipotoka shule alipiga nao stori kama mzazi yoyote tu kwa kuwauliza
"Vipi shule mnaendeleaje" na kadhalika
Alimuandaaa nyiwa awe rais lakini nyiwa alikufa
.watoto wote wa mobutu wa mke wa kwanza walikufa
Mobutu aliwazika watatu waliofatana kufa
UTAJIRI
mobutu aliwahi kuripotiwa kuwa na mali za dora za kimarekani billion 15
Lakini katika moja ya interview anadai ana dora million 15 tu uswizi.yule reporter akauliza mbona nyingi ?mobutu akajibu "hiko ni nini kwa mtu niliyekuwa rais wa nchi kubwa kama hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa "
Pia mobutu alimiliki majumba 11 zaire,ufaransa,uswizi,ubelgiji,rabat ,marakesh na cassabranka moroko ,Afrika ya kusini na kadhalika
NB
Mobutu alijijenga kanisa nyumbani kwake chini ya kanisa akamzika mkewe na watoto
Lakini baada ya kutolewa madarakani. Wanajeshi walipasua makaburi hayo na kuiba vitu vya thamani ambavyo mobutu alimzika navyo mkewe kama dhahabu nk