President Trump has been Impeached after the House of Representatives voted in favour of charging him with abuse of power and obstruction of Congress

President Trump has been Impeached after the House of Representatives voted in favour of charging him with abuse of power and obstruction of Congress

jamaa yako nani? Pascal hawezi kwenda maana yeye ni CCM...

Pascal na wenzie walisema pandikizi lipewe ili pawe na uhai CDM na bila hivyo chama kinakufa sasa Mbowe kachaguliwa sijui huko kufa kupo stage gani sasa hivi ndicho ninachomuuliza ingawa yeye hujitanabaisha kuwa hana chama kama mimi nilivyo
 
Huhu ni CCM, mwongo mkubwa. Inawezekana mwanzoni hakuwa CCM, lkn kwa vile msukuma Jiwe (ingawaje per se siyo msukuma) basi upepo umemkumba wa usukumanisation
 
Leo nimejifunza Impeachment.. 😅 😅 😍
To impeach ni kuwa amepatikana kuwa alivuja katiba. Je aondolewe? Wanakwenda kupiga kura. Kwa vile wapiga kura wengi ni republicans, basi he will survive the vote!
1576725955440.png
 
Hili swala limekuwa la vyama zaidi hivyo Trump ataendelea kuwa Rais maana Senate itapingana na maamuzi ya HOR...

Ndio Uzuri wa kuwa na Uongozi kwenye Moja wapo. Angekuwa hana uongozi wa Senate zamani sana wangemtoa Trump

Sent using Jamii Forums mobile app

Siyo kweli; wakati wa impeachment ya Clinton mwaka 1998, Congress na Senate zilikuwa chini ya Republican na bado hawakumtoa. Mwaka 1974 wakati wa impeachment ya Nixon, iwapo senators wote 42 wa republican wangesimama kumtetea Nixon, bado asingeondolewa lakini hao hao ndio waliomwambia Nixon kuwa amevunja sheria itabidi aondolewe, ndiyo maana Nixon akajiuzulu mapema. Wakati huo wanasiasa wa Marekani wote walikuwa na adui mmoja, yaani ukomunist, kwa hiyo walikuwa wanaedesha siasa zao za ndani kwa kufuata ukweli na sheria sana. Kuanzia Gingrich achafue mfumo wa kisiasa mwaka 1994, huku kukiwa hakuna hofu ya ukomusit tena, wamarekani walianza siasa za kugombana wenyewe kwa wenyewe kufuata itikadi za vyama bila hata kuangalia ukweli na sheria ziasemaje. Wote wanaomtetea Trump leo wanafanya hivyo tu kwa sababu ni wa chama chao, ingawa wanaona ukweli wa wazi wazi kuliko ule wa Benghazi au wa Fire na Fury wakati wa utawala wa Obama.

Nadhani utakuwa umewaona jinsi watetezi wa Republican wanavyowayawaya hovyo hovyo bila mantiki yoyote: Kwa mfano wanataka Whistle blower ajulikane, wakati yeye alichofanya ni kutoa tahadhali tu kuwa kuna jambo baya lifuatiliane, na wala kwenye list ya ushahidi hakuna hata neno moja la huyo Whistle blower lakini wao wameng'ang'ania huko huko na kuacha ushahidi wote uliotolewa na viongozi wa serikali waliohusika. Vile vile wanalalamika kuwa utaratibu siyo wa haki wakati Kamati zote za Congress zina wajumbe waliochaguliwa na vyama vyao, halafu utaratibu unaofuatwa ni ule uliowekwa na wao haoa hao Republican wakati walipokuwa majority.

Trump aliwahi kusema hivi kuhusu Obama hivi

Leo maneno yake yamemrudia mwenyewe!
 
