#COVID19 President Samia hires Tony Blair to help in the fight against COVID-19, and rebuild the country's reputation

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Una kibarua kizito sana!

Yani wewe Magufuli alikuchapa akiwa hai na bado anakuchapa akiwa mfu
 
 
Chige ni mbumbumbu anaeishi na hasira kwa hayati Magufuli!

Kwake huwa anaumia sana akiona Magufuli anapewa credit kwa jambo lolote lile
 
Hongera sana kwa Rais Samia
Ukweli hao jamaa wametuzidi sana maarifa yao yatatusaidia
Aise hivi ni kweli tunakubali kuwa sisi tunamaarifa madogo. Yaani uko tayari mtu wa nje aje akulelee watoto wako uliozaa kwa raha zako. Basi sawa Mungu anihurumie mimi.
 
Tunaojua Blair kazi iliyomleta hapa tuliandika eatu wnaqeza kujua identity zetu. Ngoja tumyamaze.
Kwa kweli ngoja tunyamaze tu. Tukisema sana Tutatumia bure wao waendelee kuishi. Lakini ipo siku
 
Kwamba nchi nzima ilimuelewa sana JPM kwenye chanjo?
Unamaanisha nini unaposema nchi mzima?!

Waliomwelewa ni Wafuasi wake, and of course wafuasi wake wapo nchi nzima bila kujali distribution yake kwa kila eneo. So, ana wafuasi nchi nzima lakini sio watu wote nchini ni wafuasi wake!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Una kibarua kizito sana!

Yani wewe Magufuli alikuchapa akiwa hai na bado anakuchapa akiwa mfu
Kibarua kizito zaidi ya hicho ulichojipa cha kutetea kila alichofanya hata kama ni cha kijinga!! Halafu siku hizi umejiongezea kingine... ukiona naongea jambo positive kuhusu Samia, unaumia huku ukishindwa tu kuweka wazi kinachosukuma maumivu yako!

Halafu ajabu yako wewe... Hivi unataka mkishatoa nyuzi na posts za kumsifia, ndo unataka soooote tuungane na nyinyi kumsifia hata kama anasifiwa kwa jambo la kijinga, au?

Oneni sasa... serikali hatimae inalazimika kuleta the so-called Mabeberu kuweka sawa maforofyongo ya Mungu Mtu wenu mnayetaka asikoselewe!!! Au unataka kusema wewe unafahamu zaidi uhalisia kuliko Samia na serikali yake?

Narudia kama nilivyowahi kukuambia mara kadhaa... POLE SANA!!!

Nyerere kafanya mambo mengi sana nchi hii, na amefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita lakini hadi leo watu wanamkosoa!! Sasa utaendelea kuumia sana ikiwa kila anapopigwa vitofa JPM, basi unaingia kwa sababu tu unataka awe anasifiwa tu!!!
 
Acheni ujinga,kila siku imekuwa mwendazake,mwendazake.Kamfufueni mumwadhibu! Stupid propaganda
 

Tanzania is reborn! Unachekesha sana mkuu…kwani ilikuwa imekufa?!

Kwetu sisi ilikuwa imefufuliwa…tulifunguliwa macho..tuliambiwa mchana kweupe na mzee wetu JPM kwamba sisi tumefanywa shamba la bibi huu ni ukweli usiopingika…we knew way back lakini habari zilikuwa zinasemwa chinichini..watu wanajichotea madini na wanyama wanavyotaka…..kwa hio kukatazwa kutufanya shamba la bibi Tanzania ndio imepoteza reputation…sasa hv wana hire institution kwamba we are back on business….uuuwiiiiiiiii #inJPMvoice..

Kwahio inakuwa reborn tena mkuu ili warudi…WAPI?!

Kuhusu pandemic JPM aliomba taasisi za nje kuondolea madeni nchi maskini na sio kuwapa pesa kuzidi kuwadidimiza kwenye madeni…sasa sisi ndio tuna hire ilitupate pesa…wakati survival rate ya huu ugonjwa ni 99%…huu ugonjwa upo tutaishi nao…tuchape kazi, tulime tuuze mazao yetu, tufungue viwanda vyetu, Tony Blair tumuajiri atutafutie masoko ya bidhaa zetu
 
British Standards !
 
Yani nimesoma hiyo comment yake nikatamano angekuwa karibu nianze na kofi upuuzi mkubwa sijui viumbe wengine wanamaruani gani?

Yaani ndio maana mikoa yao hadi sebule zimeuzwa kwa kweli kama pangekuwa na namna wachaga tungetengwa na hizi nyang'au za pwani.
Nchi yetu tuna bariki na kutakasa uwizi eti kisa aliyekuwepo alikuwa msimamizi sahihi wa rasilimali. Nimegundua jambo jamii za pwani zina inferiority kubwa sana to the so called whites shenzi type.
 
