Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?

Kwenye kutangaza matokeo ya mitihani ya taifa lazima kuwe na utaratibu mzuri unaozingatia kulinda faragha za watahiniwa.

Tumeshaona kabisa kuwa kuna watu wanatumia matokeo ya baadhi ya wanafunzi kuwasimanga, kuwakebehi, kuwakejeli, na hata kuwatukana hao wanafunzi pamoja na familia zao.

Nani anapenda hayo yote yamtokee? Na si tu yanamuumiza mwanafunzi bali pia yanaumiza familia yake. Kwa nini kusiwe na utaratibu wa kutumia namba badala ya majina?

Sasa hivi yeyote yule mwenye hila anaweza kwenda kwente tovuti ya NECTA na kudadisi matokeo ya yeyote yule na kuanza kumchafua. Hii si vyema kabisa. Ulazima wa kubadili utaratibu wa kuchapisha majina na matokeo ya mitihani upo.
Mking'ang'ana matokeo ya mitihani yafanywe siri mtaona watakaojiunga na A-LEVEL na hatimae VYUO VYA ELIMU YA JUU ni akina nani. Mimi nataka uwazi zaidi hata kwenye SIASA. "Private lives" za wanaotaka kuwa VIONGOZI wetu zianikwe hadharani.
 
Usiri huu mnaoung'ang'ania ndio umetufikisha hapa kwa mambo mengi. Viongozi wetu kutaja mali ni siri. Mikataba na wageni ni siri. Magonjwa ya akina Mwakyembe na Mwandosya ni siri lakini tunawatibu kwa kodi zetu. Kuanguka kwa JMK ni siri. Haya bwana.

At least hawa wanakuwa wamekubaliana na masharti ya uongozi kuwa atatakiwa kutaja mali alizonazo, je kwenye matokeo kuna hicho kitu?! Au tunawaonea kwa kuwa hawazijui sheria! Unamlazimisha matokeo yake yajulikane na hata wasiohusika ili iweje? Wilcat please bana, hebu kwa fair eh! Wildcate umefeli uanikwe hadharani?!
 
Mking'ang'ana matokeo ya mitihani yafanywe siri mtaona watakaojiunga na A-LEVEL na hatimae VYUO VYA ELIMU YA JUU ni akina nani. Mimi nataka uwazi zaidi hata kwenye SIASA. "Private lives" za wanaotaka kuwa VIONGOZI wetu zianikwe hadharani.

Matokeo ya mtihani ya mtu hayana uhusiano wowote na uwazi.

Unataka kujua matokeo ya mtu ili iweje? Unanufaika na nini?

Au moja ya manufaiko ni kufurahia kuona kama hivi mtoto wa Kikwete kapata alama za chini na kuanza kudhihakiwa yeye na familia yake? Unayafurahia hayo?
 
Mkuu ukiwa mwanaharakati mzuri huwezikosa namba ya mtihani ya unayemkuisudia! Na hapo ndo unapoonekana mkali aisee. Asikwambie mtu kuvumbua namba ya mtihani ya mtu ni sifa kubwa kuliko kuvumbua jina kitu ambacho ukitype tu kwenye google unapata!
 
Ungejisikiaje kama records zako zote za hospitali zingewekwa kwenye mtandao for the public to view?
Mkuu wangu wengi tungekimbilia kwa waganga wa kienyeji kwa kuwa wao huwa wanatoa neno moja tu lenye comfort: kila mtu ataambiwa UMELOGWA!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Matokeo ya mtihani ya mtu hayana uhusiano wowote na uwazi.

Unataka kujua matokeo ya mtu ili iweje? Unanufaika na nini?

Au moja ya manufaiko ni kufurahia kuona kama hivi mtoto wa Kikwete kapata alama za chini na kuanza kudhihakiwa yeye na familia yake? Unayafurahia hayo?
Kuna tatizo gani kutangaza matokeo haya? Mitihani inafanyika hadharani. Angalia jinsi "interview" za kutafuta AJIRA zinavyofanywa siri na matokeo yake. Wanaajiriwa hata ambao "interview" hawakufanya!
 
