jamaa yako nani? Pascal hawezi kwenda maana yeye ni CCM...
Pascal tupe
Pascal achana na hizo za Trump kwani hao hawana Demokrasia kama yetu cha muhimu hebu leta za Mlimani City vipi jamaa yetu kapenya?
Hili ni bandiko la Trump, za Mlimani City tukutanie kule, tujifunze kuheshimu mabandiko ya watu kwa kujadili mada iliyo mezani, mada hapa ni bunge la wenzetu linatimiza role yake ya kuisimamia serikali kwa kutaka kumuwajibisha rais, swali hapa jee Bunge letu hili la Ndugai lingeweza?,
mfano mzuri kabisa ni katiba imeruhusu mikutano ya siasa nchi nzima, rais Magufuli kazuia mikutano hiyo kinyume cha katiba, chama makini cha upinzani Chadema kipo bungeni, lenye uwezo wa kulishughulikia hili, kule kwenye bungeni kwenye uwezo, hawashughuliki, Chadema walitaka kulishughulikia kwa kufanya mikutano na maandamano nchi nzima as if uvunjivu wa katiba unashughulikiwa kwa mikutano na maandamano!,
juzi hapa siku ya Uhuru, Mwenyekiti Mbowe, anapiga magoti kwa Magufuli kumuomba suluhu ya mazungumzo wakae mezani wazungumze!, haki ni right sio favour, haiombwi na hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa na ikibidi inapiganiwa!. kuhusu hili Somo hili la Trump ni somo kubwa kwa Bunge letu na wabunge wetu wakiwemo wabunge mahiri na machachari kama Zitto na umachachari wa kwenye twitter lakini mule Bungeni kwenye the right forum yuko kimya!.
Siku nimekutana na Zitto mahali, nilimpa za uso kuhusu hili by telling him to his face
Wanabodi, Japo bandiko hili liko addressed kwa Mhe. Zitto, lakini hoja zake ni kwa Wapinzani wote, namuelekezea Zitto Kabwe kwa sababu kwa maoni yangu ndio mpinzani pekee kwa sasa anayeweza kusimama na rais Magufuli 2020, na Magufuli akahisi kijoto joto japo kwa mbali. Ni kwa muda mrefu...
p