Prime minister wa Zanzibar akihutbia UN Dec 1963

Prime minister wa Zanzibar akihutbia UN Dec 1963

Bin Faza

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
502
Reaction score
191
Wana JF

Kwa wale wasioijuwa zanzibar vyema, mumebahatika sana kupata darsa hili leo

Hiyo hapo chini ni hutuba ya Prime Minister wa zanzibar Mhe Mohammed Shamte akihutumia Umoja wa Maitaifa 1963,

Kwa taarifa yenu tu, kiti cha UN cha zanzibar kikalipo, nyerere alisahau kukifuta au hakuweza kukifuta kwasababu muungano wake na karume haukuwa wa mkataba kwahivo bado kiti cha znz

Bendera ya znz yenye karafuu munaioan hapo

kipo
 
Last edited by a moderator:
Mnh! Mheshimiwa ni katika serikali gani hiyo? Maana ktk kumbukumbu zangu serikali halali ya wazanzibari iliumdwa mwaka 1964 Baada ya mapinduzi matukufu ya January 12, mwaka 1964, unajua hadi Leo Palestina wanapigania kiti UN? Kwa kuwa siyo taifa huru?
 
Mnh! Mheshimiwa ni katika serikali gani hiyo? Maana ktk kumbukumbu zangu serikali halali ya wazanzibari iliumdwa mwaka 1964 Baada ya mapinduzi matukufu ya January 12, mwaka 1964, huyu waziri mkuu anayeongea mbele ya rais ni Wa serikali ipi? Na alikuwa anaongea mbele ya rais Yupii? Au katibu mkuu Wa UNO? Na akiiwakilisha serikali ya nani? Unajua hadi Leo Palestina wanapigania kiti UN? Kwa kuwa siyo taifa huru?

Ama kweli muheshimiwa wewe huna kumbu kumbu, kwahisani yako funguwa tena vitabu ikiwa huna bora uulize

Au tuseme kuna mushkila kidogo wa kilugha umeshindwa kumuelewa Ex-Mhe Prime Minister wa Zaiznabr huru anazungumzia nini?

AU NDIO JAZBA AS USUAL ............????????????????
 
Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yalifanyika mwaka 1964 chini ya uongozi wa Field Marshall Okello.Bwana shamte alikuwa akiwakilisha serekali ya kidhalimu ya kisultan.
 
Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yalifanyika mwaka 1964 chini ya uongozi wa Field Marshall Okello.Bwana shamte alikuwa akiwakilisha serekali ya kidhalimu ya kisultan.

Saa nyengine nyinyi watanganyika wana CCM munatufanya tujiulize, ivi mumesoma shule zipi? munajuwa tofauti baina ya mchana na usiku?

Hebu kada Ngongo ninatumai, ninadhani, ninafikiri kwamba kwa unajuwa tofauti baina ya UHURU NA MAPINDUZI?

ikwezekana usike jazba zako za kawaida.
 
Mwanzisha uzi mmbishi kweli, kumbe Shamte alikua chini ya Sultani? Naomba kujua, huyu mara baada ya mapinduzi alikua upande gani? Kama ndio lengo lenu kurudisha usultani Zanzibar endeleeni ila chonde chonde, ugaidi hatuupendi huku, msije mkatutengenezea wakimbizi wengine tena, WaCongo, Rwanda na Burundi wanatosha.
 
Kinachoisumbua Zanzibar ni Uarabu na Uafrika. Pro-Arabs (Wazanzibari) (akina Maalim Seif) hawataki Muungano while Pro-Africans (Wazanzibara) ndio wanaotaka Muungano! Otherwise, inakuwaje mtu mzima na akili zake kumtetea kibaraka wa Sultani Mohamed Shamte?
 
Watanganyika wengi wameugua maradhi ya malaria sugu ndio maana uwezo wao wa kufikiri unakuwa mdogo na obama kesho kutwa anawaletea vyandarua,hivi pale UN unaweza kuiwakilisha nchi bila ya nchi?shamte yupo pale kuiwakilisha jamhuri ya watu wa zanzibr.
 
Mnh! Mheshimiwa ni katika serikali gani hiyo? Maana ktk kumbukumbu zangu serikali halali ya wazanzibari iliumdwa mwaka 1964 Baada ya mapinduzi matukufu ya January 12, mwaka 1964, huyu waziri mkuu anayeongea mbele ya rais ni Wa serikali ipi? Na alikuwa anaongea mbele ya rais Yupii? Au katibu mkuu Wa UNO? Na akiiwakilisha serikali ya nani? Unajua hadi Leo Palestina wanapigania kiti UN? Kwa kuwa siyo taifa huru?

