mjanja wa kijiji
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 1,582
- 4,378
kumbe ilikuwa rahisi kumvamia kama alikuwa anaondoka na funguo za maghala ya siraha unasubiri akisafiri unafanya yako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio Kuna wengine hawajaionaUmerudia hii habari mkuu ni ya mwaka jana
Licha ya pesa na mamlaka ila hakuwa happy muda wote kama watu wanavyodhani________________________________________
Huyu bwana alikuwa tajiri wa kutupa ndani ya umaskini wa kunuka. Alitumia muda mwingi hapa duniani kula bata. Na alikula kwelikweli. Alikuwa na Meli ya kifahari maalum kwa kulia bata. Aliita Kamanyola. Ilimzungusha ndani ya mto Congo akila na kunywa vya kutoka Ulaya.
Alijenga Kasri kijijini kwake Gbadolite lenye vyumba 100 na hoteli ya kitalii ya nyota 5 iliyoitwa Motel Nzekele. Kazi kubwa zilizofanyika katika kasri hilo ilikuwa ni anasa kwa kwenda mbele.
Moja ya anasa kufuru kabisa ni ile ndoa ya binti yake Yakpwa mwaka 1992. Shela yake tu iligharimu dola za Kimarekani 70,000 sawa na (164,500,000) fedha taslimu za Kitanzania. Keki ya harusi na mapambo viligharimu dola za Kimarekani 65,000 sawa na (152,750,000) za Bongo, cheni na hereni viligharimu dola za kimarekani milioni 3 ambazo ni sawa na bilioni saba na milioni hamsini fedha taslimu za Magufuli. Na katika harusi hiyo zaidi ya wageni 2500 walikula mlo wa lobster (Kama hujawahi kula lobster jaribu kutembelea cape town fish market pale msasani utoe tongotongo) na mayai ya samaki na kishushio cha shampeni nyekundu na mvinyo kutoka Ufaransa kwa ndege ya kukodi.
Wakati wa ziara zake za majimboni aliandaliwa vibinti vibichi kabisa (bikra safi kama sufi) ili kumpa raha. Alisumbua sana enzi zake huyu jamaa. Alikuwa anakwenda kunyoa Ubelgiji na watoto wake walisoma Ufaransa na kurudi Kongo kila wikendi. Alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake, uwanja wenye uwezo wa kutua ndege aina ya Concordi, ambazo mara kwa mara alizikodi kwenda shopping Paris na Uholanzi. Akiingia shopping Hapana lilia lia kuomba punguzo la bei.
Aliwahamasisha viongozi wake kuiba kwa akili. Aliwaambia polisi na wanajeshi hawana akili kudai mshahara na wakati wanabunduki.
Alikuwa na nyumba ya kifahari katikati ya jiji la Paris, hekalu la vyumba 32 Uswisi, Kasri la adabu huko Uhispania na nyumba ya vyumba 30 huko Lausanne. Alipiga marufuku mwanasiasa yeyote kutamkwa wala kuonekana kwenye TV zaidi yake.
Mke wake wa kwanza Maria Anttoinette alikufa baada ya kupigwa na Mobutu akiwa mja mzito. Baada ya kifo, Mobutu alimuoa Bobi Ladawa, mchepuko wake wa muda mrefu. Ilikuwa amuoe mama 41, mchepuko wake wa siku nyingi lakini siku chache kabla ya harusi mama 41 alipofuka macho. Ndumba? Sijui. Lakini wakati wa ndoa yake na Bobi, Mobutu alimualika papa Paul wa II alipotembelea Kinshasa ili awe mgeni rasmi, papa alikataa. Bobi Ladawa alikuwa na pacha wake waliofanana sana , tena mke wa mtu lakini Mobutu alimpenda na kumuoa pia. Pacha akaacha mume wake akiwa na mtoto mmoja na kufuata mdundiko. Mume wa huyo pacha alifariki miaka ya 90.
Mobutu alimuhasi Karl Bond Nguza, waziri wake wa mambo ya nje baada ya kuskia jamaa alimtongoza mke wa Mobutu. Hapo kabla alitaka kumuua kwa risasi ila akaghairi. Akaamua kumhasi. Wahenga walisema ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga. Mobutu alikufa kwa kansa iliyoutafuna uume wake yaani tezi dume.