Pascal tupe
Pascal achana na hizo za Trump kwani hao hawana Demokrasia kama yetu cha muhimu hebu leta za Mlimani City vipi jamaa yetu kapenya?
Hili ni bandiko la Trump, za Mlimani City tukutanie kule, tujifunze kuheshimu mabandiko ya watu kwa kujadili mada iliyo mezani, mada hapa ni bunge la wenzetu linatimiza role yake ya kuisimamia serikali kwa kutaka kumuwajibisha rais, swali hapa jee Bunge letu hili la Ndugai lingeweza?,

mfano mzuri kabisa ni katiba imeruhusu mikutano ya siasa nchi nzima, rais Magufuli kazuia mikutano hiyo kinyume cha katiba, chama makini cha upinzani Chadema kipo bungeni, lenye uwezo wa kulishughulikia hili, kule kwenye bungeni kwenye uwezo, hawashughuliki, Chadema walitaka kulishughulikia kwa kufanya mikutano na maandamano nchi nzima as if uvunjivu wa katiba unashughulikiwa kwa mikutano na maandamano!, juzi hapa siku ya Uhuru, Mwenyekiti Mbowe, anapiga magoti kwa Magufuli kumuomba suluhu ya mazungumzo wakae mezani wazungumze!, haki ni right sio favour, haiombwi na hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa na ikibidi inapiganiwa!. kuhusu hili

Somo hili la Trump ni somo kubwa kwa Bunge letu na wabunge wetu wakiwemo wabunge mahiri na machachari kama Zitto na umachachari wa kwenye twitter lakini mule Bungeni kwenye the right forum yuko kimya!.

Siku nimekutana na Zitto mahali, nilimpa za uso kuhusu hili by telling him to his face
P.
 
jamaa yako nani? Pascal hawezi kwenda maana yeye ni CCM...
Pascal tupe
Pascal achana na hizo za Trump kwani hao hawana Demokrasia kama yetu cha muhimu hebu leta za Mlimani City vipi jamaa yetu kapenya?
Hili ni bandiko la Trump, za Mlimani City tukutanie kule, tujifunze kuheshimu mabandiko ya watu kwa kujadili mada iliyo mezani, mada hapa ni bunge la wenzetu linatimiza role yake ya kuisimamia serikali kwa kutaka kumuwajibisha rais, swali hapa jee Bunge letu hili la Ndugai lingeweza?,

mfano mzuri kabisa ni katiba imeruhusu mikutano ya siasa nchi nzima, rais Magufuli kazuia mikutano hiyo kinyume cha katiba, chama makini cha upinzani Chadema kipo bungeni, lenye uwezo wa kulishughulikia hili, kule kwenye bungeni kwenye uwezo, hawashughuliki, Chadema walitaka kulishughulikia kwa kufanya mikutano na maandamano nchi nzima as if uvunjivu wa katiba unashughulikiwa kwa mikutano na maandamano!,

juzi hapa siku ya Uhuru, Mwenyekiti Mbowe, anapiga magoti kwa Magufuli kumuomba suluhu ya mazungumzo wakae mezani wazungumze!, haki ni right sio favour, haiombwi na hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa na ikibidi inapiganiwa!. kuhusu hili Somo hili la Trump ni somo kubwa kwa Bunge letu na wabunge wetu wakiwemo wabunge mahiri na machachari kama Zitto na umachachari wa kwenye twitter lakini mule Bungeni kwenye the right forum yuko kimya!.

Siku nimekutana na Zitto mahali, nilimpa za uso kuhusu hili by telling him to his face
p
 
Pascal na wenzie walisema pandikizi lipewe ili pawe na uhai CDM na bila hivyo chama kinakufa sasa Mbowe kachaguliwa sijui huko kufa kupo stage gani sasa hivi ndicho ninachomuuliza ingawa yeye hujitanabaisha kuwa hana chama kama mimi nilivyo
Mkuu Kite Muganga, with due respect, naomba heshimu mada iliyopo mezani!, jikite kwenye mada!.
P
 
Pascal Mayalla,
Huwa nakuelewa lakini wengi huwa hatukuelewi sasa sijui ukoje wewe kwani ukivaa kombati unakuwa Mayalla Mayalla kweli na pindi ukitoa kombati unarudi kuwa kuwa Pascal yule wa kabla ya kwenda kusalimia Idodomya....kikubwa mkuu ni katiba inayokata kama msumeno bila kuangalia huyu ni msukuma au mchaga au anatoka chama gani
 
Back
Top Bottom