Unaamini wafuasi wa JPM wanaweza kufanya lolote kwa sasa?
Kwani si ndo mnaoongoza kutetea YOOOOTE aliyoyaacha JPM hata kama ni ya kijinga!!
Ubaya ni kuwa, mnalazimisha nchi yenye milk teeth iwe sawa na nchi yenye zaidi ya miaka 300 ya uhuru na civilization, tena kwa kuruka hatua za ukuaji, tutoke kwenye utumwa, tuingie kwenye capitalism, tutaendelea kuwa watumwa wa kisasa wa ndani na nje ya mipaka milele amina, na MSOGA theor is making sure of that.
Ndivyo mnavyodanganyana kwa sababu Mungu Mtu wenu aliwadanganya hawezi kuwa mtumwa wa mabeberu wakati from Day 1 anaingia madarakani, hadi siku zake za kuishi hapa duniani zinaisha, HAKUWAHI HATA MARA MOJA KUKATAA CHOCHOTE TOKA KWA MABEBERU!!
Nchi iliendelea kupokea misaada toka kwa mabeberu ikiwa hadi misaada ya kijinga kabisa kama vile kujengewa vyoo!!
Nchi iliendelea kunufaika na shughuli za NGO's za mabeberu! Kwahiyo kauli kama hizo, danganyaneni wenyewe, au tafuta watu wa kuwaambia lakini sio mimi!
Samahani, Julius, Ben na John ndio maraisi waliokuwa na mwelekeo halisi, waliojua tutokapo na tupaswapo kuwa, kama ulihitaji kujua mimi ni wa muelekeo gani, basi ni huo na falsafa za hao wajuvi ni bora sana kuwahi kuwepo hapa Tanganyika kwa maoni yangu.
Sina haja ya kuwajadili hao wengine, labda uniambie wewe what's so special alichofanya JPM?! Ametuwekea mwelekeo upi?
Mwelekeo wa kuua na kufunga watu waliokuwa wanampinga?
Mwelekeo ya kutuletea watu kama akina Sabaya ambao walitumika kunyanyasa wapinzani huku wakifanya ujambazi?!
Ametuwekea mwelekeo upi hasa?!
Hivi una habari hata ile mipago aliyoifanya ni vision ya waliomtangulia, huku vision yake yeye ikiwa ni ununuzi wa ndege ambayo ni mradi wa hovyo!! Maybe Mradi wa Bwawa la Nyerere lakini wenzake pia walitaka kuwekeza huko lakini walipoona kuna gas ya kutosha, wakaona haina haja!!
Ni mwelekeo upi hasa unaosema wewe?
SGR fine lakini nao ni mwelekeo ambao uliandaliwa na waliomtangulia na yeye akaja kufanikisha tu!! Tofauti pekee, waliomtangulia walitaka kuifanya unelectrified SGR with Chinese Company being ndie mjenzi mwenyewe, yeye akaamua iwe electrified na kumpa tenda Mturuki lakini maandalizi yalianza long ago kabla hajawa waziri!!
Sasa huo mwelekeo ambao ni very special ni upi hasa?!
Btw, hivi unafahamu kwamba rushwa kubwa kubwa zote zilizowahi kutikisa taifa hili zimetokea wakati wa Mkapa unayedai eti ndo miongoni mwa walioweka mwelekeo!! Si ndo Mkapa huyo huyo ndie aliuza karibu mashirika yote ya umma, hadi TANESCO kabla haijarudi serikalini?
Lakini pamoja na madudu hayo ya Mkapa katu usimlinganishe The Late Magufuli kwa sababu Mkapa was far more visionary than Magufuli!!