nirudie tena katiba chini ya article 16 imetoa mwongozo wa kuanzisha sheria maalumu data protection laws ambayo ingeanzisha data protection authority, poa muelewe sio kila kitu ni privacy kama sheria imeruhusu jambo kwa minajili fulani kama kutoa matokeo kwa njia ya mtandao au magazeti, kwa tanzania sio kila mtu ana acess na mtandao ndio maana wanatumia magazeti.labda mtu aibuke na ishu ya kwann wasiweke number tu badala ya majina,na kama sheria ilioruhusu nacta kufanya hivo imeanishwa basi hawezi kufungua kesi ya privacy
jiulizeni data zenu nlizotoa wkt mnaandikisha simcard zinalindwaje?ukifungua account benki nako data zako zinalindwaje+ je mtu wa benki hawezi kuzitumia against you kwa profit? nk
tukishakuwa na sheria hiyo basi tutaelewa wazi na pia kama necta wanatoa matokeo na majiba bila sheria inayowaruhusu kufanya hivo ndio unaweza kufungua kesi kuwashtaki ktk data protection authority na sio mahakama

Article 16(1) and (2) of United Republic of Tanzania Constitution of 1977 as amended form time to time provides for right to privacy. Article 16(2) of URT constitution provides for possibility of other laws to encroach the right to privacy. The said article stipulates clearly that the law maker will enact law to stipulate how privacy right may be protected, pursued or encroached by government agents.Unfortunately this requirement has not been put into implementation.
 
Wildcat hakuna ubaya kutangaza Matokeo, yatangazwe but kwa kutumia namba za watahiniwa za mitihani si namba na majina.
 
Usiri huu mnaoung'ang'ania ndio umetufikisha hapa kwa mambo mengi. Viongozi wetu kutaja mali ni siri. Mikataba na wageni ni siri. Magonjwa ya akina Mwakyembe na Mwandosya ni siri lakini tunawatibu kwa kodi zetu. Kuanguka kwa JMK ni siri. Haya bwana.

Mkuu hatuongelei usiri (secret) hapa. Tunaongelea privacy. Kuna tofauti kati ya usiri na faragha. Ni vitu viwili tofauti. The most obvious way to distinguish privacy from secret is to think about your bathroom habits. Mkuu even when you're around people you love and you're intimate with, you would still close the door when you're planning to sit on the toilet. There's no deception as to what you're doing in there with the door shut. You'd just like to poop in peace without an audience. Don't you? In that case, you're asking for privacy, not secrecy.

Assuming by "usiri" you meant privacy una maana kwamba medical records zote za Wildcard ziwekwe kwenye mitandao so EMT na wana JF wengine wazijue? Wewe ukienda Muhimbili kutibiwa si unatibiwa pia na kodi zetu pia? Is this a justification kuwa tujue unaumwa nini? Kwa vile ni kodi zetu basi rusksa madaktari ku-publish records zako ili ku-compensate kodi zetu?

So, for you it is right for:
  • Songea-based health system to post the medical records of thousands of patients on the Internet for you mlipa kodi to see?
  • An employee of Mwanyanala hospital to take a computer disk containing the names of 4,000 people who had tested positive for HIV, the virus that causes AIDS and put them on the internet?
  • WildCard, a patient at Temeke hospital, to discover that his/her medical record had been read by more than 200 of the hospital's employees?
  • A woman from Dodoma who had her doctor perform some routine tests, she received a letter from a drug company promoting a treatment for her high cholesterol?
  • Kwamba ni ruksa TIGO kumtumia WildCard SMS za TIGOPROMO usiku wa manane ukiwa umelala?
  • That in the new Constitution we should abandon the right to privacy altogether?
  • Kwa kwamba ni ruksa polisi kufanya haya?
  • UDSM1.jpg
 
Mkuu ukiwa mwanaharakati mzuri huwezikosa namba ya mtihani ya unayemkuisudia! Na hapo ndo unapoonekana mkali aisee. Asikwambie mtu kuvumbua namba ya mtihani ya mtu ni sifa kubwa kuliko kuvumbua jina kitu ambacho ukitype tu kwenye google unapata!
Tuyafanye siri mambo haya tutakapokuwa na utunzaji mzuri wa rekodi zetu tangu mtu anapozaliwa. Kwa sasa acha tuanikane wazi kabisa. Tuwawezeshe RITA kuweka kumbukumbu zetu zikae vizuri. Baada ya hapo tufanye siri mambo mengi tu.
 
Siku zote mlikua wapi msilione na kulilalamikia hili? Mmeanza kulalamika baada ya mwanaasha kuumbuliwa! Mi nasema hivi sheria ni msumeno inakata pande zote si matokeo ya watoto wakina yakhe yakianikwa mnachukulia poa ila ya watoto wa vigogo mnang'aka! Matokeo yawekwe hadharani ili kesho na kesho kutwa MWANAASHA AKIWA MENEJA WA BOT TUWEZE KUMNG'OA KIRAHISI kwa historia ya elimu yake,
 
