Nkungulume
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 2,987
- 1,209
Acheni fitina mtu ameandaa uzi maalum kwa ajili ya preta na ninyi mnachombezea hapo hapoPreta nijibu pm yangu sim yako haipo hewani kwenye airtel money yako nimekutumia Million 7 kwaajili ya dinner ya kesho!! ooh sorry nimekumbuka ulinitumia email uliniambia kile ki Benz kipya kina slow pancha kipaki kuna ki Rolls Royce new model nimekiagiza Marekani moja kwa moja! Halafu weekend hii nadhani tutakuwa Dubai kwa ya matembezi!!
Hakuna kilichoharibika ...Acheni fitina mtu ameandaa uzi maalum kwa ajili ya preta na ninyi mnachombezea hapo hapo
Lara 1 waru waru, hakuna asojua.Umevamia uwanja, una kasi na pupa
Utaja pakwa wanja, uishie kula mifupa
Nakukata kwa kwanja, nakuweka kwenye chupa
Dirisha la maombi limefungwa, jaribu kwa lara 1!
Wadai mefunga ndoa, hujawahi enda ibadani
Historiayo ina doa, hujulikani bomani
Hapa nakuchojoa, uchi mtupu sokoni
Hiyo ndoa umefungia wap?
Haupo kwake moyoni, acha turushe ndoana
Preta mekuja sokoni, rijali tunachuana
Hakujui hata usoni,wadai mumeoana
Hiyo ndoa ya ndotoni, imefutika baada ya kuamuka
Ni bora mie mlowezi, Tengeru mi mhamiaji
Wewe sifa yako wizi, mesomea ukabaji
Nzito hoja huziwezi, kwangu hoja ni kipaji
Mie mlowezi na mhamiaji, popote atakapoenda Preta, nitamfuata.
Nakupeleka India, uone mbili kwa moja
Waume huridhia,wao wawili mke mmoja
Japo spendi kuchangia, kwa Preta tajikongoja
Kama hutaki kula na wenzio, basi susa wengine tufaidi.
Lara 1 waru waru, hakuna asojua.
Mtanie auto baru, ngebe zitakuishia.
Preta Fundi subaru, moto nimejipatia.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Ndoa sio bomani, hili neno shika.
Ndoa sio Kanisani, Bali Moyoni hushika.
Moyo huwa shakani, mke wa mtu ukishika.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Acha kujikweza Mlowezi, yatakushinda mbeleni.
Preta wangu humwezi, utashushwa kulingeni
Preta mali ya mkwezi, Mlowezi taishia kutamani.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Lara moja kweli waru, tena sana mtandaoni
Mkali ka mtoza ushuru, tuli awapo nyumbani
Katu sitoe udhuru, akufaa kitandani
Lala 1 saizi yako, muache wangu Preta
Simba akiwa kimya, huyo mzee kibogoyo
Waweza hata kumfinya, amebakia poyoyo
Hathubutu kumung'unya, japo tamani kwa moyo
Simba ninaemjua, ana sauti nzito haendi kimyakimya
Sasa kura na ipigwe, sera zifike tamati
Heshima na irejeshwe, bila tumia manati
Preta piga hawa mawe, ikibidi kiberiti
Preta chagua wako mwandani, kura yako naitaka
Asije tokea Jecha, walahi sitakubali
Hapa pote patachacha, eleweni tafadhali
Nasubiri usiku kucha, matokeo ya halali
Preta piga kura sasa, ufukuze mamluki
Bado bado hamjamsisimua Preta. Endeleeni mpk mmoja ashinde. Vampire kashakimbia sijui au ligi imemshinda. Mpo vizuri wakuu
Yo most welcome sirAny one in arusha??on my way there!!
Lara moja kweli waru, tena sana mtandaoni
Mkali ka mtoza ushuru, tuli awapo nyumbani
Katu sitoe udhuru, akufaa kitandani
Lala 1 saizi yako, muache wangu Preta
Simba akiwa kimya, huyo mzee kibogoyo
Waweza hata kumfinya, amebakia poyoyo
Hathubutu kumung'unya, japo tamani kwa moyo
Simba ninaemjua, ana sauti nzito haendi kimyakimya
Sasa kura na ipigwe, sera zifike tamati
Heshima na irejeshwe, bila tumia manati
Preta piga hawa mawe, ikibidi kiberiti
Preta chagua wako mwandani, kura yako naitaka
Asije tokea Jecha, walahi sitakubali
Hapa pote patachacha, eleweni tafadhali
Nasubiri usiku kucha, matokeo ya halali
Preta piga kura sasa, ufukuze mamluki
Lara 1 waru waru, hakuna asojua.
