Ungefikiria vyema tangia NECTA wameanza kutoa majina ya watu siyo leo kwa vile mtoto wa Jeykey au Pombe kafeli ndiyo privacy isisitizwe.
Mleta mada kauliza kama huyo binti anaweza kuishtaki NECTA ila siyo wanafunzi wote. Siku zote tulikuwa wapi kufikiria kuna breach of privacy?
Angefaulu huyo binti, tungesisitiza hiyo privacy? Hayo mengine uliyoongelea kuhusu utamaduni ndiyo hivyo mkuu!
Moja ya alama ya jamii inayoendelea ni kubadilika kadiri wakati unavyokwenda. Labda mjadala huu umechelewa, na tumeuchelewesha sisi tunoamini katika privacy.
Na labda kujadili jambo hili la privacy kwa thread ya "mtoto wa rais" kunaweza kutoa picha kwamba "tunamtetea mtoto wa rais". Ukweli ni kwamba mtu yeyote anayenifuatilia maandishi yangu atajuwa simfagilii Kikwete.
Lakini je, tuache kutetea core principles za privacy eti kwa sababu tu hatukuwahi kuongelea tangu mwanzo? Hivi ukikuta jambo baya linafanyika, na limefanyika miaka mingi, utaacha kusema hili ni jambo baya kwa sababu tu limefanyika siku nyingi na hukusema?
Kama nilivyosema mwanzo, jambo la kuanika mitihani sikulifurahia tangu enzi zile tunaenda kuangalia majibu shuleni. Lakini labda siku zile hatukuwa na muamko sana, na zaidi ya hapo wengine tulikuwa tuko sana katika furaha ya kupasua kiasi hatukujali mengine. Na isitoshe hakukuwa na mtandao unaoonyesha majibu haya kwa kiasi cha leo.
Baraza la mitihani limeanza kuanika mtandaoni majibu miaka michache iliyopita, kwa hiyo hatujachelewa sana. It's not like it has been this way for fifty years. Na hata ingekuwa kwa fifty years, longevity does not make a wrong a right.
Naomba tuache kuiangalia hii issue kama ya binti wa Kikwete, tuangalie ufanisi wa system nzima, tuangalie stigma, tuangalie kwamba mfumo mzima wa kutahini mtu kwa siku moja na kumbandika daraja analokaa nalo kwa misha yote ni mbovu kama ule mfumo wa kumtahini mtu na kumpa "IQ" na kusema huyu ni "genius" na huyu bongolala.
But I know a lot of y'all are swimming in these bongo waters without realizing that you are swimming. Kwa hiyo kuhubiri privacy kwa wabongo ni kama kutaka kumwambia mtoto mdogo "unahema hewa", anaweza kukuuliza "iko wapi, mbona siioni?" . Kwa sababu iko so ubiquitous hata hawezi kuiona.
Lack of privacy is equally ubiquitous in bongo.
Watu ambao wanaulizana "marital status" kwenye kuomba kazi - kazi ambazo hazina uhusiano wowote na marital status- bila kushangaa hilo, utategemeaje washangae matokeo ya mtihani kuwa public?