Private schools (English medium) ada kupanda maradufu 2023. Serikali iingilie kati

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
12,112
Reaction score
15,060
Serikali haina budi kufanya lolote liwezekanalo kufanya Shule hizi za private zisipandishe ada kiholela. Zinaweza zikapunguziwa gharama za uendeshaji ili ziwe na nafuu kwa malipo huko serikali.

Baadhi ya Shule vikao vishaanza. Kuna ongezeko la ada la kutisha na wanajiamulia wenyewe kwa utetezi kwamba gharama za maisha zimepanda. Sina shaka na hili kwani sote, ni mashahidi. Vitu havinunuliki.

Njia pekee ni serikali kuzipunguzia Shule hizi mzigo Wa kodi.

Sijui itakuwaje JANUARY!!? Au wazazi wenzangu mnasemaje!? Tupeleke watoto Kayumba!!!
 
Peleka Kayumba Mkuu usisahamu mnunulia kidumu na mfagio na bajeti ya mihogo kila siku TOFAUTI na hapo hutoboi there's high cost of living.
 
Nikimpeleka mwanangu primary za english medium mje mniite mbwa...

Hizo shule zinafanya mzazi usijue uwezo halisi wa mwanao maana kuna cream nyingi kwenye upande wa matokeo ili kuwafurahisha wazazi.

Ukipeleka mtoto shule za kawaida inasaidia kujua uwezo wake halisi ili ufanye maamuzi kuanzia O-Level umpe support ya aina gani, umuache shule za serikali ama umpeleke private.
 
Wewe uwezo ndo unao kusumbua tu hamna lolote sabb zako hazina mashiko
 
Duh!
 
Hizo shule ni Trap hizo.

Zinakufanya mzazi Unakuwa kwenye rat race miaka kibao.

Kama upo karibu na english medium zinazomilikiwa na serikali kama olimpio, mpeleke hizo maana ada zake ni nafuu na hazipandi kiholela.

Kama upo mbali peleka kayumba kisha pale pale shuleni kayumba ongea na mwalimu wake wa hesabu na kiingereza wa kila darasa lake uwe unampa vihela vya tution tu amsimamie mtoto akiwa shuleni. Akomae nae mwanzo mwisho

Kisha nyumbani muwekee mazingira mazuri ya kujifunza.. na ikiwezekana awe na private tutor wa kiingereza.

Maisha sio ada tu. Mtoto anahitaji urithi pia wa mali. Sasa kama mzazi unapoteza hela nyingi kwenye ada hizo mali utamuandaliaje?
 
Shule za serikali zipo ndugu
 
Serikalini hadi form six buree..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…