Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?

Privacy Law: Mwanaasha J. Kikwete kuwashitaki NECTA?

tena mimi nimuombe mama salma kuwa kwa sasa amwangalie sana Ali.....la asivyo waaibika sana na hao watoto wao!!!
Kuna huyo mmoja ambae anasoma Botswana ndiyo nunda kabisa sijui atavuna nini nashangaa huyu Mwanaasha kuchemka alikuwa vizuri sana kipindi yuko shule ya msingi…….
 
Mkuu Edson..unakaa Urisino au Maeneo Ya Regent nini?...maana unaongea vitu vya ukweli sana...na s ALi tu hata Yule Khalifani na Khalifa pamoja na Rashidi Chodo aanze kuwaangalia sasa...ila mama Salma si mwalimu kwann anashindwa kuwa na watoto karibu ili awasimamie katika ELIMU?



haha....mkuu hii famillia naifahamu kwa uzuri sana we acha tu.....mengine tukiyasema hapa utasikia tume inaundwa.....kwa kifupi mama yao aangalie sana tena haka ka mwanaasha haka asipokaa sawa kitamletea mjukuu fasta.......
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
Mkuu uko sahihi kabisa. Issue ni faragha ya mtu. Nadhani hii itawafumbua macho NECTA na come next year watakuwa wamejirekebisha. Waanze kutumia namba na siyo majina. Zile namba wanazopewa wanafunzi zinakuwa zina maana gani? Pia matumizi ya ICT nadhani yapo chini sana. Miaka ya huko nyuma NBAA nasikia nao walikuwa wakiwaanika wazee wazima wakiwa wamezungusha wakati wengi wao walikuw ni mabosi, baadaye ikabidi jamaa wabadili na kuanza kuweka namba tu.

Faragha muhimu jamani. Hata humu ndani ya JF tunajitutumua na kuwasema watu openly kwa sababu tuna faragha.
 
Kuna huyo mmoja ambae anasoma Botswana ndiyo nunda kabisa sijui atavuna nini nashangaa huyu Mwanaasha kuchemka alikuwa vizuri sana kipindi yuko shule ya msingi…….[/QUO]

tena kana maneno machafu na kiburi ka cha rizone....huyo ndo atataga kabisa........
 
Hata bila NECTA kutoa matokeo haya hadharani, JF wangeyakosa?

Inawezekana wasingeyakosa, lakini kama JF ingeyapublish hapa then wangepelekwa mahakamani for breach of privacy. Lakini kwa sasa haiwezekani kwa sababu sheria ya privacy ni mbovu.
 
Mie issue yangu si mtoto wa Kikwete, ni lack of privacy kwa system nzima.

Kwa hiyo hata ingekuwa case ya Mwanaasha Kombo wa kutoka Handeni, the core issue ingebaki pale pale. Mtu kavunjiwa faragha yake, bila kujali mtu huyo ni nani.
Faragha kwenye mambo ya shule inaanzia wapi na kuishia wapi. Mtoto huyu tangu ameanza shule hakuna kilichofichwa kuhusu mambo yake ya darasani. Matokeo ya mitihani yake yote aloofanya tangu chekechea haijawahi kuwa siri. Na pengine kama aliwahi kufanya vizuri huko nyuma na zawadi alipewa kabisa. Iweje matokeo haya yafichwe?
 
Kwa mawazo yako mkuu yafanyweje
maana hata wangeandika no bado buku la matokeo linapatikana kwenye kila shule na mtu yoyote anaweza kwenda pale na kujionea
May be ungewashauri NECTA wawe na utaratibu wa kumtumia kila mwanafunzi matokeo yake kwenye private email yake au barua
na ujue sio wote wenye access na email au hata hizo barua

Hata huko mashuleni matokeo hayatakiwi kuwa kwenye vitabu kwa kila mtu kuona. Kwani kutangaza matokeo kunamsaidia nani?

