Prigozhin na Wagner yake asitisha uasi

Prigozhin na Wagner yake asitisha uasi

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073
Asubuhi ya kuamkia leo dunia nzima imekubwa na taharuki baada ya jeshi binafsi la WAGNER lililo chini ya ndigu Prigozhin liliasi na kuvamia mji wa Rostov nchini urusi na kutwaa makao makuu ya jeshi katika mkoa huo.

Licha ya kutwaa mkoa bado vikosi vyake vilianza kufanya misafara ya kutaka kuelekea Moscow.

Hatimae jioni hii bwana Evgene Prigozhin amekubali kusitisha zoezi hilo(uasi) na Kuna mazungumzo yamefanyika kwa wqpiganaji wake wote kupewa ulinzi na kutochukuliwa hatua yoyote.

Habari hii inaweza kua mbaya kwa mahasimu wa Putin na Russia kwani walishaanza kushehrekea na kujua rasmi Putin ameanguka.

Miongoni mwa makubaliano ya Prigozhin na serikali ya Moscow ambayo yameratibiwa na raisi wa Belarus (Lukashenko)

1. Waziri wa ulinzi na maafisa kadhaa kujiuzulu( Prigozhin amekua akiwashutumu mara kadhaa kua wanazuia ufanisi wa vita huko Ukraine)

2. Wqpiganaji wote wa WAGNER- PMC kupewa ulinzi dhidi ya hatua za kinidhamu.

3. Prigozhin asilimia kubwa jeshi lake litahuska na masuala ya Afrika hapo baadae,ikumbukwe WAGNER wapo Senegal, Jamhuri ya Afrika ya kati pia!!

Clips za wanajeshi wa WAGNER wakijiandaa kuondoka Rostov.

Update-
Prigozhin kuhamia nchini Belarus.

Rasmi Kremlin imesema kua wanajeshi walioshiriki kwenye "uasi" hawatoshitakiwa kwa makosa ya uharifu.

Wanajeshi wa WAGNER ambao hawakushiriki kuajiriwa kwa mikataba na wizara ya ulinzi.

NB- vikosi vya usalama vya Urusi huko mjini St Petersburg vilifanya upekuzi makao makuu ya Wagner,baadhi ya vitu walivyokuta vikiwa mali binafsi za Prigozhin.
20230624_221008.jpg

20230624_221044.jpg

Update 2.
Prigozhin akiondoka makao makuu ya jeshi mkoani Saratov pamoja na wqpiganaji wake,amepewa guarantee ya ahadi ya usalama wake kusafiri mpaka nchini Belarus.
20230624_233046.jpg

vita ina drama hatari. ila mbona mapema wanakubali yaishe.
Kitendo alichofanya ni hatari sana na hata kama NATO/USA wakisema wanamuunga mkono,just imagine Russia kama angeamua kutumia nguvu zake zote,ikiwemo silaha za nyuklia ama kutumia washirika wake kutoka Belarus, Chechen, Dagestan etc.

All in all,mwisho wa Prigozhin umefika,amevuka mipaka, suluhu pekee kwake ni kukimbia USA apewe hifadhi ya kisiasa na ukibaraka!!
 
Wewe nae,akimbilie US wakati kule anatafutwa na FBI.
 
Yes, hapo hakuna kumaliza ujinga kama huo kirahisi namnahiyo, labda kama walipanga pamoja kuzingua watu tu, vinginevyo mmoja katiya Putin ama huyo Prigozhn lazima ataondoka Russia kwa style yotote, akiwa mzima ama ubongo imesimama.
 
Wewe nae,akimbilie US wakati kule anatafutwa na FBI.

Kwa alichokifanya,lazima kina mkono na USA/NATO. Leo mjini Moscow raia walianza kupigiwa simu na unknown caller zikiwataka wananchi kuunga mkono uasi na wajitokeze kuandamana. Prigozhin hana nguvu hiyo peke yake, kumbuka hata UKRAINE kwenye vita anasaidiwa na Moscow.
 
Kitendo alichofanya ni hatari sana na hata kama NATO/USA wakisema wanamuunga mkono,just imagine Russia kama angeamua kutumia nguvu zake zote,ikiwemo silaha za nyuklia ama kutumia washirika wake kutoka Belarus, Chechen, Dagestan etc.

All in all,mwisho wa Prigozhin umefika,amevuka mipaka, suluhu pekee kwake ni kukimbia USA apewe hifadhi ya kisiasa na ukibaraka!!
Mbona wanasema Putin ndo kaomba poo
 
Huo ulikuwa ni mchezo wa Russia, baada ya hapa wasaliti halisi waliojipendekeza nadhani wataliwa vichwa.
 
Back
Top Bottom