Wewe ni kilaza mkubwa.unamacho lakini huoni.unamasikio lakini husikii.huna akili lakini unataka kufikiria mambo.what kind of person are you?jee unajua maana ya neno mapinduzi?jee unamjua huyo waziri mkuu alikuwa ana asili ya jamii gani na nani aliyepindulia mwaka 64?ukiyajibu maswali hao ndo utajua kama zanzibar imepata uhuru ama haikupata.kama wewe ni msomi speculate utapata jawabu litakalo kufurahisha.kama ni mwanafunzi wa kidato cha nne na cha sita hutoweza kujua ukweli wewe endelea na msimamo wako huo huo uliona.kwasababu jf siku hzi imevamia na form 4 and form 6 leaver.
 
Mazindu Msambule

Mwanzisha uzi mmbishi kweli, kumbe Shamte alikua chini ya Sultani? Naomba kujua, huyu mara baada ya mapinduzi alikua upande gani? Kama ndio lengo lenu kurudisha usultani Zanzibar endeleeni ila chonde chonde, ugaidi hatuupendi huku, msije mkatutengenezea wakimbizi wengine tena, WaCongo, Rwanda na Burundi wanatosha.

Kwa nyinyi watanganyika sulatan ni mbaya kwa sisi wazanzibari ni mzuri tena sana sana sana kupita kipimo,

leo hii ukiwauliza wazanzibari sio wazanzibara (wazanzibara waliletwa kufanya makazi tu) nani bora awe mtawala wa zanzibar....sultan au tanganyika....basi mia fil mia watachaguwa sulatan.

sisi wazanzibari hatusikii kama ni waafrika the way u ppl think u are

Kwa ufupi tu Mazindu Msambule, sisi wazanzibari hatuna problem na sulatan na hilo ninakuomba uwaambie watanganyika wenzako woooooooooote, tia magazeti kauli hiyo

Nyinyi watanganyika ni mahuluku shida tu, ugaidi wenu umo ndnai ya vyama vyenu vya siasa CCM, CDM na vitakavokuja baadae, humo ndio munamoteswa na kuuliwa huku munapiga makofi

Last ujuwe kila unaposoma makala zangu mimi kama mzanzibari ni PRO SULATAN 100% na hatutaki muungano na tanganyika

bora kutawaliwa na waarabu matajiri na wenye kujuwa thamani ya mali na vitu kuliko watanganyika masikini na wasiojuwa thamani ya mali na vitu................kazi yenu udini njaa tu..........
 
hapa ndio nimeelewa, asante kwa ufafanuzi.!!!
 
Huu ukoloni mweusi tumeshachoka nao,mzee kifimbo cheza katuletea umasikini+ufukara,tuachiwe tupumueeeeee...
 
bora kutawaliwa na waarabu matajiri na wenye kujuwa thamani ya mali na vitu kuliko watanganyika masikini na wasiojuwa thamani ya mali na vitu................kazi yenu udini njaa tu..........
Huyo bwana wenu sultani hatarudi kamwe! hata muungano ukivunjika hatarud, bora Tanganyika iitawale pemba kwa nguvu kuliko mwarabu kurudisha usultani wake!
 
Ama kweli muheshimiwa wewe huna kumbu kumbu, kwahisani yako funguwa tena vitabu ikiwa huna bora uulize

Au tuseme kuna mushkila kidogo wa kilugha umeshindwa kumuelewa Ex-Mhe Prime Minister wa Zaiznabr huru anazungumzia nini?

AU NDIO JAZBA AS USUAL ............????????????????

Mohammed Shamte Hamadi alikuwa Chief Minister wa Zanzibar kati ya June 5, 1961 na June 24, 1963.

Alikuwa Prime Minister kuanzia June 24, 1964 hadi January 12, 1964

Swali linakuja alitoa hiyo hotuba UN akiwa kama Chief Minister au Prime Minister?

Ukishajibu hili swali, then nitakuja na the very big big question.
 
Mnh! Mheshimiwa ni katika serikali gani hiyo? Maana ktk kumbukumbu zangu serikali halali ya wazanzibari iliumdwa mwaka 1964 Baada ya mapinduzi matukufu ya January 12, mwaka 1964, huyu waziri mkuu anayeongea mbele ya rais ni Wa serikali ipi? Na alikuwa anaongea mbele ya rais Yupii? Au katibu mkuu Wa UNO? Na akiiwakilisha serikali ya nani? Unajua hadi Leo Palestina wanapigania kiti UN? Kwa kuwa siyo taifa huru?