nirudie tena katiba chini ya article 16 imetoa mwongozo wa kuanzisha sheria maalumu data protection laws ambayo ingeanzisha data protection authority, poa muelewe sio kila kitu ni privacy kama sheria imeruhusu jambo kwa minajili fulani kama kutoa matokeo kwa njia ya mtandao au magazeti, kwa tanzania sio kila mtu ana acess na mtandao ndio maana wanatumia magazeti.labda mtu aibuke na ishu ya kwann wasiweke number tu badala ya majina,na kama sheria ilioruhusu nacta kufanya hivo imeanishwa basi hawezi kufungua kesi ya privacy
jiulizeni data zenu nlizotoa wkt mnaandikisha simcard zinalindwaje?ukifungua account benki nako data zako zinalindwaje+ je mtu wa benki hawezi kuzitumia against you kwa profit? nk
tukishakuwa na sheria hiyo basi tutaelewa wazi na pia kama necta wanatoa matokeo na majiba bila sheria inayowaruhusu kufanya hivo ndio unaweza kufungua kesi kuwashtaki ktk data protection authority na sio mahakama

Aksante kwa kuliweka wazi ishu si kutangaza matokeo ishu ni kutangaza matokeo kwa kuanika mnajinahalisi ya watahiniwa. Si walitoa namba za mitihani? Kilamtahiniwa anajua nambayake kwa nini wasiyatoe kwa kuainisha na namba?
 
Ungefikiria vyema tangia NECTA wameanza kutoa majina ya watu siyo leo kwa vile mtoto wa Jeykey au Pombe kafeli ndiyo privacy isisitizwe.
Mleta mada kauliza kama huyo binti anaweza kuishtaki NECTA ila siyo wanafunzi wote. Siku zote tulikuwa wapi kufikiria kuna breach of privacy?
Angefaulu huyo binti, tungesisitiza hiyo privacy? Hayo mengine uliyoongelea kuhusu utamaduni ndiyo hivyo mkuu!

Moja ya alama ya jamii inayoendelea ni kubadilika kadiri wakati unavyokwenda. Labda mjadala huu umechelewa, na tumeuchelewesha sisi tunoamini katika privacy.

Na labda kujadili jambo hili la privacy kwa thread ya "mtoto wa rais" kunaweza kutoa picha kwamba "tunamtetea mtoto wa rais". Ukweli ni kwamba mtu yeyote anayenifuatilia maandishi yangu atajuwa simfagilii Kikwete.

Lakini je, tuache kutetea core principles za privacy eti kwa sababu tu hatukuwahi kuongelea tangu mwanzo? Hivi ukikuta jambo baya linafanyika, na limefanyika miaka mingi, utaacha kusema hili ni jambo baya kwa sababu tu limefanyika siku nyingi na hukusema?

Kama nilivyosema mwanzo, jambo la kuanika mitihani sikulifurahia tangu enzi zile tunaenda kuangalia majibu shuleni. Lakini labda siku zile hatukuwa na muamko sana, na zaidi ya hapo wengine tulikuwa tuko sana katika furaha ya kupasua kiasi hatukujali mengine. Na isitoshe hakukuwa na mtandao unaoonyesha majibu haya kwa kiasi cha leo.

Baraza la mitihani limeanza kuanika mtandaoni majibu miaka michache iliyopita, kwa hiyo hatujachelewa sana. It's not like it has been this way for fifty years. Na hata ingekuwa kwa fifty years, longevity does not make a wrong a right.

Naomba tuache kuiangalia hii issue kama ya binti wa Kikwete, tuangalie ufanisi wa system nzima, tuangalie stigma, tuangalie kwamba mfumo mzima wa kutahini mtu kwa siku moja na kumbandika daraja analokaa nalo kwa misha yote ni mbovu kama ule mfumo wa kumtahini mtu na kumpa "IQ" na kusema huyu ni "genius" na huyu bongolala.

But I know a lot of y'all are swimming in these bongo waters without realizing that you are swimming. Kwa hiyo kuhubiri privacy kwa wabongo ni kama kutaka kumwambia mtoto mdogo "unahema hewa", anaweza kukuuliza "iko wapi, mbona siioni?" . Kwa sababu iko so ubiquitous hata hawezi kuiona.

Lack of privacy is equally ubiquitous in bongo.

Watu ambao wanaulizana "marital status" kwenye kuomba kazi - kazi ambazo hazina uhusiano wowote na marital status- bila kushangaa hilo, utategemeaje washangae matokeo ya mtihani kuwa public?
 
Tuyafanye siri mambo haya tutakapokuwa na utunzaji mzuri wa rekodi zetu tangu mtu anapozaliwa. Kwa sasa acha tuanikane wazi kabisa. Tuwawezeshe RITA kuweka kumbukumbu zetu zikae vizuri. Baada ya hapo tufanye siri mambo mengi tu.