Nahizunika sana kwa baadhi ya replies. To me Magufuli ataendelea kuwa bora daima
Magufuli alikuwa ni mtu mwenye independent mind na results-oriented. Hii tabia ya ombaomba, na bembeleza bembeleza (kutafuta kibaba) hakuwa nayo, jambo ambalo ndilo lililonivutia kwenye utendaji wake! Hakuwa mtu perfect kwa watu wote, lakini tutamkumbuka kwa mema aliyoifanyia nchi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unaumia sana mkuu!

Yani unatumia nguvu nyingi sana hapa Jf kwa ajili ya kumshusha thamani Jpm!

Nakushauri uongeze juhudi maana kazi unayo!

Wewe uko tayari kutetea ovu lolote la awamu hii ya Samia na yote unafikiri watu wakiongelea uovu wa awamu hii unahisi wanampa credit Magu!

Hahahha una kazi nzito sana
 
Unamaanisha nini unaposema nchi mzima?!

Waliomwelewa ni Wafuasi wake, and of course wafuasi wake wapo nchi nzima bila kujali distribution yake kwa kila eneo. So, ana wafuasi nchi nzima lakini sio watu wote nchini ni wafuasi wake!
Basi Magu anawafuasi wengi sana nchi hii. Imagine kati ya dozi milioni 1 zilizoletwa ni dozi hata nusu hazijaisha takriban miezi 3 sasa!

Hivi shida ni nini hebu twambie!

Yani haters wa Magu mmeshindwa kuwapiku wafuasi wake walau kwa kushambulia zile chanjo milioni tu zilizododa kule maabara?
 
Same old story...

Nimeuliza hapa mara kadhaa lakini sijajibiwa, labda unisaidie wewe!!

Sote tumeona alivyo-deal na Accacia, tena cha ajabu ali-deal na makinikia ambayo yana-account only 30% ya mapato ya Acacia. Je, unataka kusema ni Acacia peke yake ndio waliokuwa wanaiibia Tanzania?
Maajabu haya...

Umekopa pesa kwa sababu nyingine, halafu unataka usamehewe madeni kwa sababu nyingine?

Na kama kweli aliamini madeni yanazidi kudidimiza, kwanini aliendelea kukopa huku akiaminisha watu kwamba ni pesa za ndani?! Magu alikopa Standard Chartered Bank na Credit Suisse!

Hivi mnaelewa maana ya kukopa kwenye private financial institutions?!

Magu alijaa janja janja tu! Kama vile kujifanya kuwaponda mabeberu huku akiaminisha wafuasi wake kwamba hatuwahitaji, lakini anapita mlango wa nyuma anapokea misaada ya hao hao mabeberu, huku akienda kukopa kwa hao hao mabeberu!!
 
Chige hawezi kukuelewa yeye akili zake ni kama za mabavicha wengine wanaohisi maendeleo yao yataletwa na mzungu
 
Ni majitu majinga aina ya hawa kina Chige!

Fikiria Magu bado anawachapa hata baada ya kufa
Tumekuwa taifa la vijana wajinga waliojaa propaganda bila kuwa na uwezo wa kufikiri kwa kina.Ukitazama nyuzi nyingi tunajadili mtu badala ya issues.Vyuo siku hz vinazalisha hopeless imbeciles wengi .
 
Unaona sasa! Kwani aliyesema Blair kaletwa ku-rebuild reputation ni mimi?

Una-rebuild vipi kitu ambacho kilikuwa intact?

Na kama hakikuwa intact nani kasababisha kutokuwa intact?

Na kama reoutation iliondoka, lazima irejeshwe!!

Btw, huo uovu ninaotetea ni upi?!

Narudia, mwambieni mleta mada aweke ripoti kamili! Tony Blair Institute hawawezi kuchukua pesa kwa Tanzania!! Narudia, ikiwa taasisi iliwekwa kitimoto kwa kuchukua pesa kwa Saudi Arabia nchi ambayo haina shida, kwa akili yako unatarajia watakuwa stupid wachukue pesa kwa nchi maskini?

And FYI, Tanzania ni moja tu kati ya nchi zaidi ya 10 za Afrika ambako TBI wanafanya kazi! Najia hii habari kwanu chungu kwa sababu kwa mara nyingine inathibitisha Magu aliivuruga nchi!!

Kuhusu Samia, YEEEEEES, endelea KUUMIA lakini akifanya jambo zuri tutamuunga mkono, especially anapofanya jambo la kurekebisha mafyorofyongo ya Magu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…