Huyu kamaa anaongea chini ya serikali ya zanzibar kwa kuwakilisha wazanzibari na sulatani wa zwazanzibar,hilo sio geni mfumo huo upo Uk,Nertherland,Scandinavia.

serikali anayoiwakilisha huyu jamaa ilichaguliwa kidemokrasi kwa kupigiwa kura na wazanzibar,hizo propaganda za kuwa serikali ilikuwa ya kisultatani hazaina msingi,Sultani wa zanzibar ana "Generation" zaidi ya kumi na moja(11) zanzibar,kuanzaia babu na babu mpaka akafika yeye kupewa usulatani

Karume kawa mtawala wa zanzibar hakuzaliwa zanzibar, hana hata generation moja zanzibar hana hata mojomba au shangazi zanzibar,Sasa Sultani wa zanzibar na karume nani mzanzibar nani ana haki ya kutawala zanzibar,kwa fikira zako kwanini Karume amekubali kuiunganisaha zanzibar na Tanganyika,jibu kwasababu aliuwa mgeni na alijua wazanzibari watamgeuka,kaa ufikiri kwanini mungano unapigwa na walio wengi zanzibar,jibu kwasababu wazanzibar hawakushirikishwa

kama mapinduzi yangefanyika Kwa wakait huu wa leo yangeitwa "genocide"
 
African American

Huyo bwana wenu sultani hatarudi kamwe! hata muungano ukivunjika hatarud, bora Tanganyika iitawale pemba kwa nguvu kuliko mwarabu kurudisha usultani wake!

wewe na fikra zako, yaani ni chaguo lako msikilazi......

sisi wazanizbar tukiponyoka katika makucha ya mkoloni weusi mwenye njaa, mambo yatakuwa tofauti. na wewe mtanganyika hutoweza kumzuia mzanzibari yoyote kurejea zanzibar, akiwa alikuwa mfalme au alikuwa raia...itakuwa ni juu ya waznaizbari kuamua hilo

Kuitawala pemba kwa nguvu njooni, mreno alishindwa hapa na akangolewa na mwarabu itakuwa nyinyi?????

kama unahisi ninamuona sulatan kuwa ni bwana wangu sawa lakini ninajuwa wazi kwamba zanzibar ikirejea katika hali yake ya zamani, wewe na watanganyika wenzako mutakuja zanzibar kutafuta kazi...............isipokuwa safari hii tutakuangalieni vuyema musije mukafanya mapinduzi mengine
 
Ni kweli siku hiyo Shamte alihutubia UN na ndiyo siku Zanzibar ilipojiunga na UN, ilikuwa December 16, 1963.

Lakini ni kweli pia kwamba Wednesday, May 06, 1964, sovereignity ya Zanzibar na Tanganyika zilifutwa rasmi na kiti cha Zanzibar na cha Tanganyika kwenye UN kikapotea kukawa na kiti kimoja tu cha Jamhuri ya Muungano.

Mleta mada inaelekea umejitahidi na kufanikiwa kuwakomba baadhi ya wachangiaji katika ujinga ulio nao wa kutoujua ukweli huu.

Cc: Bin Faza, Babuji, Ngongo, Zumbemkuu, Mazindu Msambule, Bobwe, Mandi, Idawa
 
Huyo bwana wenu sultani hatarudi kamwe! hata muungano ukivunjika hatarud, bora Tanganyika iitawale pemba kwa nguvu kuliko mwarabu kurudisha usultani wake!

hayo uliyoyazungumza ni "racism in reverse",sifikirii kama wazanzibar wanataka sultani arudi isipokuwa wanataka kurudisha hadhi yao irudi.usisahau kuwa utamaduni,mila na desturi za wazanzibar na watanganyika ni vitu viwili tafauti,jambo hilo ndilo linalowafanya wazanzibari wajione wako tafauti na wenzao wa bara na ndio wanatakake kuwa kivyao wapate kuendeleza utamaduni na mila zao zao
 
... sisi wazanzibari hatuna problem na sulatan ...Last ujuwe kila unaposoma makala zangu mimi kama mzanzibari ni PRO SULATAN 100% ...

Hata yeye alipokimbia mara ya mwisho alisema "if my people want me back I will certainly go"

[video=youtube_share;7kTuy1cY5GA]http://youtu.be/7kTuy1cY5GA[/video]
 
Back
Top Bottom