Pamoja na kwamba Mobutu aliuchukia ukristo alijenga kanisa nyumbani kwake na kuwazika mke na watoto wake.Kwa nini alichukia ukristo? Akiwa anajiandaa kwa mtihani wa darasa la 12, alitoroka seminari na kwenda kumuona mchumba wake. Wakati anarudi mapadre walimkamata na adhabu yake iliamuriwa asiende kidato cha tano na badala yake apelekwe jeshini. Mobutu aliumia sana kutokwenda kidato cha tano. Aliposhika dola aliwapiga marufuku mapadri wa Zaire kubatiza watoto kwa majina ya kizungu.
Mobutu alikuwa ni mtu wa visasi. Alimfanyia kitu kibaya sana Pierre Mulele ambaye alikuwa rafiki wa Lumumba. Baada ya Lumumba kufariki Mulele alikimbimbilia Brazzaville. Mobutu alimtumia ujumbe kumuomba arudi nyumbani ampe nafasi ya uongozi. Alivyorudi tu Mobutu alimkamata Mulele na kuanza kumkata kidole kimoja baada ya kingine mpaka akafa.
Nyerere, Kaunda na Mobutu waliunda Mulungushi Club ili kujadili Ukombozi wa Afrika miaka ya sabini. Lakini kila walilojadili Mobutu alivujisha siri kwa wafaransa. Mwalimu akaona ujinga, akaachana naye, club ikafa.
Lakini pia Nyerere alivyomwambia Mobutu anaongeza nchi kidikteta, Mobutu alimwambia Nyerere kwamba Zaire si Tanzania kama haamini wabadilishane nchi na kama atakubali kuwa Rais wa Zaire hatamaliza hata miezi mitatu, atapinduliwa na mwanamke.
Alimtia jela hayati Fránco Luambo Màkiadi kwa kumkosoa kupitia uimbaji wake. Akampa shariti la kutumia akili yake kutafuta kitu kitakachomfurahisha ili amwachie huru. Frànco akamtungia kibao cha kumfagilia kilichojulikana kama Candidat na Bisso Mobutu. Mobutu alifurahi mno, akamtoa kifungoni na kumfanyia Frànco pati ya kufa mtu Ikulu kisha kumwachia huru.
Miaka miwili kabla ya kifo chake alijigamba kuwa tangu azaliwe hakuwahi kuugua kiasi cha kulazwa hospitali. Alipougua hakupona.
Mobutu alikuwa mwoga sana, alipokuwa anasafiri kwenda nje ya nchi, aliondoka na waziri wa ulinzi, mkuu wa majeshi na funguo za maghala ya silaha lazima awe nazo yeye kwenye briefcase yake.
Huyu bwana aliamini sana katika mambo ya ushirikina (ndumba). Aliajiri waganga 100 Ikulu. Miaka ya 1975 alikodi wachawi na waganga wote wa Zaire kwenda Ujerumani kwenye mechi kuwanga ili timu ishinde. Walipigwa tisa kwa nunge.
Mobutu alipendwa sana na nchi za Magharibi kwa sababu alionekana kusimamia maslahi yao kwa kupambana na ukomunisti. Alimuandaa mwanaye wa kwanza Nyiwa ili kumrithi lakini Nyiwa alikufa kwa UKIMWI mwaka 1994. Ukomunist ulipokufa walimfyekelea kule kama maganda ya ndizi. Alifia Morocco mwaka 1997 na kuzikwa na watu wasiozidi 6 pamoja na utajiri wote aliokuwa nao.
C&P (Comred Mbwana Camerôò Allyamtu)
Jonas savimbi alijua lugha 7 ikiwemo english,french,kileno,nkAiseee kwa hiyo jamaa alizikwa ki mbwa,na yule jamaa wa angola mwenye phd aliyekufa kifala ,wanamuita savimbi naye alipata tabu sana ila niliambia alikuwa na akari sana darasani
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah mkuu kanungila ,za siku ?Huyu jamaa unayemzungumzia si mjombaake lucas mobutu
Walikua na ndumba kinomaHuyu jamaa namkubali sana. Kuna mtu hapa JF anaitwa lucas mobutu sijui ni ndugu yake maana anamjua kinoma
HahahahahahahaAlisumbua sana enzi zake na kwa kuonesha yeye ni mwanaume alibadili jina la nchi husika kutoka belgian congo kwenda Zaire ya Mobutu.
Bado wapo hai?H
Hawa mapacha wanaishi Morocco na wanapewa hadhi ya kifalme.