Hapo ulipo una accounti za benki ambazo unazitumia kufanya more complicated transactions than exam results na bado benki hawatoi account information zako kwa public.
 
Ungefikiria vyema tangia NECTA wameanza kutoa majina ya watu siyo leo kwa vile mtoto wa Jeykey au Pombe kafeli ndiyo privacy isisitizwe.
Mleta mada kauliza kama huyo binti anaweza kuishtaki NECTA ila siyo wanafunzi wote. Siku zote tulikuwa wapi kufikiria kuna breach of privacy?
Angefaulu huyo binti, tungesisitiza hiyo privacy? Hayo mengine uliyoongelea kuhusu utamaduni ndiyo hivyo mkuu!

Ungejisikiaje kama records zako zote za hospitali zingewekwa kwenye mtandao for the public to view?
 
Faragha kwenye mambo ya shule inaanzia wapi na kuishia wapi. Mtoto huyu tangu ameanza shule hakuna kilichofichwa kuhusu mambo yake ya darasani. Matokeo ya mitihani yake yote aloofanya tangu chekechea haijawahi kuwa siri. Na pengine kama aliwahi kufanya vizuri huko nyuma na zawadi alipewa kabisa. Iweje matokeo haya yafichwe?

Jamani Wildcat matokeo yake ya chekechea umeyajuaje?
 
And... Has the law maker enacted laws specificaly prohibiting necta, or any other person, to place in public newspaper, or a website, public examination results of public or and private school? If yesn there is a case. If no, the is none!
 
Nafikiri kuna wachache wanaoielewa hii mada

Mwanajamiione nafikiri issue kubwa hapa ni Je huyu binti anaweza kuisue NECTA for breach of her privacy as per the constitution of the URT
Kwa majibu ya watu wengi ni No kwa kuwa NECTA imeanzishwa kwa sheria ya bunge ambalo limeipa mamlaka kufanya mambo yote na kuregulate masuala yote yanayohusiana na mitihani
Bile vile NECTA imepewa mamlaka ya kujitungia sheria zake ( regulations) kuregulaet day to day activities za Baraza
Chini ya mamlaka hayo ililopewa chini ya sheria za kuanzishwa kwake ni kwamba baraza lisimamie mitihani, lisimamie usahihishaji wa mitihani husika na kutangaza matokeo
Utangazaji wa matokeo huo kwamba utangazwe kwa wahusika kwa mujibu wa sheria zilizounda baraza ambapo Baraza litatangaza kwa namna litakayoona inafaa na bila kuathiri sheria au kanuni nyingine yoyote.
Consitution of the URT ina kifungu kinachosema kuwa privacy ya mtu izingatiwe ila ukienda mbali zaidi Article 30 ya the same Consitution inasema kuwa na hapa nanukuuu sehemu yake:-
Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6; 34 ya 1994 ib. 5
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya.......

NECTA ina sheria yake na kanuni zake ambazo zinalifanya baraza hilo kuendesha shughuli zake bila kuathiri au kuingilia mambo mengine na sheria hiyo haijaharamisha au kuvunja kipengele chochote na imepitishwa na Bunge kuwa sheria na inalipa baraza mamlaka ya kufanya jambo lolote ambalo halivunji wala kuharamisha jambo lolote
Kusema kuwa kutangaza matokeo kwa njia wanayotumia NECTA ni kuvunja sheria au kuingilia uhuru wa watu ni kinyume maana sheria ya kuanzishwa kwake inalipa baraza kufanya jambo lolote ambalo linaonekana na linafaa kutfanywa na baraza na halivunji sheria yoyote. Ngalia hapa chini mamlaka ya baraza:-
Powers and duties of Council Acts Nos. 4 of 1987 Sch.; 2 if 1998 Sch.
(1) The Council shall have power to do things and to act in all ways necessary for, or incidental to the purposes for which it is established.
(2) In particular and without prejudice to the generality of subsection (1), but subject to the provisions of subsection (4), the Council shall have power–
(a) to administer the properties of the Council both movable and immovable;
(b) to administer the funds and other assets of the Council;
(c) to signify the acts of the Council by use of the common seal;
(d) subject to the provisions of this Act, to appoint any officers of the Council whom it may deem necessary;
(e) to review regulations relating to examinations;
(f) to consider and approve subjects suitable for examination;
(g) to appoint panels or boards of examiners;
(h) to enter into arrangements, whether reciprocal or otherwise, with other persons or organisations, whether within or outside the United Republic, for the recognition of awards granted in respect of examinations falling within their respective responsibilities;
(i) to do all other acts and things which may be provided for in this Act or which may be prescribed.