Mtanie auto baru, ngebe zitakuishia.
Preta Fundi subaru, moto nimejipatia.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Ndoa sio bomani, hili neno shika.
Ndoa sio Kanisani, Bali Moyoni hushika.
Moyo huwa shakani, mke wa mtu ukishika.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Acha kujikweza Mlowezi, yatakushinda mbeleni.
Preta wangu humwezi, utashushwa kulingeni
Preta mali ya mkwezi, Mlowezi taishia kutamani.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Penzi halipigiwi kura, ndugu Macho fumbua.
Usilete mikwara ya chura, koo lisije kupasukia.
Hata Ulete zako kakara, katu sintokimbia.
Mwanaume rijali, lara hato mkimbia.
Kwa Kuwa wewe mawenge, lara awe lako chaguo.
Umfikishe kunako kilinge, kama sio mume Mzinguo.
Umuwache Preta aringe, mimi ndiye lake chaguo.
Kuku wangu mwenyewe, kwanini kura ipigwe.
Kura asiliye politiki, Preta sio ngumbaru.
Hutomshawishi rafiki, hata iwe sukari guru.
Hata Ulete unafiki, atakususa ka kaburu.
Preta wangu wa enzi, kura alishapiga kitambo.
Hakuna Lubuva wa Jecha, matokeo anayo Preta.
Nafsiyo inakupekecha, mwenzio nina peta,
Wakesha Macho kufikicha, mimi ngoma ninakokota.
Preta wangu umeambika, poyoyo denda zawatoka
Kura kupiga muhimu, sitake ushindi mezani
Ngoja nikupe Elimu, nikurudishe darasani
Ili atoe utamu, ajiridhishe moyoni
Kura tunapiga kila siku, sio tu siasani. Kupiga kura ni kuamua.
Wasopenda piga kura, wamezoea urithi
Hawachelewi kufura, wakikosa vya mirathi
Hawawezi kuchakura,wanapiga tu hadithi
Ukizoewa vya kunyonga, kuchinja hutaweza
Preta chonde naomba, fanya uamuzi sasa
Wameshaanza kugomba, mtego wao sijanasa
Mafuriko tanisomba, nkiambulia garasa
Preta njoo, ukate mzizi wa fitna sasa hivi
Wawili tu tumebaki, Vampire limekimbia
Amua tukate keki, nianze kushangilia
Mashabiki siwataki, sije anza niibia
Amua haraka sana kabla Vampire_hunter hajarudi
Kuna wajinga wamevamia, huu uzi bila kujua
Preta mi ndo ananizimia, moyoni kwake nimetulia
Anasubiri kunivulia, penzi aweze npatia
Nampa vitu mpaka analia, dozi inamuingia
Wewe ndo muongo, wadai umeshapewa
Kaka yako Mhe Muhongo, madaraka amelewa
Kwa makini yangu bongo, wewe ni wa kubezwa
Kama umeshapewa, hapa watafuta nini?
Hujapewa asilani, punguza zako hadaa
Hapa walilia nini, kwakweli nakushangaa
Umekula cha gizani, ambacho hajaandaa
Kama angekuwa amekuonjesha, mngeyamaliza kwa pm
Kijana huna staha, watangaza ya chumbani
Hilo halina msamaha, metolewa shindanoni
Preta hapendi karaha, omba japo msamaha
Umemkosea Preta adabu kwa kudai umeonja
Preta mpe atakaye sitiri, mambo yako ya chumbani
Huyu mvivu kufikiri, yote weka hadharani
Hawezi kutunza siri, ujana mwingi kichwani
Hufai kupewa huba kama huwezi mwenzio kumsitiri
Penzi si soko la hisa, kwamba kila mtu aone
Kijana punguza visa, ama kweli kua uyaone
Rudia nkupe vitasa, piga mpaka ukome
Rudi jandoni, ukafundwe staha
Habari wakuu,
Mimi ni mgeni humu naomba knena. . Sorry nimesahau U hapo kwenye knena. . . Ilitakiwa kuwa kunena, yaani kuongea....
Naomba nitumie fursa hii adhwiim na jukwaa lenu kumtongoza binti mrembo aitwaye Preta ...
Maana pm kwake zipo nyingi kiasi hatapay attention kwangu...Naomba wengine muwe watazamaji ispokuwa kwa anayejijua mtaalam wa kutongoza namruhusu anisaidie...
Preta my love, naomba uwe serious apa uache yale majibu yako yakiboya...
Please, njoo mpnz
Preta vp mbona kimya??