Nafikiri kuna wachache wanaoielewa hii mada
Mwanajamiione nafikiri issue kubwa hapa ni Je huyu binti anaweza kuisue NECTA for breach of her privacy as per the constitution of the URT
Kwa majibu ya watu wengi ni No kwa kuwa NECTA imeanzishwa kwa sheria ya bunge ambalo limeipa mamlaka kufanya mambo yote na kuregulate masuala yote yanayohusiana na mitihani
Bile vile NECTA imepewa mamlaka ya kujitungia sheria zake ( regulations) kuregulaet day to day activities za Baraza
Chini ya mamlaka hayo ililopewa chini ya sheria za kuanzishwa kwake ni kwamba baraza lisimamie mitihani, lisimamie usahihishaji wa mitihani husika na kutangaza matokeo
Utangazaji wa matokeo huo kwamba utangazwe kwa wahusika kwa mujibu wa sheria zilizounda baraza ambapo Baraza litatangaza kwa namna litakayoona inafaa na bila kuathiri sheria au kanuni nyingine yoyote.
Consitution of the URT ina kifungu kinachosema kuwa privacy ya mtu izingatiwe ila ukienda mbali zaidi Article 30 ya the same Consitution inasema kuwa na hapa nanukuuu sehemu yake:-
Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 34 ya 1994 ib. 5
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya.......
NECTA ina sheria yake na kanuni zake ambazo zinalifanya baraza hilo kuendesha shughuli zake bila kuathiri au kuingilia mambo mengine na sheria hiyo haijaharamisha au kuvunja kipengele chochote na imepitishwa na Bunge kuwa sheria na inalipa baraza mamlaka ya kufanya jambo lolote ambalo halivunji wala kuharamisha jambo lolote
Kusema kuwa kutangaza matokeo kwa njia wanayotumia NECTA ni kuvunja sheria au kuingilia uhuru wa watu ni kinyume maana sheria ya kuanzishwa kwake inalipa baraza kufanya jambo lolote ambalo linaonekana na linafaa kutfanywa na baraza na halivunji sheria yoyote. Ngalia hapa chini mamlaka ya baraza:-
Powers and duties of Council Acts Nos. 4 of 1987 Sch.; 2 if 1998 Sch.
(1) The Council shall have power to do things and to act in all ways necessary for, or incidental to the purposes for which it is established.
(2) In particular and without prejudice to the generality of subsection (1), but subject to the provisions of subsection (4), the Council shall have power–
(a) to administer the properties of the Council both movable and immovable;
(b) to administer the funds and other assets of the Council;
(c) to signify the acts of the Council by use of the common seal;
(d) subject to the provisions of this Act, to appoint any officers of the Council whom it may deem necessary;
(e) to review regulations relating to examinations;
(f) to consider and approve subjects suitable for examination;
(g) to appoint panels or boards of examiners;
(h) to enter into arrangements, whether reciprocal or otherwise, with other persons or organisations, whether within or outside the United Republic, for the recognition of awards granted in respect of examinations falling within their respective responsibilities;
(i)
to do all other acts and things which may be provided for in this Act or which may be prescribed.
Hapo unaona kufanya jambo lolote liliruhusiwa chini ya sheria ya kuanzishwa kwake ikiwemo kutangaza matokeo kwa namna itakayoona inafaa na iliyopitishwa na sheria ya kuanzishwa kwake au kwa njia yoyote itakayoona inafaa
So tuseme wazi kuwa sijaona sehem yoyote ambapo Baraza limeenda kinyume cha Sheria au kanuni za kuanzishwa kwake mpaka lifikie kushtakiwa kuwa limeingilia privacy ya mtu