Hapo unaona kufanya jambo lolote liliruhusiwa chini ya sheria ya kuanzishwa kwake ikiwemo kutangaza matokeo kwa namna itakayoona inafaa na iliyopitishwa na sheria ya kuanzishwa kwake au kwa njia yoyote itakayoona inafaa
So tuseme wazi kuwa sijaona sehem yoyote ambapo Baraza limeenda kinyume cha Sheria au kanuni za kuanzishwa kwake mpaka lifikie kushtakiwa kuwa limeingilia privacy ya mtu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Faragha kwenye mambo ya shule inaanzia wapi na kuishia wapi. Mtoto huyu tangu ameanza shule hakuna kilichofichwa kuhusu mambo yake ya darasani. Matokeo ya mitihani yake yote aloofanya tangu chekechea haijawahi kuwa siri. Na pengine kama aliwahi kufanya vizuri huko nyuma na zawadi alipewa kabisa. Iweje matokeo haya yafichwe?

Kwenye kutangaza matokeo ya mitihani ya taifa lazima kuwe na utaratibu mzuri unaozingatia kulinda faragha za watahiniwa.

Tumeshaona kabisa kuwa kuna watu wanatumia matokeo ya baadhi ya wanafunzi kuwasimanga, kuwakebehi, kuwakejeli, na hata kuwatukana hao wanafunzi pamoja na familia zao.

Nani anapenda hayo yote yamtokee? Na si tu yanamuumiza mwanafunzi bali pia yanaumiza familia yake. Kwa nini kusiwe na utaratibu wa kutumia namba badala ya majina?

Sasa hivi yeyote yule mwenye hila anaweza kwenda kwente tovuti ya NECTA na kudadisi matokeo ya yeyote yule na kuanza kumchafua. Hii si vyema kabisa. Ulazima wa kubadili utaratibu wa kuchapisha majina na matokeo ya mitihani upo.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Uzuri wa JF ndio huu, ya kwamba pale watu wentgine hushinda kutazama hapa kuna vichwa ambavyo vinadiriki kwenda ndani zaidi ya maswala mazito na tukapata utetezi toka pande mbili tofauti..Kusema kweli nimefurahi sana kuona hoja hii japokuwa imetokana na mtoto wa rais. Inaonyesha unyonge wetu sisi wenyewe ktk kutafuta haki na na Uhuru wetu wenyewe isipokuwa pale wakuu zetu wanapohusika.

Hata hivyo, kuanika majina ya watoto ktk magazeti, mtandao na kadhalika ni kuvunja haki na Uhuru wa mtoto huyo ambaye bahati mbaya sheria haikumtazama yeye. Unapokwenda ktk gazeti na kutafuta majina ya watoto majirani au marafiki inakusaidia nini wewe msomaji?.. Hii inaonyesha wazi jinsi tulivyokuwa wadaku na tabia za kishenzi hadi ktk sheria zetu kutaka kujua mambo ya watu wengine wakati yetu wenyewe yametushinda.
 
Hata huko mashuleni matokeo hayatakiwi kuwa kwenye vitabu kwa kila mtu kuona. Kwani kutangaza matokeo kunamsaidia nani?

Hapo ulipo una accounti za benki ambazo unazitumia kufanya more complicated transactions than exam results na bado benki hawatoi account information zako kwa public.

