Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Hahaaaaa...... ama kweli wewe ndo Jambazi. lol...
 
Kujituma kwa mke wa mtu, hilo wazolo wallah ni batili
Kamwe ndugu usithubutu, kama muungwana nia yako badili
Umuwache mke wa mtu, mimi moto ndiye mume halali,
Preta wangu mahamumu, Achana na hawa walowezi.

Mpenzi Preta chunga sana, usijentupa kisa hawara,
Hao ni walaghai sana, katu haiwaishi mikwara,
Kwa hadaa hodari sana, angalia usije pata hasara,
Preta wangu mahamumu, Achana na hawa walowezi,

Preta wewe ndo wangu malkia, hata King'asti anajua hilo,
Watu8 mtani chonde shuhudia, pia mod Mexen Melo,
Hatukuanza kwa kuotea, kitambo tumelianza jambo,
Preta Wangu mahamumu, Achana na hawa walowezi.

Preta wewe ni kichuna wangu, wa milele na hata enzi,
Wewe ni mwandani wangu, chonde usigawe langu penzi,
Umekuwa mboni yangu, yadharau yao mabenzi,
Preta wangu mahamumu, Achana na hawa walowezi.
 
PakaJimmy... I learned something new about you, brother!. Kukuchokonoa wewe huko unakojificha ni kuanzisha thread ya kumsema Preta!. Unaibuka mara moja... Happy new year bana!. Hivi huyu Preta ndo huyo kwenye hako ka picha?.
 
hii ngoja nijaribu kwa beki tatu, baadae...
 
hii kweli sherehe imevamiwa na ngedere!!
 
PakaJimmy... I learned something new about you, brother!. Kukuchokonoa wewe huko unakojificha ni kuanzisha thread ya kumsema Preta!. Unaibuka mara moja... Happy new year bana!. Hivi huyu Preta ndo huyo kwenye hako ka picha?.
Mkuu Yegomasika
Salaam Mkuu wangu.
Hakika ni siku nyingi sasa zimepita kiongozi.
Naamini uko vizuri. Mambo ya maisha yanatupoteza kwenye ramani mkuu!.. Ila nimepata taarifa za uwepo wa thread inayomtaka Preta kwa udi na uvumba, nikaona hebu nije nitazamie, maana kabinti tumekalea wenyewe, sasa ni lazima tushuhudie uondokaji wake. Tunataka kaende kwa heshima japo kidogo Mkuu!
Hivi Mkuu ulinambia umeshaoa, au bado?...Haka kabinti kapo singo, na hiyo ndiyo picha yake halisi.
Mana sasa naona huyu, sijui Hunter, sijui Vampaya bado haeleweki!
Ukipita Arusha siku moja tafadhali sana nijuze nikuonyeshe dhahabu hiyo ilipo!...Utafurahi!
 
Uwiii! Mbona wagombea mnaongezeka kwa kasi wakati Lubuva ameshatangaza majina rasmi ya wagombea?
 


Umevamia uwanja, una kasi na pupa
Utaja pakwa wanja, uishie kula mifupa
Nakukata kwa kwanja, nakuweka kwenye chupa
Dirisha la maombi limefungwa, jaribu kwa lara 1!

Wadai mefunga ndoa, hujawahi enda ibadani
Historiayo ina doa, hujulikani bomani
Hapa nakuchojoa, uchi mtupu sokoni
Hiyo ndoa umefungia wap?

Haupo kwake moyoni, acha turushe ndoana
Preta mekuja sokoni, rijali tunachuana
Hakujui hata usoni,wadai mumeoana
Hiyo ndoa ya ndotoni, imefutika baada ya kuamuka

Ni bora mie mlowezi, Tengeru mi mhamiaji
Wewe sifa yako wizi, mesomea ukabaji
Nzito hoja huziwezi, kwangu hoja ni kipaji
Mie mlowezi na mhamiaji, popote atakapoenda Preta, nitamfuata.

Nakupeleka India, uone mbili kwa moja
Waume huridhia,wao wawili mke mmoja
Japo spendi kuchangia, kwa Preta tajikongoja
Kama hutaki kula na wenzio, basi susa wengine tufaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…