Aksante Mkuu.
 
Kuna tatizo gani kutangaza matokeo haya? Mitihani inafanyika hadharani. Angalia jinsi "interview" za kutafuta AJIRA zinavyofanywa siri na matokeo yake. Wanaajiriwa hata ambao "interview" hawakufanya!

Umeziona threads zote zilizoanzishwa zinazohusiana na matokeo ya huyo binti? Kama umeziona, yaliyoandikwa humo nayo umeyasoma? Na kama umeyasoma, wewe unayaonaje? Yanastahili au hayastahili?

Usaili wa kutafuta ajira katika sekta za umma hautakiwi ufanywe uwe siri. Mchakato mzima wa ajira za umma unatakiwa uwe ni wa uwazi na huru kwa sababu Watanzania wote wanashikilia dau katika umma wao.
 
Siku zote mlikua wapi msilione na kulilalamikia hili? Mmeanza kulalamika baada ya mwanaasha kuumbuliwa! Mi nasema hivi sheria ni msumeno inakata pande zote si matokeo ya watoto wakina yakhe yakianikwa mnachukulia poa ila ya watoto wa vigogo mnang'aka! Matokeo yawekwe hadharani ili kesho na kesho kutwa MWANAASHA AKIWA MENEJA WA BOT TUWEZE KUMNG'OA KIRAHISI kwa historia ya elimu yake,

Hii haijaathiri mtoto wa Kikwete tu.

Kuna dada na kaka zetu kibao wanakosa amani kwa stigma ya "kafeli", wamejifungia hata kutoka nje wanaona noma sasa kwa sababu kila mtu mwenye mtandao anawagoogle tu.

Hii si fresh.
 
Mkuu hatuongelei usiri (secret) hapa. Tunaongelea privacy. Kuna tofauti kati ya usiri na faragha. Ni vitu viwili tofauti. The most obvious way to distinguish privacy from secret is to think about your bathroom habits. Mkuu even when you're around people you love and you're intimate with, you would still close the door when you're planning to sit on the toilet. There's no deception as to what you're doing in there with the door shut. You'd just like to poop in peace without an audience. Don't you? In that case, you're asking for privacy, not secrecy.

Assuming by "usiri" you meant privacy una maana kwamba medical records zote za Wildcard ziwekwe kwenye mitandao so EMT na wana JF wengine wazijue? Wewe ukienda Muhimbili kutibiwa si unatibiwa pia na kodi zetu pia? Is this a justification kuwa tujue unaumwa nini? Kwa vile ni kodi zetu basi rusksa madaktari ku-publish records zako ili ku-compensate kodi zetu?

So, for you it is right for:
  • Songea-based health system to post the medical records of thousands of patients on the Internet for you mlipa kodi to see?
  • An employee of Mwanyanala hospital to take a computer disk containing the names of 4,000 people who had tested positive for HIV, the virus that causes AIDS and put them on the internet?
  • WildCard, a patient at Temeke hospital, to discover that his/her medical record had been read by more than 200 of the hospital's employees?
  • A woman from Dodoma who had her doctor perform some routine tests, she received a letter from a drug company promoting a treatment for her high cholesterol?
  • Kwamba ni ruksa TIGO kumtumia WildCard SMS za TIGOPROMO usiku wa manane ukiwa umelala?
  • That in the new Constitution we should remove the right to privacy altogether?
Unayoyaeleza hapa ni mambo ambayo yanatoka ndani ya mtu. Hayo kwa kweli yanahitaji usiri wa kutosha. Mitihani, interview za ajira, kufunga ndoa, kugombea UONGOZI, ... Haya hayahitaji usiri wowote hasa kwa Tanzania hii ambayo usiri kidogo tu mambo yanapindishwa kwelikweli!
 
Naona bado huelewi tofauti ya usiri na faragha!
 
Hata kama disclosure ya majina isingekuwa wazi, huyo mtoto alikuwa anasoma pekee darasani? Hapana!! Basi hao wanafunzi wenzie wangeyajua matokeo yake, na kwa sababu ni mtoto wa MKULU, habari ya UFAULU wake ingesambaa kama moto wa nyika. Jamani tuwe wakweli, mimi mwenyewe mwanangu kapata Div IV ya pt.31 sasa niende mahakamani kwa sababu matokeo yake yamebandikwa mtandaoni?? Hapana. KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA!! Awe mtoto wa Mkulu ama wangu mimi, awe kasoma FEDHA (Sorry FEZA) ama Nsyasya (kama huyu wa kwangu). Tafakari, Chukua Hatua!!
 
Back
Top Bottom