Mkuu tunarudi pale pale
Sheria inayosimamia bank inasema wazi kuwa mambo yote yanayohusiana na account za mteja ni siri ya bank na mteja na hairuhusiwi kutolewa kwa mtu wa tatu ila kwa kibali cha mahakama
Sheria iliyoanzisha NECTA haijasema hayo wala hakuna kipengele kinachosema kuwa matokeo ya mitihani ni siri ya NECTA na mwanafunzi na hairuhusiwi kuyatoa
may be ipigwe kelele kuweka kipengele kuwa baraza haliruhusiwi kutangaza matokeo ya mtu yoyote bila ridhaa yake
 
Inawezekana wasingeyakosa, lakini kama JF ingeyapublish hapa then wangepelekwa mahakamani for breach of privacy. Lakini kwa sasa haiwezekani kwa sababu sheria ya privacy ni mbovu.
Usiri huu mnaoung'ang'ania ndio umetufikisha hapa kwa mambo mengi. Viongozi wetu kutaja mali ni siri. Mikataba na wageni ni siri. Magonjwa ya akina Mwakyembe na Mwandosya ni siri lakini tunawatibu kwa kodi zetu. Kuanguka kwa JMK ni siri. Haya bwana.
 
Hata huko mashuleni matokeo hayatakiwi kuwa kwenye vitabu kwa kila mtu kuona. Kwani kutangaza matokeo kunamsaidia nani?

Umenikumbusha enzi hizo primary matokeo ya mitihani ya kila mwanafunzi yalikuwa ni siri ya walimu na mwanafunzi husika. Utajua tuu matokeo ya mwanafunzi mwingine kama akiamua kukuonyesha. Matokeo ambayo yalikuwa yanajulikana ni yale tu ya wanafunzi waliokamata namba moja hadi tatu. Na hii ilikuwa ni kwa ajili ya kupewa zawadi kwa kufanya vizuri. Na tulikuwa hatuambiwi wamepata maksi gani kwenye kila somo. It was merely the overall pass.
 
Uzuri wa JF ndio huu, ya kwamba pale watu wentine hushinda kutazama hapa kuna vichwa ambavyo vinadiriki kwenda ndani zaidi ya maswala mazito na tukapata utetezi toka pande mbili tofauti..Kusema kweli nimefurahi sana kuona hoja hii japokuwa imetokana na mtoto wa rais. Inaonyesha unyonge wetu sisi wenyewe ktk kutafuta halkia na Uhuru wetu wenyewe isipokuwa pale wakuu zetu wanapohusika.

Hata hivyo, kuanika majina ya watoto ktk magazeti, mtandao na kadhalika ni kuvunja haki na Uhuru wa mtoto huyo ambaye bahati mbaya sheria haikumtazama yeye. Unapokwenda ktk gazeti na kutafuta majina ya waototo majirani au marafiki inakusaidia nini wewe msomaji?.. Hii inaonyesha wazi jinsi tulivyokuwa wadaku na tabia za kishenzi hadi ktk sheria zetu kutaka kujua mambo ya watu wengine wakati yetu wenyewe yametushinda.
Kaka Mkandara aksante sana. Nadhan mada imepotoshwa na mtoa mada kwa kuweka jina la mtoto wa mkuu. Pengine sehemu ya mwanaasha angeweka watahiniwa (ofcoz hapa angelenga aliofeli) ingeleta picha tofauti kidogo.

Hivi kwa nibni matokeo yanayobandikwa vyuoni mfano UDSM hubandikwa registration number and not names?! Nakumbuka kwa sie ambao hakukuwa na Zalongwa wala ARIS tulikuwa tunabandikiwa kwenye mbao za matangazo kama si kwenye kuta. Na ninaamini hata hao wanaotumia mitandao sasa hivi wanapewa Passwords ambazo zinawawezesha kuona matokeo ya mtahiniwa tu bila kuona ya wenzake. Au hii nayo haihusiani na privacy?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom