Hii nchi nadhani nadhani tatizo kubwa ni elimu yetu mbovu, hivi kazi ya Balozi nje ya nchi ni ipi? Tuna Balozi wa kudumu UN na tuna waziri wa mambo ya nje, hakuna haha ya kuhire institute ya Blair kujenga reputation hewa iliyopotea. Hivi hiyo reputation iliyopotea kimataifa ni ipi?
Pia ni low IQ ya Hali ya juu kuhire Blair institute Kwa sababu ya Tanzania ku access COVID 19 vaccines, ni utopolo Kwa ufupi maana tuna wizara ya afya, tuna MSD ambayo imekuwa ikiagiza na kusambaza madawa nchini na mbaya zaidi tuna kitengo na watalaam wa tiba ya magonjwa ya mlipuko yaani hao wote hawana uwezo w ku access COVID 19 vaccines?
Tony Blair ni mfanya biashara anajua Samia world bank wame approve pesa za COVID 19 , hivyo yeye anawaza ile pesa kwenda kwenye institute yake na kampata mama yenu mpendwa, hata USA na mataifa Yana sukuma kila nchi za Dunia ya tatu wapate pesa kutoka world bank ili in return pesa zote zinarudi kwao kw ajiri ya kupata chanjo za corona by force , sisi kama nchi tutabakiwa na kulipa loans na pesa itakuwa imekwenda kwao, kwahiyo ni lazima uwe kiongozi wa kutafakari haya mambo Kwa kina sio kuitikia Kwa kila jambo.
Mataifa hayo wanajua Tanzania population inskuwa , mil60 kuchanjwa wote maana yake serikali itshitaji si chini ya trilion 3 , so world bank na IMF na WHO hawaoni shida ku approve pesa Kwa ajiri ya chanjo Kwa sababu immediately zikiwa approved astrazeneca, Pfizer, Johnson ndo hao wata supply hizo dawa, hivo WHO Yuko pale kutoa mapande kama yakina zidane kwao, so go against ndipo utaona Cha moto. Tujiulize tu ni proposal ngapi ziko pending world bank kutoka Tanzania au nchi zingine za Dunia ya tatu kuomba fedha za kuanzisha viwanda ili kujikwamue na kuweka vijana wetu kwenye ajira hazijawa approved? Ok good let's focus on COVID-19, tuko million 60, tuliochanjwa laki 3 , waliokufa hawafiki hata elfu moja, hata tunapoongea hapa Bado mil60 yote hawako mahospitalini wakipumulia machine na haitatokea , hii force kutoka majuu sio Kwa ajili ya kuzuia corona na Kwa ajili ya kuuza vaccines, hatukatai tusichanjwe lakini kama taifa tuangalie priority zetu na agenda zetu kwanza, agenda ya taifa hili sio kuhire institute kuondoa reputation hewa, agenda yetu ni maendeleo na kuondoa umasikini uliokithiri Tanzania, vijana wapate ajira wajiingizie kipato na sio mengine .